JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS – SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

PO-ETHICS SECRETARIAT Logo
WANACHUO WAMETAKIWA KUJIFUNZA UTUNZAJI WA MAZINGIRA NA BIASHARA YA HEWA UKAA
27 Feb, 2026
WANACHUO WAMETAKIWA KUJIFUNZA UTUNZAJI WA MAZINGIRA NA BIASHARA YA HEWA UKAA

Wanachuo wa klabu za maadili nchini ambao pia ni wanachama wa Klabu za Maadili wametakiwa kujifunza biashara ya hewa ya ukaa na kutafsiri kibiashara kwani inaweza kuwa mkombozi mkubwa wa uchumi kwa mtu binafsi pamoja na Taifa kwa ujumla.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Mhe. Jabir Shekimweri wakati wa uzinduzi wa bustani ya maadili iliyopo karibu na Chuo cha Biashara CBE kilichopo jijini Dodoma tarehe 27 Februari 2026.

Aidha Mhe. Shekimweri amesema katika dunia ya hewa ukaa ukifanikiwa kusajili ekari zako kuanzia moja na ukapanda miti ya aina yoyote ile, dunia ina teknolojia ya kujua pale unazalisha hewa kwa kiasi gani na wanakulipa fedha nzuri ambayo inaweza kukutoa kwenye umasikini na ukawa bilionea.

Tujifunze biashara ya hewa ukaa kuna wengine hapa tumetoka vijijini tunaweza kupata ata ekari moja au zaidi tukazisajili na kupanda miti baada ya miaka mitatu au zaidi inawezekana baada ya kumaliza chuo ikawa msaada mkubwa kiuchumi,” Mhe, Shekimweri.

Katika hatua nyingine Kamisha wa Maadili, Mhe. Jaji (Stahiki) Sivangilwa Mwangesi amesema leo hatupandi mti tu bali tunapanda maadili, uwajibikaji na uongozi bora kwani uongozi bora haupimwi kwa maneno mazuri tu bali kwa vitendo vinavyoleta manufaa katika jamii.

“Sekretarieti ya Maadili inaunga mkono juhudi za Serikali ya kuifanya Dodoma kuwa ya kijani kwa kuzipa ushirikiano klabu za maadili kwa kutunza mazingira, amesema.

Mhe. Mwangesi alibainisha kuwa wanachama wa Klabu za Maadili wanatakiwa kuwa mabalozi wa kesho, kwani mti ambao mtapanda leo ni ahadi ambayo mnaitoa kwa taifa lenu kwamba mtakuwa viongozi ambao mnaojali, kuwajibika na kulinda rasilimali za umma.

“Tusipande miti kwa ajili ya picha ya leo bali tupande miti kwa ajili ya kivuli cha kesho,” Mhe. Mwangesi alisisitiza.

Naye Mstahiki Meya wa jiji la Dodoma, Mhe. Alimwoni Chaula amesema Jiji la Dodoma ndio mmiliki wa eneo la bustani ya maadili lakini wameamua kulitoa kwa Sekretarieti ya Maadili kwa ajili ya kutunza mazingira na kuifanya Dodoma iwe ya kijani, eneo hili liko mjini na thamani yake kwa sasa ni zaidi ya shilingi za Kitanzania Bilioni 10 lakini jiji tumetoa kipaombele cha kutunza mazingira.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu ya Maadili wa Chuo cha CBE, Ndg. Kimu Kambona ameishukuru Sekretarieti ya Maadili kwa alama ambayo wameweka kwenye Chuo chao kwa kuanzisha bustani ya maadili iliyopo jirani na chuo chao.

Aidha Mwenyekiti wa klabu ya maadili wa Chuo cha Mipango Ndg. Libwanga Kizota amefafanua kuwa wanachama wake wa Mipango watachukua jukumu la kuhakikisha sehemu hiyo inakuwa safi na ya kuvutia.

Hafla hiyo imeudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Dodoma pamoja na wanachama wa Kbalu za Maadili kutoka Chuo cha CBE, Chuo cha Mipango na Chuo Kikuu cha Mtakatifu John.

 

 

Online Help
Kuanzisha Enzi Mpya katika Udhibiti wa Sekta ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania
Ofisi ya maadili inafanya kazi na imewashughulikia viongozi wengi sana kupitia Baraza la Maadili ambalo pia liliendeshwa mwaka 2013 Novemba mkoani Tabora. Viongozi mbalimbali waliokuwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili waliitwa kwenye Baraza na kuhojiwa na Baraza linatoa mapendekezo na kuyawasilisha mapendekezo hayo kwa Rais kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu na kisheria kwa viongozi husika.

" >
Kifungu cha 11(1) cha Sheria ya Maadili kimeainisha wazi mali zinazotakiwa kutajwa kuwa ni fedha taslimu, fedha zilizopo katika taasisi za kifedha kama vile benki, hisa, nyumba, mashamba, magari, mitambo na mali nyinginezo. Kiongozi anatakiwa kutoa tamko la mali anazomiliki yeye mwenyewe, mke/mume na watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane. Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni zinatakiwa kujazwa kila mwaka na kiongozi hutumiwa fomu hizo na Ofisi ya Maadili na pia zinapatikana katika mtandao wa maadili yaani www.ethicssecretariat.go.tz. Sheria inamtaka kiongozi kutolea tamko madeni yake ili kuweza kujua kuwa kiongozi anamiliki mali zipi na pia kutambua kuwa amezipata vipi mali hizo ukilinganisha na kipato cha kiongozi husika. Kiongozi kuwa na mali nyingi si dhambi kwani hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetamka wazi kuwa kila raia ana haki ya kumiliki mali ila ofisi inataka kujiridhisha uhalali wa jinsi mali ilivyopatikana. Mapendekezo katika Katiba mpya yanasisitiza maadili kwa kutenganisha uongozi na biashara.

" >
Wananchi wengi wamejijengea dhana kuwa bila pesa huwezi kupata huduma ya kiserikali kitu ambacho si kweli kwani huduma nyingi za kiserikali zinatolewa bure kabisa ila cha msingi wananchi wanatakiwa kutoa taarifa katika vyombo husika pindi wanapotakiwa kulipia huduma ambazo zinatolewa bure. Jamii inatakiwa kubadilika na kuamini kuwa si lazima kutoa rushwa ndipo upate huduma. Wapo wananchi wengi ambao walileta malalamiko kama hayo na Ofisi ya Maadili iliyashughulikia, hivyo wananchi wasisite kutembelea Ofisi zetu kwa ajili ya kutoa taarifa kama hizo.

" >
Kutoa lugha chafu ni ukiukwaji wa maadili. Ndani ya Bunge kuna Kamati ya Maadili ambayo ipo kwa ajili ya kuwawajibisha wabunge wanaotoa lugha chafu. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa upande wake ilifanya semina kwa wabunge ili kuwakumbusha mipaka ya utendaji kazi na maadili kwa ujumla, na tangu wakati huo matumizi ya lugha chafu bungeni yamepungua kwa kiasi kikubwa.

" >