JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS – SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

PO-ETHICS SECRETARIAT Logo
Klabu za Maadili zatajwa kichocheo cha taaluma na nidhamu Hanang
20 May, 2026
Klabu za Maadili zatajwa kichocheo cha taaluma na nidhamu Hanang

Kuanzishwa kwa Klabu za Maadili katika shule za msingi na sekondari wilayani Hanang mkoani Manyara kumetajwa kuwa moja ya sababu za mabadiliko kinidhamu na ukuaji wa taaluma miongozi mwa wanafunzi wilayani humo.

Hayo yamesemwa kwa nyakati tofauti na viongozi, walimu na wanafunzi wa shule zenye Klabu za Maadili wilayani humo wakati wa zoezi la kutembelea wanachama wa klabu hizo lililofanyika kuanzia tarehe 18 hadi 20 Mei, 2026 na kuratibiwa na Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kaskazini-Arusha.

Akizungumzia uwepo wa klabu hizo  Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Hanang Bi. Sophia Msoffe amesema klabu za maadilli zimekua chanzo katika kujenga maadili na hali ya kujiamini kwa wanafunzi hasa katika kujieleza au kuchangia jambo lolote la kitaaluma.

“Klabu hizi zimekua zikifanyika katika mazingira huru ambapo watoto wanakua na nafasi ya kuonyesha walichonacho na pia kupokea kwa undani kile wanachopata kutoka kwa walimu walezi wa klabu na wakufunzi kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma,” alisema Bi. Sophia.

Kwa upande wake mkuu wa shule ya sekondari Measkron Bw. Seluwin Mkisi amesema licha ya klabu hizo kuwa nyenzo muhimu katika kukuza taaluma na uadilifu pia imesaidia kuwajenga kiroho wanafunzi na kupelekea kuwa na tabia njema.

“Licha ya kusaidia upande wa taaluma, lakini uwepo wa klabu hii umesaidia kuwajenga watoto wetu kiroho, kwa sababu tunapoongelea maadili ni pamoja na muonekano ambao upelekea tabia njema na hatimaye kupata watoto waadilifu kimwili na kiroho pia,” alisema mwalimu Mkisi.

Nae mwalimu mlezi wa Klabu ya Maadili shule ya msingi Jorodom Bi. Rose Manda amesema kuwa uwepo wa klabu ya maadili shuleni hapo umechangia katika kupunguza utoro na kurekebisha nidhamu kwa wanafunzi hasa kupitia kazi mbali mbali wanazofanya katika klabu yao.

“Klabu ya maadili imechangia kurekebisha nidhamu na kupunguza utoro kwa kiasi kikubwa hapa shuleni, huku wanafunzi ambao sio wanachama wakijitaidi kuwa na nidhamu nzuri na kuhudhuria shule bila kukosa kwa kuamini kuwa ipo siku watapata nafasi ya kuwa wanachama wa klabu ya maadili,” alisema mwalimu huyo.

Kwa upande wake mwanafunzi wa sekondari ya Wasichana Nangwa, Sharifa Saidi amesema uwepo wa  Klabu ya Maadili umesaidia wao kuwa na maadili mazuri ndani na nje ya shule kwa kuwa watiifu na kuheshimu wazazi na watu wengine kwa kuyafanya yale wanayofundishwa kwenye klabu yao.

Mradi wa Klabu za Maadili kwa shule za msingi, sekondari na vyuo umekua ukiratibiwa na Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambapo kupitia mradi huo wanachama wa klabu hizo wamekua wakifanya shughuli mbali mbali kama vile kupanda miti, kutengeneza bustani za maua na mboga mboga pamoja na sanaa za maigizo kwa lengo la kukuza taaluma na kuwajenga kimaadili na uzalendo angali wakiwa wanafunzi.

 

 

Online Help
Kuanzisha Enzi Mpya katika Udhibiti wa Sekta ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania
Ofisi ya maadili inafanya kazi na imewashughulikia viongozi wengi sana kupitia Baraza la Maadili ambalo pia liliendeshwa mwaka 2013 Novemba mkoani Tabora. Viongozi mbalimbali waliokuwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili waliitwa kwenye Baraza na kuhojiwa na Baraza linatoa mapendekezo na kuyawasilisha mapendekezo hayo kwa Rais kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu na kisheria kwa viongozi husika.

" >
Kifungu cha 11(1) cha Sheria ya Maadili kimeainisha wazi mali zinazotakiwa kutajwa kuwa ni fedha taslimu, fedha zilizopo katika taasisi za kifedha kama vile benki, hisa, nyumba, mashamba, magari, mitambo na mali nyinginezo. Kiongozi anatakiwa kutoa tamko la mali anazomiliki yeye mwenyewe, mke/mume na watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane. Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni zinatakiwa kujazwa kila mwaka na kiongozi hutumiwa fomu hizo na Ofisi ya Maadili na pia zinapatikana katika mtandao wa maadili yaani www.ethicssecretariat.go.tz. Sheria inamtaka kiongozi kutolea tamko madeni yake ili kuweza kujua kuwa kiongozi anamiliki mali zipi na pia kutambua kuwa amezipata vipi mali hizo ukilinganisha na kipato cha kiongozi husika. Kiongozi kuwa na mali nyingi si dhambi kwani hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetamka wazi kuwa kila raia ana haki ya kumiliki mali ila ofisi inataka kujiridhisha uhalali wa jinsi mali ilivyopatikana. Mapendekezo katika Katiba mpya yanasisitiza maadili kwa kutenganisha uongozi na biashara.

" >
Wananchi wengi wamejijengea dhana kuwa bila pesa huwezi kupata huduma ya kiserikali kitu ambacho si kweli kwani huduma nyingi za kiserikali zinatolewa bure kabisa ila cha msingi wananchi wanatakiwa kutoa taarifa katika vyombo husika pindi wanapotakiwa kulipia huduma ambazo zinatolewa bure. Jamii inatakiwa kubadilika na kuamini kuwa si lazima kutoa rushwa ndipo upate huduma. Wapo wananchi wengi ambao walileta malalamiko kama hayo na Ofisi ya Maadili iliyashughulikia, hivyo wananchi wasisite kutembelea Ofisi zetu kwa ajili ya kutoa taarifa kama hizo.

" >
Kutoa lugha chafu ni ukiukwaji wa maadili. Ndani ya Bunge kuna Kamati ya Maadili ambayo ipo kwa ajili ya kuwawajibisha wabunge wanaotoa lugha chafu. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa upande wake ilifanya semina kwa wabunge ili kuwakumbusha mipaka ya utendaji kazi na maadili kwa ujumla, na tangu wakati huo matumizi ya lugha chafu bungeni yamepungua kwa kiasi kikubwa.

" >