WATUMISHI WA SEKRETARIETI YA MAADILI WATAKIWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA WELEDI NA UADILIFU.

Watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa weledi na uadilifu wa kiwango cha juu kwa maslahi mapanaya taifa letu.
Kauli hiyo imetolewana Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Sivangilwa Mwangesi katika kikao cha baraza la wafanyakazi wa Sekretarieti ya Maadili kilichofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) tarehe 24 Agosti,2023.
Katika hotuba yake ya ufunguzi, Mhe. Mwangesi alisema kuwa katika kutekeleza majukumu ya Taasisi watumishi wanatakiwa kuacha uzembe, uvivu na kuepuka kufanya kazi kwa mazoea ili kujenga imani kwa wananachi na Serikali iliyopo madarakani na kwamba wasiwe chanzo au sababu ya kukwamisha utekelezaji wa majukumu.
“Kila mtumishi kwa nafasi yake anatakiwa kuacha uzembe na kufanya kazi kwa weledi na kutambua kuwa ana wajibu wa kukuza maadili” amesema na kuongeza kuwa watumishi wa Sekretarieti ya Maadili wafanye kazi kwa bidii na kutunza siri za Serikali.
Aidha, Mhe. Mwangesiameeleza kuwa changamotozinazoikabilitaasisi zimepungua kwa kiasi kikubwa ikiwemo uhaba wa majengo ya ofisi zinazomilikiwa na taasisi, ambapo kwa sasa Ofisi inategemea kukamilisha baadhi ya majengo yake katika mwaka huu wa fedha.
Awali akitoa neno la ukaribisho katika kikao hicho Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Bi.Teddy Njau alieleza kuwa kikao hicho ni kwa mujibu wa Waraka wa Rais , Na. 1 wa mwaka 1971 unaoelekeza kila Taasisi kuwa na Baraza la Wafanyakazi