JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS – SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

PO-ETHICS SECRETARIAT Logo
Walezi wa Klabu za Maadili wapatiwa mafunzo ya Maadili
01 Mar, 2026
Walezi wa Klabu za Maadili wapatiwa mafunzo ya Maadili

Walezi wa klabu za Maadili ambao ni walimu kutoka shule za msingi , sekondari  na vyuo katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi wamepatiwa mafunzo kuhusu maadili na namna ya kuanzisha na kuendeleza klabu za maadili.  

Mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kaskazini-Arusha yalifanyika tarehe 27 Februari, 2026 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

Akifungua mafunzo hayo Afisa Elimu Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Abel Ntupwa alisema kuwa mafunzo hayo kwa walimu walezi wa klabu za maadili ni muhimu kwa sababu mwalimu ndio mlezi mkuu wa wanafunzi anapokua shuleni.

“Kuwepo kwa klabu za maadili katika Taasisi za elimu ni jambo zuri kwani huongeza uadilifu, kupunguza changamoto ya utoro, huongeza kasi ya ufaulu na huchochea mwenendo mwema kwani wahenga walisema mtoto umleavyo ndivyo akuavyo,” alisema.

Aidha Bw. Ntupwa alieleza kuwa upo umuhimu mkubwa wa walimu walezi wa klabu hizo kupatiwa  mafunzo ya mara kwa mara kwani itasaidia katika kujenga kizazi chenye misingi imara ya maadili na kupata Taifa lenye Viongozi bora.

“Semina hii ni muhimu na tunaomba ndugu zetu wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kutukumbuka tena hapo baadae maana ni imani yangu mafunzo haya yatakua chachu ya kuwaongezea ujuzi kwa namna ya kuzifungua na kuziendeleza klabu hizi mkoani kwetu,” alisema.

Awali akitoa neno la utangulizi Katibu Msaidizi Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kaskazini –Arusha Bw. Gerald Mwaitebele alieleza kuwa jukumu kubwa wao kama Taasisi ni kusimamia na kukuza Maadili ya Viongozi wa Umma nchini hivyo wanaanza kuwaandaa mapema Viongozi wenye maadili.

“Kama chombo chenye wajibu wa kusimamia na kukuza maadili nchini tumeamua kwa dhati kabisa kuanzisha klabu za maadili katika shule za Msingi, Sekondari na Vyuo vya Elimu kwa lengo la kusimamia maadili katika ngazi ya chini kama usemi usemao samaki mkunje angali mbichi, “alisema.

Katika mafunzo hayo mada mbalimbali ziliwasilishwa ikiwa ni pamoja na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, majukumu ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma , misingi ya maadili   katika utumishi wa umma pamoja na mada kuhusu mwongozo wa ufunguaji na uendeshaji wa Klabu za maadili.

 

 

 

Online Help
Kuanzisha Enzi Mpya katika Udhibiti wa Sekta ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania
Ofisi ya maadili inafanya kazi na imewashughulikia viongozi wengi sana kupitia Baraza la Maadili ambalo pia liliendeshwa mwaka 2013 Novemba mkoani Tabora. Viongozi mbalimbali waliokuwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili waliitwa kwenye Baraza na kuhojiwa na Baraza linatoa mapendekezo na kuyawasilisha mapendekezo hayo kwa Rais kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu na kisheria kwa viongozi husika.

" >
Kifungu cha 11(1) cha Sheria ya Maadili kimeainisha wazi mali zinazotakiwa kutajwa kuwa ni fedha taslimu, fedha zilizopo katika taasisi za kifedha kama vile benki, hisa, nyumba, mashamba, magari, mitambo na mali nyinginezo. Kiongozi anatakiwa kutoa tamko la mali anazomiliki yeye mwenyewe, mke/mume na watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane. Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni zinatakiwa kujazwa kila mwaka na kiongozi hutumiwa fomu hizo na Ofisi ya Maadili na pia zinapatikana katika mtandao wa maadili yaani www.ethicssecretariat.go.tz. Sheria inamtaka kiongozi kutolea tamko madeni yake ili kuweza kujua kuwa kiongozi anamiliki mali zipi na pia kutambua kuwa amezipata vipi mali hizo ukilinganisha na kipato cha kiongozi husika. Kiongozi kuwa na mali nyingi si dhambi kwani hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetamka wazi kuwa kila raia ana haki ya kumiliki mali ila ofisi inataka kujiridhisha uhalali wa jinsi mali ilivyopatikana. Mapendekezo katika Katiba mpya yanasisitiza maadili kwa kutenganisha uongozi na biashara.

" >
Wananchi wengi wamejijengea dhana kuwa bila pesa huwezi kupata huduma ya kiserikali kitu ambacho si kweli kwani huduma nyingi za kiserikali zinatolewa bure kabisa ila cha msingi wananchi wanatakiwa kutoa taarifa katika vyombo husika pindi wanapotakiwa kulipia huduma ambazo zinatolewa bure. Jamii inatakiwa kubadilika na kuamini kuwa si lazima kutoa rushwa ndipo upate huduma. Wapo wananchi wengi ambao walileta malalamiko kama hayo na Ofisi ya Maadili iliyashughulikia, hivyo wananchi wasisite kutembelea Ofisi zetu kwa ajili ya kutoa taarifa kama hizo.

" >
Kutoa lugha chafu ni ukiukwaji wa maadili. Ndani ya Bunge kuna Kamati ya Maadili ambayo ipo kwa ajili ya kuwawajibisha wabunge wanaotoa lugha chafu. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa upande wake ilifanya semina kwa wabunge ili kuwakumbusha mipaka ya utendaji kazi na maadili kwa ujumla, na tangu wakati huo matumizi ya lugha chafu bungeni yamepungua kwa kiasi kikubwa.

" >