
Jaji wa Rufani Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi
Kamishna wa Maadili
Wasifu
Latest Downloads
Tovuti Mashuhuri
Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
Kutoa lugha chafu ni ukiukwaji wa maadili. Ndani ya Bunge kuna Kamati ya Maadili ambayo ipo kwa ajili ya kuwawajibisha wabunge wanaotoa lugha chafu. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa upande wake ilifanya semina kwa wabunge ili kuwakumbusha mipaka ya utendaji kazi na maadili kwa ujumla, na tangu wakati huo matumizi ya lugha chafu bungeni yamepungua kwa kiasi kikubwa.
Wananchi wengi wamejijengea dhana kuwa bila pesa huwezi kupata huduma ya kiserikali kitu ambacho si kweli kwani huduma nyingi za kiserikali zinatolewa bure kabisa ila cha msingi wananchi wanatakiwa kutoa taarifa katika vyombo husika pindi wanapotakiwa kulipia huduma ambazo zinatolewa bure. Jamii inatakiwa kubadilika na kuamini kuwa si lazima kutoa rushwa ndipo upate huduma. Wapo wananchi wengi ambao walileta malalamiko kama hayo na Ofisi ya Maadili iliyashughulikia, hivyo wananchi wasisite kutembelea Ofisi zetu kwa ajili ya kutoa taarifa kama hizo.
Ofisi ya maadili inafanya kazi na imewashughulikia viongozi wengi sana kupitia Baraza la Maadili ambalo pia liliendeshwa mwaka 2013 Novemba mkoani Tabora. Viongozi mbalimbali waliokuwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili waliitwa kwenye Baraza na kuhojiwa na Baraza linatoa mapendekezo na kuyawasilisha mapendekezo hayo kwa Rais kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu na kisheria kwa viongozi husika.
Kifungu cha 11(1) cha Sheria ya Maadili kimeainisha wazi mali zinazotakiwa kutajwa kuwa ni fedha taslimu, fedha zilizopo katika taasisi za kifedha kama vile benki, hisa, nyumba, mashamba, magari, mitambo na mali nyinginezo. Kiongozi anatakiwa kutoa tamko la mali anazomiliki yeye mwenyewe, mke/mume na watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane. Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni zinatakiwa kujazwa kila mwaka na kiongozi hutumiwa fomu hizo na Ofisi ya Maadili na pia zinapatikana katika mtandao wa maadili yaani www.ethicssecretariat.go.tz. Sheria inamtaka kiongozi kutolea tamko madeni yake ili kuweza kujua kuwa kiongozi anamiliki mali zipi na pia kutambua kuwa amezipata vipi mali hizo ukilinganisha na kipato cha kiongozi husika. Kiongozi kuwa na mali nyingi si dhambi kwani hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetamka wazi kuwa kila raia ana haki ya kumiliki mali ila ofisi inataka kujiridhisha uhalali wa jinsi mali ilivyopatikana. Mapendekezo katika Katiba mpya yanasisitiza maadili kwa kutenganisha uongozi na biashara.
Chombo chenye mamlaka ya kutunga sheria ni Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Bunge kupitia wabunge wake ndio walihusika katika kutunga sheria hiyo na wananchi waliwakilishwa na wabunge wao.
Sheria imetaja pia mali za watoto wa kiongozi husika zinatakiwa pia kutolewa tamko na endapo kiongozi ataficha hizo mali basi sheria itachukua mkondo wake.
Utekelezaji wa Sheria ya Maadili unafuata Orodha ya viongozi wa Umma ambayo imeainishwa katika kifungu 4(1) cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Aidha, Mhe. Rais ameongeza orodha ya viongozi mwaka 2013.
Kifungu cha 6 cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma kimeorodhesha mambo ambayo kiongozi anatakiwa kuzingatia, pamoja na mambo mengine, kiongozi wa umma anatakiwa afanye kazi kwa uaminifu,huruma ,kujizuia na tamaa na kuzingatia viwango vya juu vya maadili ili imani ya wananchi na matumaini katika uadilifu, haki na kutopendelea kwa serikali vilindwe na kuimarishwa.
Sheria zipo na zinatakiwa kufuatwa, isipokuwa wananchi wanalalamika tu bila kupeleka malalamiko yao katika ofisi husika kama Ofisi za Maadili. Cha msingi wananchi wanatakiwa kupeleka malalamiko ya viongozi mbali mbali wanaokiuka maadili kwa kuwa wao ndio wako karibu na viongozi hivyo wanajua tabia na mienendo yao katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku. Wabunge wengi wamekuwa wakilalamikiwa kukiuka maadili kwa kuwa shughuli za Bunge zinaonekana moja kwa moja kupitia runinga, hivyo kuonekana kuwa wanaongoza katika kukiuka maadili lakini sio kweli, Ofisi imeshughulikia malalamiko mengi kutoka kwa wananchi dhidi ya viongozi mabali mbali na si wabunge na walikuwa na tuhuma nzito kuliko hata mabishano yanayotokea Bungeni.
Chombo chenye mamlaka ya kutunga sheria ni Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Bunge kupitia wabunge wake ndio walihusika katika kutunga sheria hiyo na wananchi waliwakilishwa na wabunge wao.