JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS – SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

PO-ETHICS SECRETARIAT Logo
WAKUU WA VITENGO VYA MANUNUZI NCHINI WATAKWA KUJIEPUSHA NA VITENDO VINAVYOASHIRIA UWEPO WA MGONGANO WA MASLAHI
16 Apr, 2026
WAKUU WA VITENGO VYA MANUNUZI NCHINI WATAKWA KUJIEPUSHA NA VITENDO VINAVYOASHIRIA UWEPO WA MGONGANO WA MASLAHI

Wakuu wa Idara na Vitengo vya Ununuzi na Ugavi wa Taasisi za Umma nchini wametakiwa kuzingatia viwango vya maadili vinavyotambulika katika utaratibu wa ununuzi wa umma nchini, vinavyosisitiza Uadilifu, Usawa, Uaminifu, kuheshimu sheria, uwazi na kuepuka Mgongano wa Maslahi.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Idara ya Ukuzaji wa Maadili Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw. Waziri Kipacha alipokuwa akifungua mafunzo kuhusu maadili kwa wakuu wa Idara/Vitengo vya Ununuzi yaliyofanyika tarehe 16 Aprili, 2026 katika ukumbi wa Hoteli ya SAANAN jijini Dodoma.

Bw. Kipacha katika hotuba yake amebainisha kuwa ununuzi wa umma ndio njia ambayo Serikali inatumia kupata bidhaa na huduma zinazohitajika nchini na kwamba sehemu kubwa ya Bajeti ya Serikali inatumika katika ununuzi wa bidhaa na huduma.

Ameongeza kuwa nchini Tanzania sehemu kubwa ya bajeti ya serikali hutumiwa katika ununuzi wa bidhaa na huduma za umma, hivyo ununuzi wa umma ni mfumo ambao uko katika hatari ya rushwa na kwamba hatari ya vitendo visivyo vya kimaadili katika mchakato wa ununuzi ni kubwa ambayo inahitaji mikakati mahususi ya kuidhibiti.

“Pamoja na kuwepo kwa Sheria, Kanuni na miongozo kuhusiana na ununuzi wa Umma Maadili binafsi ni muhimu katika kuhakikisha ununuzi wa umma kimaadili” amesema.

Aidha amefafanua kuwa kuonekana kwa thamani ya fedha  za Serikali katika ununuzi wa umma kunaanzia katika mchakato na taratibu za ununuzi zilivyofanyika na makosa yoyote ambayo ni kinyume na Maadili katika kusimamia mchakato huo kunasababisha upatikanaji wa bidhaa na huduma hafifu kutoka kwa Wazabuni na kutopatikana kwa thamani halisi ya fedha kutokana na ununuzi uliofanyika na hivyo kutia serikali hasara ambayo italazisha serikali kutumia fedha nyingine kwa ajili ya kupata bidhaa au huduma hiyo tena jambo ambalo ni kinyume na  Maadili.

Awali akitoa neno la ufunguzi, Katibu Msaidizi, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bi. Sigolwike Mkamati alisema kuwa lengo la mafunzo haya ni kuwakumbusha viongozi wa umma kuhusu masuala ya kimaadili ya kuzingatiwa katika utekelezaji wa shughuli za Serikali.

Bi. Mkamati ameyataja baadhi ya malengo hayo kuwa ni pamoja na kusisitiza umuhimu wa kuzingatia maadili ya uongozi ili kudumisha imani ya wananchi kuhusu uwajibikaji wa viongozi wa umma na utaratibu wa kutoa maamuzi serikalini.

Amesema lengo lingine ni kuhimiza masuala yanayohusu mgongano wa maslahi na namna ya kudhibiti ili kulinda maslahi ya umma na pia kukumbushana kuhusu taratibu za Ujazaji wa Tamko la Rasilimali na Madeni kwa njia ya Mtandao (ODS).

Jumla ya mada tatu (3) zimejadiliwa katika mafunzo hayo ambazo ni udhibiti wa Mgongano wa Maslahi katika Ununuzi wa Umma nchini, changamoo za kimaadili na wajibu wa Wakuu wa Idara na Vitengo vya Ununuzi wa Umma kudumisha uadilifu katika mchakato wa ununuzi na Mada ya mwisho ni Mfumo na Ujazaji wa Tamko la Rasilimali na Madeni kwa njia ya Mtandao (Online Declaration System (ODS.)

Online Help
Kuanzisha Enzi Mpya katika Udhibiti wa Sekta ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania
Ofisi ya maadili inafanya kazi na imewashughulikia viongozi wengi sana kupitia Baraza la Maadili ambalo pia liliendeshwa mwaka 2013 Novemba mkoani Tabora. Viongozi mbalimbali waliokuwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili waliitwa kwenye Baraza na kuhojiwa na Baraza linatoa mapendekezo na kuyawasilisha mapendekezo hayo kwa Rais kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu na kisheria kwa viongozi husika.

" >
Kifungu cha 11(1) cha Sheria ya Maadili kimeainisha wazi mali zinazotakiwa kutajwa kuwa ni fedha taslimu, fedha zilizopo katika taasisi za kifedha kama vile benki, hisa, nyumba, mashamba, magari, mitambo na mali nyinginezo. Kiongozi anatakiwa kutoa tamko la mali anazomiliki yeye mwenyewe, mke/mume na watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane. Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni zinatakiwa kujazwa kila mwaka na kiongozi hutumiwa fomu hizo na Ofisi ya Maadili na pia zinapatikana katika mtandao wa maadili yaani www.ethicssecretariat.go.tz. Sheria inamtaka kiongozi kutolea tamko madeni yake ili kuweza kujua kuwa kiongozi anamiliki mali zipi na pia kutambua kuwa amezipata vipi mali hizo ukilinganisha na kipato cha kiongozi husika. Kiongozi kuwa na mali nyingi si dhambi kwani hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetamka wazi kuwa kila raia ana haki ya kumiliki mali ila ofisi inataka kujiridhisha uhalali wa jinsi mali ilivyopatikana. Mapendekezo katika Katiba mpya yanasisitiza maadili kwa kutenganisha uongozi na biashara.

" >
Wananchi wengi wamejijengea dhana kuwa bila pesa huwezi kupata huduma ya kiserikali kitu ambacho si kweli kwani huduma nyingi za kiserikali zinatolewa bure kabisa ila cha msingi wananchi wanatakiwa kutoa taarifa katika vyombo husika pindi wanapotakiwa kulipia huduma ambazo zinatolewa bure. Jamii inatakiwa kubadilika na kuamini kuwa si lazima kutoa rushwa ndipo upate huduma. Wapo wananchi wengi ambao walileta malalamiko kama hayo na Ofisi ya Maadili iliyashughulikia, hivyo wananchi wasisite kutembelea Ofisi zetu kwa ajili ya kutoa taarifa kama hizo.

" >
Kutoa lugha chafu ni ukiukwaji wa maadili. Ndani ya Bunge kuna Kamati ya Maadili ambayo ipo kwa ajili ya kuwawajibisha wabunge wanaotoa lugha chafu. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa upande wake ilifanya semina kwa wabunge ili kuwakumbusha mipaka ya utendaji kazi na maadili kwa ujumla, na tangu wakati huo matumizi ya lugha chafu bungeni yamepungua kwa kiasi kikubwa.

" >