JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS – SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

Utoaji wa Matamko
Utoaji wa Matamko
  • Tunatoa Fomu ya Tamko la  Rasilimali,  Maslahi  na Madeni,  Fomu ya Tamko la Mgongano wa Maslahi, Fomu ya Tamko la Zawadi na Rejesta ya Zawadi wakati wote;
  • Tunatoa  fomu  au  barua  ya  kukiri  mapokezi  ya  Tamko  la  Rasilimali, Maslahi na Madeni la kila mwisho wa mwaka, ndani ya siku saba (7) za kazi;
  • Tunatoa  fomu  au  barua  ya  kukiri  mapokezi  ya  Tamko  la  Rasilimali, Maslahi na Madeni la mwanzo wa uongozi linalotolewa na Kiongozi ndani ya siku 30 baada ya kupata wadhifa, ndani ya siku saba (7) za kazi;
  • Tunatoa fomu au barua ya kukiri mapokezi ya Tamko la Mwisho wa kutumikia wadhifa linalotolewa na Kiongozi ndani ya miezi mitatu kabla ya kustaafu, ndani ya siku saba (7) za kazi;
  • Tunatoa barua ya kukiri mapokezi ya Tamko la Mgongano wa Maslahi ndani ya siku saba (7)  za kazi;
  • Tunatoa barua ya kukiri mapokezi ya Rejesta ya Zawadi ndani ya siku saba (7)  za kazi; na
  • Tunatoa barua ya kukiri mapokezi ya Tamko la Zawadi kutoka kwa wateja wa ndani, ndani ya siku tau (3) za kazi;
Online Help
Kuanzisha Enzi Mpya katika Udhibiti wa Sekta ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania
Ofisi ya maadili inafanya kazi na imewashughulikia viongozi wengi sana kupitia Baraza la Maadili ambalo pia liliendeshwa mwaka 2013 Novemba mkoani Tabora. Viongozi mbalimbali waliokuwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili waliitwa kwenye Baraza na kuhojiwa na Baraza linatoa mapendekezo na kuyawasilisha mapendekezo hayo kwa Rais kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu na kisheria kwa viongozi husika.

" >
Kifungu cha 11(1) cha Sheria ya Maadili kimeainisha wazi mali zinazotakiwa kutajwa kuwa ni fedha taslimu, fedha zilizopo katika taasisi za kifedha kama vile benki, hisa, nyumba, mashamba, magari, mitambo na mali nyinginezo. Kiongozi anatakiwa kutoa tamko la mali anazomiliki yeye mwenyewe, mke/mume na watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane. Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni zinatakiwa kujazwa kila mwaka na kiongozi hutumiwa fomu hizo na Ofisi ya Maadili na pia zinapatikana katika mtandao wa maadili yaani www.ethicssecretariat.go.tz. Sheria inamtaka kiongozi kutolea tamko madeni yake ili kuweza kujua kuwa kiongozi anamiliki mali zipi na pia kutambua kuwa amezipata vipi mali hizo ukilinganisha na kipato cha kiongozi husika. Kiongozi kuwa na mali nyingi si dhambi kwani hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetamka wazi kuwa kila raia ana haki ya kumiliki mali ila ofisi inataka kujiridhisha uhalali wa jinsi mali ilivyopatikana. Mapendekezo katika Katiba mpya yanasisitiza maadili kwa kutenganisha uongozi na biashara.

" >
Wananchi wengi wamejijengea dhana kuwa bila pesa huwezi kupata huduma ya kiserikali kitu ambacho si kweli kwani huduma nyingi za kiserikali zinatolewa bure kabisa ila cha msingi wananchi wanatakiwa kutoa taarifa katika vyombo husika pindi wanapotakiwa kulipia huduma ambazo zinatolewa bure. Jamii inatakiwa kubadilika na kuamini kuwa si lazima kutoa rushwa ndipo upate huduma. Wapo wananchi wengi ambao walileta malalamiko kama hayo na Ofisi ya Maadili iliyashughulikia, hivyo wananchi wasisite kutembelea Ofisi zetu kwa ajili ya kutoa taarifa kama hizo.

" >
Kutoa lugha chafu ni ukiukwaji wa maadili. Ndani ya Bunge kuna Kamati ya Maadili ambayo ipo kwa ajili ya kuwawajibisha wabunge wanaotoa lugha chafu. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa upande wake ilifanya semina kwa wabunge ili kuwakumbusha mipaka ya utendaji kazi na maadili kwa ujumla, na tangu wakati huo matumizi ya lugha chafu bungeni yamepungua kwa kiasi kikubwa.

" >