WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR WATEMBELEA MAKAO MAKUU SEKRETARIETI YA MADILI YA VIONGOZI WA UMMA.

Wajumbe wa Kamati ya Baraza la Wawakilishi, Zanzibar inayoshughulikia viongozi wakuu tarehe 22 Agosti, 2023 imetembelea ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma jijini Dodoma kwa lengo la kujifunza jinsi taasisi hiyo inavyotekeleza majukumu yake.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Mchano Othman Said amesema,“tumekuja hapa Dodoma kwa lengo la kujifunza jinsi taasisi yenu inavyofanya kazi.”
Wajumbe wengine wa Kamati hiyo walioshiriki katika ziara ni; Mhe. Mussa Foum Mussa, Mhe. Abdalla Abbas Wadi, Mhe. Maryam Thani Juma, Mhe. Zena Abdallah Salum, Mhe. Haji Shaaban Waziri, Mhe. Ali Alawy Ali, Mhe. Mwaisha Mohammed Kheir, Mhe. Shawana Mohammed Haji, Mhe.Amina Abeid Hemed na Mhe. Massoud Ali Hamad.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, ameomba Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kufanyakazi kwa kushirikiana na Tume ya Maadili ya Zanzibar.
“Naomba ofisi hii ifanyekazi kwa kushirikiana na Tume ya Maadili Zanzibar ili kukuza Maadili ya Viongozi wa Umma nchini,” amesema.
Kwa upande wake Mhe. Sivangilwa mwangesi, Kamishna wa Maadili amewaeleza wajumbe wa kamati kuwa changamoto kubwa inayoikabili Sekretarieti ya Maadili ni, uelewa mdogo wa wananchi kuhusu maadili ya Viongozi wa Umma.
“Wananchi wengi hawana uelewa kuhusu ukiukwaji wa Maadili ya Viongozi wa Umma jambo linalosababisha kutotoa taarifa katika taasisi yetu kuhusu viongozi wanaokiuka maadili kwa mujibu wa Sheria,” amesema.
Amezitaja changamoto nyingine kuwa ni baadhi ya viongozi wa umma kuwa mbali kijiografia kutoka mahali zilipo ofisi zetu na uelewa mdogo wa matumizi ya Teknoloji ya Habari na Mawasiliano kwa wananchi.