JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS – SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

Wazazi, Walezi na Walimu watakiwa kukemea vitendo vya ukatili kwa Watoto Nchini
05 Dec, 2025
Wazazi, Walezi na Walimu watakiwa kukemea vitendo vya ukatili kwa Watoto Nchini

Wazazi, walezi na walimu nchini wametakiwa kukemea vitendo vya ukatili kwa watoto kwa kuwatunza na kuwalinda watoto kwa kuwapatia chakula, malezi bora. Muda wa kuzungumza nao na kuwaelekeza ikiwa ni pamoja na kusimamia matumizi ya simu, mitandao ya kijamii na kushiriki kikamilifu katika mikutano ya shule, vikao vya wazazi pamoja na programu za malezi nchini.

Wito huo umetolewa na Bw. Hamad Kaaya Katibu Tawala wa Wilaya kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mhe. Almishi Hazali alipokuwa akifungua Mdahalo kuhusu changamoto za kimaadili kwa wanafunzi na ufumbuzi wake uliofanyika tarehe 5 Disemba, 2025 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang.

Aidha Bw. Kaaya katika hotuba yake amezitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni pamoja na watoto wa shule kubakwa na wazazi na kumaliza kesi hizo nje ya mfumo pamoja na kukosa msaada rasmi wa sheria, watoto kutopata chakula cha mchana mashuleni, migogoro ya kifamilia, ulevi na wazazi kutengana, matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii jambo linalopelekea watoto kupotoshwa na maudhui ya ngono, ukatili, utapeli matusi na tabia zisizofaa.

Ameongeza kuwa changamoto nyingine zinazowakumba watoto ikiwa ni pamoja na ushawishi hasi wa makundi rika jambo linalopelekea watoto kuingizwa katika tabia kama utoro, uvutaji sigara, ulevi, na umalaya kwa watoto wa kike na changamoto nyingine ni pamoja na kukosekana kwa muda wazazi kujihusisha na malezi ya watoto wao

Aidha Bw. Kaaya amebainisha hatua za msingi zinazopaswa kuchukuliwa ili kuboresha maadili na kulinda watoto ikiwa ni pamoja na kuweka mkakati madhubuti wa kuripoti matukio ya ukatili na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria, kuzuia wazazi kumaliza kesi nje ya mfumo wa sheria. Kuimarisha ulinzi wa watoto mashuleni na katika jamii, kuzuia matumizi mabaya ya mitandao pamoja na kutoa elimu ya malezi bora kwa jamii.

Naye Katibu Msaidizi Sekreetarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya kaskazini Arusha Bw. Gerald Mwaitebele alitoa wito kwa wazazi, walezi na waalimu nchini kuhakikisha kuwa watoto wanasimamiwa kikamilifu ili kupambana na ukatili kwa watoto unaofanywa na watu wasiowaadilifu.

Kongamano hilo limefanyika ikiwa ni kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu Duniani ambayo hufanyika kila mwaka tarehe 10 Disemba.

Online Help
Kuanzisha Enzi Mpya katika Udhibiti wa Sekta ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania
Ofisi ya maadili inafanya kazi na imewashughulikia viongozi wengi sana kupitia Baraza la Maadili ambalo pia liliendeshwa mwaka 2013 Novemba mkoani Tabora. Viongozi mbalimbali waliokuwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili waliitwa kwenye Baraza na kuhojiwa na Baraza linatoa mapendekezo na kuyawasilisha mapendekezo hayo kwa Rais kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu na kisheria kwa viongozi husika.

" >
Kifungu cha 11(1) cha Sheria ya Maadili kimeainisha wazi mali zinazotakiwa kutajwa kuwa ni fedha taslimu, fedha zilizopo katika taasisi za kifedha kama vile benki, hisa, nyumba, mashamba, magari, mitambo na mali nyinginezo. Kiongozi anatakiwa kutoa tamko la mali anazomiliki yeye mwenyewe, mke/mume na watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane. Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni zinatakiwa kujazwa kila mwaka na kiongozi hutumiwa fomu hizo na Ofisi ya Maadili na pia zinapatikana katika mtandao wa maadili yaani www.ethicssecretariat.go.tz. Sheria inamtaka kiongozi kutolea tamko madeni yake ili kuweza kujua kuwa kiongozi anamiliki mali zipi na pia kutambua kuwa amezipata vipi mali hizo ukilinganisha na kipato cha kiongozi husika. Kiongozi kuwa na mali nyingi si dhambi kwani hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetamka wazi kuwa kila raia ana haki ya kumiliki mali ila ofisi inataka kujiridhisha uhalali wa jinsi mali ilivyopatikana. Mapendekezo katika Katiba mpya yanasisitiza maadili kwa kutenganisha uongozi na biashara.

" >
Wananchi wengi wamejijengea dhana kuwa bila pesa huwezi kupata huduma ya kiserikali kitu ambacho si kweli kwani huduma nyingi za kiserikali zinatolewa bure kabisa ila cha msingi wananchi wanatakiwa kutoa taarifa katika vyombo husika pindi wanapotakiwa kulipia huduma ambazo zinatolewa bure. Jamii inatakiwa kubadilika na kuamini kuwa si lazima kutoa rushwa ndipo upate huduma. Wapo wananchi wengi ambao walileta malalamiko kama hayo na Ofisi ya Maadili iliyashughulikia, hivyo wananchi wasisite kutembelea Ofisi zetu kwa ajili ya kutoa taarifa kama hizo.

" >
Kutoa lugha chafu ni ukiukwaji wa maadili. Ndani ya Bunge kuna Kamati ya Maadili ambayo ipo kwa ajili ya kuwawajibisha wabunge wanaotoa lugha chafu. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa upande wake ilifanya semina kwa wabunge ili kuwakumbusha mipaka ya utendaji kazi na maadili kwa ujumla, na tangu wakati huo matumizi ya lugha chafu bungeni yamepungua kwa kiasi kikubwa.

" >