JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS – SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

Waziri Mkuu aitaka Sekretarieti ya Maadili kufanya marekebisho ya Sheria kujumuisha Watumishi wa sekta nyeti
11 Dec, 2025
Waziri Mkuu aitaka Sekretarieti ya Maadili kufanya marekebisho ya Sheria kujumuisha Watumishi wa sekta nyeti

Waziri Mkuu wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) ameiagiza Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kufanya marekebisho ya Sheria na Kanuni ili kujumuisha baadhi ya watumishi wa umma waliopo katika sekta nyeti kujaza fomu ya Tamko la Rasilimali na Madeni.

Mheshimiwa Nchemba ametoa agizo hilo tarehe 11.12.2025 jijini Dodoma alipofanya ziara ya kikazi katika Makao Makuu ya taasisi hiyo ili kujionea shughuli zinazotekelezwa na Sekretarieti ya Maadili na kutoa uelekeo wa maeneo yanayotakiwa kufanyiwa kazi.

Mhe. Waziri Mkuu alisema kuwa zipo baadhi ya sekta ama nyadhifa mbalimbali za watumishi ambazo ni kitovu cha ukiukwaji wa maadili unaosababisha upotevu na ubadhilifu wa fedha za Umma, lakini watumishi wa sekta hizo hawawajibiki na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Namba 13 ya mwaka  1995 inayowataka Viongozi wa Umma kujaza Fomu ya Tamko la Rasilimali na Madeni.

“Tunaweza kuwa tunatekeleza kikamilifu suala la usimamizi wa matamko kwa viongozi wa umma , lakini uhalisia wake masuala ya  ukosefu wa maadili yakaendelea nchini,” amesema na kuongeza kuwa, “maeneo ambayo fedha ya umma zinapotea ni manunuzi ya umma, eneo la makusanyo hasa watumishi wanaohusika na makadilio ya kodi, maafisa wanaohusika na mikataba, utoaji wa leseni za madini, sekta ya ardhi, wajumbe wa zabuni, ukaguzi na udhibiti hivi ndivyo vyanzo vikubwa vya upotevu wa fedha za Serikali,” ameeleza.

”Watumishi wa sekta hizi hawawawajibiki na Sheria ya Maadili kwa kujaza fomu ya Tamko la Rasilimali na Madeni wao wanatoa kiapo cha Ahadi ya Uadilifu ambacho hata asipokizingatia hakuna sheria inayombana hivyo, eneo hili liangaliwe kwa upana zaidi kwa kubadilishwa Sheria na kanuni ili nao wawajibike kwa sababu wapo katika nafasi zinazoshawishi upokeaji wa rushwa  kuliko hata viongozi wao wanaowasimamia,” alisema Mhe Waziri Mkuu.

“Fanyeni mapitio ya haraka ya sheria na kanuni ili watumishi hawa wajumuishwe katika kutoa Tamko la Rasilimali na Madeni. Hatuwezi kuendelea na utaratibu kwenye nchi ambayo kuna watu wenye uwezo wa kuchukua kitu kwa niaba ya watu wengine halafu na watu wengine wakawa wanaugulia maumivu.

Amesema, kwa jinsi inavyoweza kukidhi haja, liwe ni jambo linalohusu watumishi wa umma shirikisheni na vyombo vingine watawaambia maeneo viashiria vikubwa vya rushwa vilipo ili kule ambako rushwa imekithiri pafuatiliwe kwa karibu.

“Asilimia 76% ya fedha za serikali zimeelekezwa katika ununuzi wa vitu mbalimbali hapa ndipo eneo ambalo kuna mianya ya rushwa wahusika wanachukua fedha nyingi ambazo haziendi kwenye utekelezaji wa miradi ya serikali badala yake wanaweka mifukoni,  watumishi hawa wanapaswa kuangaliwa kwa jicho la karibu na Taasisi hii ili waweze kufuatiliwa na kuchunguzwa kwa kina namna ya utekelezaji wa majukumu yao,” alisema.

Mhe. Waziri Mkuu alieleza kuwa katika eneo ambalo Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania analitupia jicho ni eneo la uadilifu kwa Viongozi na Watumishi wa Umma. Mhe. Rais anataka kuona Viongozi na watumishi wa Umma wanawajibika katika maeneo yao ya kazi ili wananchi wanufaike na rasilimali zao.

Mhe. Waziri Mkuu alisema kuwa Sekretarieti ya Maadili ina majukumu kubwa, nyeti na mazito katika kuhakikisha kuwa rasilimali za nchi zinalindwa.

“Tunataka kuona Taasisi hii inakuwa  kimbilio kwa kila mtu anayeona kuna ukiukwaji wa maadili, kila mwananchi aamini kuwa akifika katika Taasisi hii atapata ufumbuzi wa changamoto yake hivyo, niwaase kusimamia maadili kwa kiwango cha juu. Mtu ambaye hataki kuwa na nidhamu binafsi, sisi Serikali tumlazimishe.

Katika ziara hiyo Mhe. Waziri Mkuu aliongozana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete (Mb) pamoja na Katibu Mkuu Ikulu Bw. Majula Mahendeka

 

 

Online Help
Kuanzisha Enzi Mpya katika Udhibiti wa Sekta ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania
Ofisi ya maadili inafanya kazi na imewashughulikia viongozi wengi sana kupitia Baraza la Maadili ambalo pia liliendeshwa mwaka 2013 Novemba mkoani Tabora. Viongozi mbalimbali waliokuwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili waliitwa kwenye Baraza na kuhojiwa na Baraza linatoa mapendekezo na kuyawasilisha mapendekezo hayo kwa Rais kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu na kisheria kwa viongozi husika.

" >
Kifungu cha 11(1) cha Sheria ya Maadili kimeainisha wazi mali zinazotakiwa kutajwa kuwa ni fedha taslimu, fedha zilizopo katika taasisi za kifedha kama vile benki, hisa, nyumba, mashamba, magari, mitambo na mali nyinginezo. Kiongozi anatakiwa kutoa tamko la mali anazomiliki yeye mwenyewe, mke/mume na watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane. Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni zinatakiwa kujazwa kila mwaka na kiongozi hutumiwa fomu hizo na Ofisi ya Maadili na pia zinapatikana katika mtandao wa maadili yaani www.ethicssecretariat.go.tz. Sheria inamtaka kiongozi kutolea tamko madeni yake ili kuweza kujua kuwa kiongozi anamiliki mali zipi na pia kutambua kuwa amezipata vipi mali hizo ukilinganisha na kipato cha kiongozi husika. Kiongozi kuwa na mali nyingi si dhambi kwani hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetamka wazi kuwa kila raia ana haki ya kumiliki mali ila ofisi inataka kujiridhisha uhalali wa jinsi mali ilivyopatikana. Mapendekezo katika Katiba mpya yanasisitiza maadili kwa kutenganisha uongozi na biashara.

" >
Wananchi wengi wamejijengea dhana kuwa bila pesa huwezi kupata huduma ya kiserikali kitu ambacho si kweli kwani huduma nyingi za kiserikali zinatolewa bure kabisa ila cha msingi wananchi wanatakiwa kutoa taarifa katika vyombo husika pindi wanapotakiwa kulipia huduma ambazo zinatolewa bure. Jamii inatakiwa kubadilika na kuamini kuwa si lazima kutoa rushwa ndipo upate huduma. Wapo wananchi wengi ambao walileta malalamiko kama hayo na Ofisi ya Maadili iliyashughulikia, hivyo wananchi wasisite kutembelea Ofisi zetu kwa ajili ya kutoa taarifa kama hizo.

" >
Kutoa lugha chafu ni ukiukwaji wa maadili. Ndani ya Bunge kuna Kamati ya Maadili ambayo ipo kwa ajili ya kuwawajibisha wabunge wanaotoa lugha chafu. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa upande wake ilifanya semina kwa wabunge ili kuwakumbusha mipaka ya utendaji kazi na maadili kwa ujumla, na tangu wakati huo matumizi ya lugha chafu bungeni yamepungua kwa kiasi kikubwa.

" >