Wawakilishi wa vyombo vya habari nchini Kanda ya Kusini Mtwara wapigwa msasa kuhusu Maadili
Vyombo vya habari nchini vimetakiwa kuhakikisha vinatoa mchango mkubwa katika kuimarisha na kukuza maadili ya viongozi wa Umma nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Msaidizi Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kanda ya kusini Mtwara Bw. Manula alipokuwa akifungua kikao kazi na wawakilishi wa vyombo vya habari kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi Kanda ya kusini Mtwara tarehe 10 mwezi April 2026.
Aidha Bw Manula katika hotuba yake amesisitiza ushiriano mzuri kati ya Sekretarieti na vyombo vya habari nchini kuhakikisha Maadili ya viongozi yanaimarika kupitia vyombo vya habari nchini.
Ameongeza kuwa ushirikiano kati ya Sekretarieti ya Maadili na vyombo vya habari utasaidia kupanua uwigo na kujenga imani ya wanachi na Sekretarieti pamoja wananchi kwa ujumla.
Bw. Manula ametoa wito kwa wawakilishi wa vyombo hivyo vya habari wanakuwa mabalozi wazuri katika kuhakikisha kuwa Maadili yanakuzwa na kuimarika kwa kutoa Elimu ya Maadili kupitia vyombo mbalimbali vya habari nchini
Akitoa neno la ufunguzi Mkurugenzi wa mipango na ufatiliaji Bw. Omary Juma amewataka wawakilishi wa vyombo vya habari nchini kuhakikisha ushirikiano uliopo kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na vyombo vya habari katika kanda ya kusini Mtwara unaimarika katika kusimamia na kukuza maadili kwa kuelimisha umma na wananchi kupitia vyombo vya habari.
Akitoa mada kuhusu majukumu ya Sekretarieti ya Maadili Afisa Maadili kanda ya kusini Mtwara Bw. Yusuph Sumbu ametaja baadhi ya majukumu ya Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma kuwa ni pamoja na kupokea Matamko ya Raslimali na madeni ya viongozi wa Umma, kutoa Elimu ya Maadili kwa viongozi na wananchi pamoja na kupokea malalamiko dhidi ya viongozi wanaokiuka maadili kutoka kwa wanachi na kuanzisha kufanya uchunguzi wa kina kuhusianana malalamiko hayo.
Kikao kazi hicho cha siku moja kilikuwa na lengo la kuhakikisha ushirikiano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na vyombo vya habari unaimarika katika kuhakikisha kuwa uwajibikaji wa viongozi unaongezeka kupitia vyombo vya habari nchini.
