Je kuna umuhimu wowotewa wananchi kujua Sheria ya Maadili na kama upo wanaipataje Sheria hiyo?
Kila mwananchi anatakiwa kuifahamu Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Kwa kuifahamu Sheria hiyo wataisaidia Ofisi kwa kutoa taarifa za ukiukwaji wa maadili unaofanywa na viongozi mbali mbali. Wananchi wanaweza kupata elimu ya maadili kupitia njia mbali mbali kama vile redio, semina na matukio ya kitaifa ambayo yanakusanya watu wengi kwa pamoja kwa mfano maadhimisho ya sherehe za wakulima nchini(nanenane) ambapo Ofisi ya Maadili huwa inatoa elimu kwa umma katika banda la maadili. Elimu inatolewa pia kupitia kipindi cha redio na kipindi maalum cha maadili kinachorushwa na Televisheni ya Taifa (TBC) siku ya Jumatatu na Star tv siku ya Jumanne kuanzia saa moja kamili hadi saa moja na nusu jioni. Hivyo, wananchi wanashauriwa wafuatilie ili kujifunza zaidi majukumu ya ofisi yetu.