Je Ofisi inatoa motisha wowote kwa wananchi ili watoe taarifa ya Viongozi wanaokiuka Maadili?
Je Ofisi inatoa motisha wowote kwa wananchi ili watoe taarifa ya Viongozi wanaokiuka Maadili?
Suala la maadili ni suala la tabia na linahitaji litoke ndani mwa mtu. Mtu mwenyewe atambue ubaya wa jambo analoliona na awe tayari kulitolea taarifa bila hata kupewa motisha wa fedha. Watu wote wawe tayari kutoa taarifa bila hata kupewa motisha wowote wakitambua kuwa kila mmoja analo jukumu la kulinda taifa letu.