WATUMISHI WA KANDA YA KUSINI MTWARA WAMETAKIWA KUWA WAADILIFU:

Watumishi wa Kanda ya Kusini Mtwara, wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa Uadilifu, Umakini, na weledi wa kiwango cha juu.
Kauli hiyo, imetolewana Kamishna wa Maadili Mhe, Jaji Sivangilwa Mwangesi, katika ziara yake ya kutembelea Kanda ya kusini Mtwara tarehe 21 juni, 2023.
Aidha, Mhe Mwangesi katika hotuba yake ameongeza kuwa, ziara hiyo ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza rasmi tarehe16 juni, na kuhitimishwa tareha 23 juni, 2023.
Mhe, Kamishna alifafanua kuwa,lengo kubwa la ziara yake katika maadhimisho haya ni pamoja na kuwakumbusha watumishi na viongozi wa Umma kwa ujumla kuhusu wajibu wao, na maadili katika kutekeleza majukumu yao ya kilasiku.
Kuhusu changamoto zilizopo katika kanda hiyo, Mhe, Mwangesi alifafanua kuwa, kuhusu uhaba wa watumishi na upungufu wa magari , suala hio linafanyiwa kazii na mchakato unaendelea.
Mhe, Mwangesia mewataka watumishi wa Kanda hiyo kutunza jengo la Ofisi ambalo ni zuri na kubwa ili lweze kudumu kwa muda mrefu ikiwani sehemu ya uboreshaji wa mazingira ya kufanyia kazi.
Aliongeza kuwa, Sekretarieti iko katika mchakato wakuanzisha mfumo wa Online Decrelation Systerm(ODS )ambao utasaidia kurahisisha utekelezaji wa Majukumu ya Taasisi na pia kuwawezesha Viongozi kutuma matamko yao kwa njia ya Mtandao kwa uhakika na urahisi zaidi tofauti na ilivyo sasa.
Ziara hii ya Mhe, Kamishna wa Maadili ,katika Kanda ya kusini Mtwara ni iMaadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kitaifa iliyoanza rasmi tarehe 16 juni, na kuhitimishwa tarehe 23 Juni, 2023.