Katibu Msaidizi Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kati- Dodoma Bi. Jasmin Awadhi akitoa neno la utangulizi katika kongamano la siku ya Maadili na Haki za Binadamu. Kongamano hilo lilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Singida Disemba 10,2024.
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Jaji (Stahiki) Mathew Mwaimu akifungua kongamano la siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa ambalo limefanyika ukumbi wa PSSSF jijini Dodoma tarehe 10 Disemba, 2024. Mhe. Mathew ni mgeni rasmi wa kongamano hilo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (Mb) akiongea na waandishi wa Habari wakati akizindua Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa mwaka 2024. Hafla ya uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi tarehe 5 Disemba, 2024. Kulia kwa Mhe. Waziri ni Bw. Mululi Mahendeka, Katibu Mkuu Ikulu na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Jaji (Stahiki) Mathew Mwaimu.
Mgeni rasmi ambaye ni Katibu Ukuzaji Maadili kutoka Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw. Waziri Kipacha akifungua semina ya maadili iliyoandaliwa na klabu ya maadili ya Chuo cha Mipango. Semina hiyo ilifanyika kampasi ya chuo hicho eneo la Miyuji Kaskazini jijini Dodoma tarehe 16 Novemba, 2024.
Katibu Msaidizi Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Kanda ya Kaskazini Bw. Gerald Mwaitebele akiambatana na Afisa Maadili Bw. Tumaini Mgalla wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mogitu iliyoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, walipokuwa wanafungua Klabu ya Maadili kwa wanafunzi wa shule hiyo tarehe 12 Novemba 2024.
Ndugu Kiongozi, Sekretarieti ya Maadili inapokea Tamko la Raslimali, Maslahi na Madeni kwa njia ya mtandao (Online Declaration System-ODS.) kuanzia tarehe 1 Oktoba hadi 31 Disemba, 2024.
Afisa Maadili kutoka Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kanda ya kati- Dodoma Bw. Joshua Mwambande akiongoza kiapo cha Ahadi ya Uadilifu kwa viongozi kutoka Tume ya kurekebisha sheria. Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Tume ya kurekebisha sheria iliyopo katika Chuo kikuu cha Dodoma tarehe 13 Novemba,2024.
Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji (Mst) Sivangilwa Mwangesi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya awali kwa watumishi kutoka Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Mafunzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa Ofisi hiyo Jijini Dodoma tarehe 11 Novemba,2024. Kulia kwa Kamishna ni Katibu Idara ya Ukuzaji Maadili Bw. Waziri Kipacha na kushoto kwa Kamishna ni Katibu Idara ya Uzingatiaji Maadili Bw. Kassim Mkwawa.
Afisa Maadili kutoka Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kati Dodoma, Bi. Amina Muru akiongea na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mlimwa ya jijini Dodoma kuhusu umuhimu wa klabu za maadili baada ya kufika shuleni hapo Novemba 7, 2024.
Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Bw. Massaile Mussa akiwa katika picha ya pamoja na walezi wa Klabu za Maadili walioshiriki mafunzo ya walimu walezi wa Klabu za Maadili yaliyofanyika katika shule ya Sekondari Arusha tarehe 26 Agosti 2024