Mamlaka na Majukumu
Mamlaka na Majukumu
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ina mamlaka na majukumu yafuatayo:-
- Kupokea taarifa za mali na madeni zinazohitajika kutolewa na Viongozi wa Umma kwa mujibu wa Sheria;
- Kupokea malalamiko na tuhuma kuhusu ukiukwaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma kutoka kwa wanachi;
- Kufanya uchunguzi wa awali wa tuhuma au malalamiko dhidi ya kiongozi yoyote wa umma anayetuhumiwa kuvunja masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi;
- Kuanzisha na kufanya uchunguzi wowote kuhusu ukiukwaji wa Maadili yaliyotajwa katika Sheria bila kusubiri malalamiko kutoka kwa Wananchi;
- Kuhakiki taarifa za Rasilimali na Madeni zinazotolewa na Viongozi wa Umma kwa mujibu wa Sheria;
- Kuwaelimisha Viongozi wa Umma na Wananchi kuhusu Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma pamoja na kazi za Sekretarieti;
- Kutunza daftari la Rasilimali , Maslahi na Madeni ya Viongozi wa Umma;
- Kuratibu na kuwezesha shughulli za Baraza la Maadili;
- Kuwasilisha kwa Rais mapendekezo ya Baraza la Maadili kuhusu uchunguzi wa kina wa tuhuma za ukiukwaji wa maadili dhidi ya Viongozi wa Umma;
- Kufanya utafiti juu ya uzingatiaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
- Kumtaka mtu yoyote kufika mbele ya Sekretarieti ya Maadili kwa ajili ya mahojiano ambayo yatasaidia katika uchunguzi wa ukiukwaji wa maadili;
- Kukagua akaunti ya Benki ya Kiongozi yoyote wa Umma kwa idhini ya Mahakama pale ambapo Sekretarieti inatarajia kufanya uchunguzi dhidi ya kiongozi husika;
- Kumtaka Kiongozi anayetuhumiwa kwa kutoa tamko la uongo la rasilimali zake kuthibitisha au kurekebisha Tamko lake;
- Kutoa idhini ya kukagua Daftari la Raslimali, Maslahi na Madeni ya Kiongozi wa Umma kwa Mwananchi aliyekidhi vigezo;
- Kumtaka mtu yoyote kuwasilisha kitabu, nyaraka au nakala iliyothibitishwa au kielelezo chochote ambacho kitasaidia uchunguzi kuhusu ukiukwaji wa Maadili.