Watumishi wa TRA- Arusha waaswa kuzingatia Ahadi ya Uadilifu


Watumishi wa TRA- Arusha waaswa kuzingatia Ahadi  ya Uadilifu
11
Sep
2023

Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Arusha wametakiwa kuzingatia masharti ya Ahadi ya Uadilifu katika utendaji kazi wao wa kila siku.

Hayo yalisemwa na Afisa wa Maadili kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kaskazini-Arusha Bw. Tumaini Mgalla i wakati akitoa mada kuhusu Ahadi ya Uadilifu kwa watumishi haohivi karibuni .

Bw. Mgalla alieleza kuwa Hati ya Ahadi ya Uadilifu ni tamko rasmi la kimaandishi linalotolewa na Viongozi wa Umma pindi wanapoteuliwa au kuchaguliwa kuonyesha dhamira ya kuzingatia misingi ya maadili na mapambano dhidi ya rushwa.

Katika mada yake Bw.Mgalla alizitaja athari za kukiuka masharti ya Ahadi ya Uadilifu kuwa ni pamoja na kiongozi wa umma kuchukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria, wananchi kutokuwa na imani na serikali yao.

“Kiongozi wa Umma asipoyaishi yale aliyoahidi katika kiapo chake ni dhahiri kuwa wananchi watakosa imani na kiongozi huyo pamoja na Serikali kwa ujumla,” alisema.

Aidha Bw. Mgalla alifayataja baadhi ya masharti yaliyopo katika Hati ya Ahadi ya Uadilifukuwa ni pamoja na;Uwazi katika utekelezaji wa shughuli za umma na kufanya maamuzi; Uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu ya umma;Uadilifu katika utendaji wa kazi za umma naKuzingatia weledi katika utendaji kazi za umma.

Masharti mengine ni; Uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu; Uzalendo kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;Uaminifu katika shughuli za umma ili kulinda fedha na mali nyinginezo za umma;Kuepuka mgongano wa maslahi, Matumizi sahihi ya taarifa na Kutoa huduma bora bila upendeleo.

“Baada ya kiongozi wa umma kusaini hati hiyo, anawajibika kutekeleza masharti yote yaliyoko katika Hati ya Ahadi ya Uadilifu ili kuleta uwazi katika utendaji wake wa kazi na wananchi kuwa na imani na Serikali yao,” alisema.