DC Mwaipaya: Tusisubili hadi tuitwe na Maadili
Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Mhe. Abdallah Mwaipaya ametoa wito kwa viongozi wa umma nchini kuondokana na tabia ya kusubiri hadi waitwe na Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ndio waanze kujaza Tamko la Rasilimali na Madeni.
Wito huo ameutoa wakati akifungua mafunzo ya ujazaji wa Tamko la Rasilimali na Madeni kwa njia ya mtandao (Online Declaration System - ODS) yaliyotolewa kwa viongozi wa umma mkoani Mtwara tarehe 6 Machi, 2026 katika ukumbi wa Maadili Mtwara.
Mhe. Mwaipaya amesema kuwa Viongozi wa Umma wanatakiwa kuwasiliana na Sekretarieti ya Maadili mapema pale ambapo watapata changamoto hili iweze kutatuliwa mapema na kuepuka kuitwa na kwa kosa la kushindwa kujaza Tamko la Rasilimali na Madeni.
Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa wilaya, kama hujaitwa usije kudhani unajaza ni gelesha tu kwa kuwa kila mwaka una jaza na hujawai kuitwa na kuona kama wanakusumbua tu ila tambua Sekretarieti ya Maadili wakati wowote wanaweza kukuita na kutaka utoe maelezo kuhusu Tamko lako, hivyo ni wajibu wetu sote kama viongozi kuepuka adhaa ya kujaza rasilimali kwa mazoea.
“Kuna siku utaitwa kwa kosa tu la kushindwa kujaza Tamko la Rasilimali na Madeni kwa uzembe wako au kwa kuwa ulichukulia poa kwa kuwa kila mwaka unajaza ila siku utapoacha kujaza ndio siku utaitwa na kutakiwa kueleza,” alisema Mhe. Mwaipaya.
Kaimu Katibu Msaidizi Kanda ya Kusini - Mtwara Bw. Ramadhan Ramadhan aliwaambia viongozi kuwa dirisha la kujaza Tamko la Rasilimali na Madeni la mwaka linafunguliwaga mapema kuanzia tarehe 1 Oktoba hadi 31 Disemba kila mwaka, hivyo ni wajibu kwa viongozi kuanza kujaza mapema pale dirisha linapokuwa wazi.
Afisa Maadili kutoka Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw. Ramadhan Ng’wanang’waka alitoa mafunzo kwa viongozi hao namna ya kujaza Tamko kwa njia ya mtandao.
