JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS – SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

PO-ETHICS SECRETARIAT Logo
WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI NCHINI WATAKIWA KUWA MABALOZI WAZURI KATIKA KUKUZA MAADILI NCHINI.
30 Mar, 2026
WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI NCHINI WATAKIWA KUWA MABALOZI WAZURI KATIKA KUKUZA MAADILI NCHINI.

Wamiliki wa vyombo vya habari nchini wametakiwa kuwa mabalozi wazuri katika jitihada za  kukuza na kuimarisha   Maadili ya Viongozi wa Umma nchini kupitia vyombo mbali mbali vya Habari kama vile Redio, magazeti, Luninga pamoja na mitandao ya kijamii.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu msaidizi sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma Kanda ya Magharibi Tabora Bibi Anna Mbasha alipokuwa akifungua kikao kazi kuhusu mchango wa vyombo vya habari katika kukuza Maadili nchini, kilichofanyika katika Hoteli ya JM mkoani Tabora tarehe 30 Machi 2026.

Bibi Mbasha amebainisha kuwa vyombo vya habari vina mchango Mkubwa katika jitihada za kukuza na kudumisha Maadili ya Viongozi wa Umma nchini katika kuhakikisha kuwa Maadili ya viongozi waUmma yanaimarika kwa kuelimisha na kuhabarisha umma kuhusu umuhimu wa Maadili kupitia vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Aidha Bibi Mbasha katika hotuba yake amebainisha kuwa lengo la kikao hicho pamoja na mambo mengine ni kuongeza hamasa ya wanahabari kushiriki kikamilifu katika kukuza maadili ya viongozi wa Umma nchini pamoja na kutambua nafasi ya vyombo vya habari katika kuelimisha umma na kudumisha ushirikiano baina ya vyombo vya habari na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

”Jukumu la ukuzaji wa Maadili ya viongoziwa umma ni letu sote na linalenga kuongeza uelewa wa viongozi wa umma na wananchi kwa ujumla wake

Hivyo vyombo vya habari vina jukumu la kutoa taarifa kuhusu ukiukwaji wa wa Maadili ya viongozi pale yanapojitokeza katika maeneo mbali mbali nchini amesema”

Awali akitoa neno la utangulizi kuhusu lengo la kikao hicho Mkurugenzi wa Mipango na Tathimini kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma makao makuu Bw. Omary  Juma ameeleza baadhi ya  majukumu ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambayo ni pamoja na kupokea matamko ya viongozi wa umma kuhusu Raslimali na Madeni yanayotolewa na viongozi wa umma kwa mujibu wa sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Ametaja jukumu lingine la msingi kuwa ni kufanya uchunguzi wa kina wa malalamiko  na taarifa  za ukiukwaji wa maadili  kwa mujibu wa sheria ya maadili ya viongozi wa umma kutoka kwa wananchi.

Bwana Juma pia amewataka wamiliki wa vyombo vya habari nchini kutumia kikao kicho muhimu kujenga mahusiano mema na Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma na pia kutoa ushirikiano mwema katika kuhabarisha Umma katika kuhakikisha masuala ya maadili yanapewa kipaumbele kupitia vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Kikao hiki kimewashirikisha wamiliki wa vyombo vya habari nchini kutoka katika kanda ya Magharibi kutoka katika mikoa ya Shinyanga,Kigoma,Simiyu na Tabora.

Online Help
Kuanzisha Enzi Mpya katika Udhibiti wa Sekta ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania
Ofisi ya maadili inafanya kazi na imewashughulikia viongozi wengi sana kupitia Baraza la Maadili ambalo pia liliendeshwa mwaka 2013 Novemba mkoani Tabora. Viongozi mbalimbali waliokuwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili waliitwa kwenye Baraza na kuhojiwa na Baraza linatoa mapendekezo na kuyawasilisha mapendekezo hayo kwa Rais kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu na kisheria kwa viongozi husika.

" >
Kifungu cha 11(1) cha Sheria ya Maadili kimeainisha wazi mali zinazotakiwa kutajwa kuwa ni fedha taslimu, fedha zilizopo katika taasisi za kifedha kama vile benki, hisa, nyumba, mashamba, magari, mitambo na mali nyinginezo. Kiongozi anatakiwa kutoa tamko la mali anazomiliki yeye mwenyewe, mke/mume na watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane. Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni zinatakiwa kujazwa kila mwaka na kiongozi hutumiwa fomu hizo na Ofisi ya Maadili na pia zinapatikana katika mtandao wa maadili yaani www.ethicssecretariat.go.tz. Sheria inamtaka kiongozi kutolea tamko madeni yake ili kuweza kujua kuwa kiongozi anamiliki mali zipi na pia kutambua kuwa amezipata vipi mali hizo ukilinganisha na kipato cha kiongozi husika. Kiongozi kuwa na mali nyingi si dhambi kwani hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetamka wazi kuwa kila raia ana haki ya kumiliki mali ila ofisi inataka kujiridhisha uhalali wa jinsi mali ilivyopatikana. Mapendekezo katika Katiba mpya yanasisitiza maadili kwa kutenganisha uongozi na biashara.

" >
Wananchi wengi wamejijengea dhana kuwa bila pesa huwezi kupata huduma ya kiserikali kitu ambacho si kweli kwani huduma nyingi za kiserikali zinatolewa bure kabisa ila cha msingi wananchi wanatakiwa kutoa taarifa katika vyombo husika pindi wanapotakiwa kulipia huduma ambazo zinatolewa bure. Jamii inatakiwa kubadilika na kuamini kuwa si lazima kutoa rushwa ndipo upate huduma. Wapo wananchi wengi ambao walileta malalamiko kama hayo na Ofisi ya Maadili iliyashughulikia, hivyo wananchi wasisite kutembelea Ofisi zetu kwa ajili ya kutoa taarifa kama hizo.

" >
Kutoa lugha chafu ni ukiukwaji wa maadili. Ndani ya Bunge kuna Kamati ya Maadili ambayo ipo kwa ajili ya kuwawajibisha wabunge wanaotoa lugha chafu. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa upande wake ilifanya semina kwa wabunge ili kuwakumbusha mipaka ya utendaji kazi na maadili kwa ujumla, na tangu wakati huo matumizi ya lugha chafu bungeni yamepungua kwa kiasi kikubwa.

" >