JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS – SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

PO-ETHICS SECRETARIAT Logo
KAMATI YA BUNGE IMETOA MIEZI MITATU KUKAMILIKA KWA JENGO LA MAADILI MWANZA.
15 Mar, 2026
KAMATI YA BUNGE IMETOA MIEZI MITATU KUKAMILIKA KWA JENGO LA MAADILI  MWANZA.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imetoa miezi mitatu kwa Serikali kukamilisha ujenzi wa jengo la Maadili lililopo wilayani Ilemela mkoani Mwanza likiwa tayari kwa ajili ya kutoa huduma..

 

Mwenyekiti wa Kamati, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) amemtaka Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete kuhakikisha jengo linakamilika ifikapo mwezi Juni, 2026 na kuialika kamati ije kuzindua jengo hilo.

 

Maagizo hayo yametolewa na Mwenyekiti wa Kamati, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) wakati kamati yake ilipotembelea na kukagua mradi huo tarehe 15, Machi 2026.

 

“Hapa tumemsikiliza Kamishna wa Maadili akisema jengo linatakiwa kukamilika ifikapo Aprili, 2026 lakini sisi tukiangalia jinsi lilivyo kwa sasa haiwezekani kwa muda huo jengo likawa limekamilka”  Mhe. Ndumbaro.

 

Pia, Mwenyekiti Ndumbaro amemtaka mkandarasi wa ujenzi wa jengo hilo kufanya kazi kwa haraka kwa kuwa kwakuwa hakuna changamoto ya upatikanaji wa fedha.

 

“Kwa mkandarasi wa kiwango chako hupaswi kusubiri cheti ndio ulipwe, Serikali haijawai kumuzulumu mtu, wewe fanya kazi maliza utalipwa fedha zako, sisi tunachohitaji kazi hii ikamilike” Mhe. Ndumbaro.

 

Kamishina wa Maadili, Mhe. Jaji (Stahiki) Sivangilwa Mwangesi, amesema kukamilika kwa jengo la utawala la Maadili Kanda ya Ziwa itakwenda kuokoa fedha shilingi milioni 70 ambazo wanatumia kulipa kodi kila mwaka.

 

“Taasisi yetu ina Kanda nane na kati ya hizo ni kanda tatu tu ndio zinamiliki majengo na zilizobaki zote zimepangisha hali inayofanya Taasisi kutumia fedha shilingi milioni mia tatu kwa ajili ya pango” Mhe. Mwangesi.

 

Akiongea katika zoezi hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (Mb) amesema uwepo wa jengo Kanda ya Ziwa utasaidia watumishi kufanya vyema kazi ya kusimamia maadili ya Viongozi wa Umma kwa uhuru na ufanisi mkubwa.

 

Online Help
Kuanzisha Enzi Mpya katika Udhibiti wa Sekta ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania
Ofisi ya maadili inafanya kazi na imewashughulikia viongozi wengi sana kupitia Baraza la Maadili ambalo pia liliendeshwa mwaka 2013 Novemba mkoani Tabora. Viongozi mbalimbali waliokuwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili waliitwa kwenye Baraza na kuhojiwa na Baraza linatoa mapendekezo na kuyawasilisha mapendekezo hayo kwa Rais kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu na kisheria kwa viongozi husika.

" >
Kifungu cha 11(1) cha Sheria ya Maadili kimeainisha wazi mali zinazotakiwa kutajwa kuwa ni fedha taslimu, fedha zilizopo katika taasisi za kifedha kama vile benki, hisa, nyumba, mashamba, magari, mitambo na mali nyinginezo. Kiongozi anatakiwa kutoa tamko la mali anazomiliki yeye mwenyewe, mke/mume na watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane. Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni zinatakiwa kujazwa kila mwaka na kiongozi hutumiwa fomu hizo na Ofisi ya Maadili na pia zinapatikana katika mtandao wa maadili yaani www.ethicssecretariat.go.tz. Sheria inamtaka kiongozi kutolea tamko madeni yake ili kuweza kujua kuwa kiongozi anamiliki mali zipi na pia kutambua kuwa amezipata vipi mali hizo ukilinganisha na kipato cha kiongozi husika. Kiongozi kuwa na mali nyingi si dhambi kwani hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetamka wazi kuwa kila raia ana haki ya kumiliki mali ila ofisi inataka kujiridhisha uhalali wa jinsi mali ilivyopatikana. Mapendekezo katika Katiba mpya yanasisitiza maadili kwa kutenganisha uongozi na biashara.

" >
Wananchi wengi wamejijengea dhana kuwa bila pesa huwezi kupata huduma ya kiserikali kitu ambacho si kweli kwani huduma nyingi za kiserikali zinatolewa bure kabisa ila cha msingi wananchi wanatakiwa kutoa taarifa katika vyombo husika pindi wanapotakiwa kulipia huduma ambazo zinatolewa bure. Jamii inatakiwa kubadilika na kuamini kuwa si lazima kutoa rushwa ndipo upate huduma. Wapo wananchi wengi ambao walileta malalamiko kama hayo na Ofisi ya Maadili iliyashughulikia, hivyo wananchi wasisite kutembelea Ofisi zetu kwa ajili ya kutoa taarifa kama hizo.

" >
Kutoa lugha chafu ni ukiukwaji wa maadili. Ndani ya Bunge kuna Kamati ya Maadili ambayo ipo kwa ajili ya kuwawajibisha wabunge wanaotoa lugha chafu. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa upande wake ilifanya semina kwa wabunge ili kuwakumbusha mipaka ya utendaji kazi na maadili kwa ujumla, na tangu wakati huo matumizi ya lugha chafu bungeni yamepungua kwa kiasi kikubwa.

" >