RATIBA YA MAFUNZO KWA VIONGOZI WA UMMA
Kwa kuzingatia misingi ya maadili iliyoainishwa katika Ibara ya 132 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995, ambayo yanamtaka kila kiongozi wa umma kuzingatia viwango vya juu vya maadili ili kukuza utu, uwazi, uadilifu, uwajibikaji na kuimarisha imani ya wananchi kuhusu utendaji wa viongozi wa umma; Ofisi ya Rais, Sekretariet ya Maadili ya viongozi wa Umma (ES) kwa ushirikiano na Chuo Cha Uhasibu Arusha (IAA) wameingia makubaliano (MoU) ya kutoa mafunzo, kufanya utafiti na ushauri kwenye masuala yahusuyo Maadili ya viongozi wa Umma. Kwa kuanzia, ES na IAA watatoa mafunzo kwa Viongozi wa Umma. Viongozi wanaohusika ni wale waliotajwa kwenye kifungu cha 4 cha sheria ya maadili ya viongozi wa umma, sura 398, kama ilivyofanyiwa marekebisho kupitia tangazo la Serikali na. 857 la tarehe 24/11/2023.
