Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Manungu ya wilayani Kongwa mkoani Dodoma Bw. Geofrey Fredrick akiongoza zoezi la upandaji miti iliyotolewa na Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kati-Dodoma. Zoezi hilo lilifanyika shuleni hapo tarehe 19 Machi,2025.
Afisa Maadili kutoka Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma,Kanda ya Kaskazini Arusha, Bw.Josephat Mkumbwa akiongea na Wanachama wa Klabu ya Maadili wa shule ya Msingi Kimandolu Halmashauri ya Jiji la Arusha, alipofanya ziara ya kutembelea Klabu hiyo tarehe 12 Machi,2025.
Katibu Msaidizi Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kaskazini Arusha Bw. Gerald Mwaitebele akimkabidhi Hati ya Ahadi ya Uadilifu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Bw. Gracian Makota baada ya kula kiapo hicho katika Ofisi ya Mkurugenzi wilayani Simanjiro tarehe 28 Februari, 2025.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma wakiwa katika picha ya pamoja na Kamishna wa Maadili Jaji (Stahiki) Sivangilwa Mwangesi (katikati) baada ya mkutano wa Baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hiyo Dodoma tarehe 12 Machi,2025.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bi. Teddy Njau akitoa neno la utangulizi katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo. Mkutano huo ulifanyika makao makuu ya ofisi hiyo jijini Dodoma tarehe 12 Machi,2025.
Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji (Stahiki) Sivangilwa Mwangesi akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Mkutano huo ulifanyika makao makuu ya ofisi hiyo jijini Dodoma tarehe 12 Machi,2025.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene (Mb) akikata utepe kuzindua makubaliano ya ushirikiano kati ya Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA). Kushoto kwa Waziri ni Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji (Stahiki) Sivangilwa Mwangesi na kulia kwake ni Mkuu wa Chuo cha IAA Prof. Eliamani Sedoyeka. Uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa PSSSF jijini Dodoma tarehe 6 Machi, 2025.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya maadili wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi katika mafunzo ya Maadili yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita tarehe 6 Machi 2025.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martin Shigella akifungua mafunzo ya maadili kwa Viongozi wa umma wa Mkoa wa Geita yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita tarehe 6 Machi, 2025.
Katibu Msaidizi Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kaskazini-Arusha Bw. Gerald Mwaitebele akiongoza zoezi la upandaji miti katika ziara ya kutembelea klabu za Maadili katika shule ya sekondari ya Mwakoko iliyopo wilayani Same mkoani Kilimanjaro tarehe 11 Februaru,2025.