Ofisi ya Maadili imewahi kuchukua hatua gani kwa viongozi wanaokiuka maadili. Mfano wa viongozi watatu ambao wamewahi kuwajibishwa na Ofisi ya Maadili?
Ofisi ya Maadili imewahi kuchukua hatua gani kwa viongozi wanaokiuka maadili. Mfano wa viongozi watatu ambao wamewahi kuwajibishwa na Ofisi ya Maadili?
Ofisi ya maadili inafanya kazi na imewashughulikia viongozi wengi sana kupitia Baraza la Maadili ambalo pia liliendeshwa mwaka 2013 Novemba mkoani Tabora. Viongozi mbalimbali waliokuwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili waliitwa kwenye Baraza na kuhojiwa na Baraza linatoa mapendekezo na kuyawasilisha mapendekezo hayo kwa Rais kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu na kisheria kwa viongozi husika.