JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS – SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

Wachunguzi wapigwa msasa katika uchunguzi wa masuala ya kifedha na kidigitali
27 Oct, 2023
Wachunguzi wapigwa msasa katika uchunguzi wa masuala ya kifedha na kidigitali

Watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambao ni wachunguzi wamepatiwa mafunzo kuhusu Uchunguzi wa fedha na uchunguzi wa kidigtali. Mafunzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa Point Zone Jijini Arusha tarehe 08 Mei,2023.

Akifungua mafunzo hayo Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Sivangilwa Mwangesi alisema kuwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imeona ipo haja ya kuwapatia watumishi hao mafunzo hayo kutokana na kukua kwa sayansi na teknolojia katika maeneo mbalimbali kama vile biashara, mifumo ya fedha , na maeneo mengine ambayo yameleta mabadiliko makubwa katika utendaji kazi wa Serikali na sekta nyingine .

Mhe. Kamishna alieleza kuwa kutokana na changamoto zilizobainika wakati wa utekelezaji wa baadhi ya majukumu ikiwepo suala la kufanya uchunguzi wa masuala ya fedha na uchunguzi wa kidigitali Sekretarieti ya Maadili imeona ipo haja ya kuwapatia watumishi wake mafunzo hayo ili kupata elimu ya uchunguzi wa kiteknolojia.”Tumeona kuwa ni lazima kujifunza na kuelewa namna ya kufanya kazi kulingana na mifumo hii ya kidigitali kadri inavyobadilika ili kupata matokeo mazuri hasa katika nyanja hii ya uchunguzi” alisema.

Aidha Mhe. Kamishna alisema kuwa matarajio ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa umma katika mafunzo hayo ni kuwapata watumishi ambao wataweza kuwa wakufunzi watakaoweza kuwafundisha watumishi wengine namna ya kufanya uchunguzi wa kifedha pamoja na uchunguzi wa kidigitali katika kukusanya taarifa zinazotokana uchunguzi mbalimbali.”Tumewaleteni nyie wachache ili mkawe waalimu kwa watumishi wengine ambao hawapo hapa” alisema .

Awali akielezea majukumu ya Sektetarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Katibu Idara ya Usimamizi wa Maadili Bw, John Kaole alisema kuwa pamoja na majukumu megine Sektetarieti ya Maadili ina jukumu la kupokea fomu za tamko la Rasilimali, Maslahi na Madeni ya viongozi wa umma na kufanya uchunguzi wa awali wa ukiukwaji wa maadili ambao hubainisha kama kuna vihatarishi vyovyote vya ukiukwaji wa Maadili.”Tunafanya uchunguzi wa awali kwa Viongozi wa Umma na endapo tukibaini kuwa kuna ukiukwaji wa maadili tunawapeleka katika Baraza la Maadili kwa ajili ya uchunguzi wa kina” alisema.

Naye mshiriki wa mafunzo hayo ambaye ni Afisa Uchunguzi Mwandamizi kutoka Makao Makuu Dodoma Bw. Gideon Mafwiri alisema kuwa watumishi hao wamekua na changamoto ya kukosa weledi wa kutosha katika uchunguzi wa masuala ya fedha na uchunguzi wa kidigitali iliyopekelea kushindwa kupatataarifa sahihi katika uchunguzi wa masuala ya fedha na kidigitali” Tumekutana na baadhi ya viongozi wa umma hususan wafanyabiashara kuendesha biashara zao kimtandao na sisi hatukuwa na uweledi wa kutosha katika eneo hili la uchunguzi hivyo baada ya mafunzo haya ni imani yetu kwamba tutakuwa na weledi wa kutosha katika maeneo hayo”alisema.

Mafunzo hayo ya siku tano kwa watumishi hao yaliongozwa na waratibu kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kutoka Makao Makuu Dodoma.

Online Help
Kuanzisha Enzi Mpya katika Udhibiti wa Sekta ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania
Ofisi ya maadili inafanya kazi na imewashughulikia viongozi wengi sana kupitia Baraza la Maadili ambalo pia liliendeshwa mwaka 2013 Novemba mkoani Tabora. Viongozi mbalimbali waliokuwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili waliitwa kwenye Baraza na kuhojiwa na Baraza linatoa mapendekezo na kuyawasilisha mapendekezo hayo kwa Rais kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu na kisheria kwa viongozi husika.

" >
Kifungu cha 11(1) cha Sheria ya Maadili kimeainisha wazi mali zinazotakiwa kutajwa kuwa ni fedha taslimu, fedha zilizopo katika taasisi za kifedha kama vile benki, hisa, nyumba, mashamba, magari, mitambo na mali nyinginezo. Kiongozi anatakiwa kutoa tamko la mali anazomiliki yeye mwenyewe, mke/mume na watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane. Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni zinatakiwa kujazwa kila mwaka na kiongozi hutumiwa fomu hizo na Ofisi ya Maadili na pia zinapatikana katika mtandao wa maadili yaani www.ethicssecretariat.go.tz. Sheria inamtaka kiongozi kutolea tamko madeni yake ili kuweza kujua kuwa kiongozi anamiliki mali zipi na pia kutambua kuwa amezipata vipi mali hizo ukilinganisha na kipato cha kiongozi husika. Kiongozi kuwa na mali nyingi si dhambi kwani hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetamka wazi kuwa kila raia ana haki ya kumiliki mali ila ofisi inataka kujiridhisha uhalali wa jinsi mali ilivyopatikana. Mapendekezo katika Katiba mpya yanasisitiza maadili kwa kutenganisha uongozi na biashara.

" >
Wananchi wengi wamejijengea dhana kuwa bila pesa huwezi kupata huduma ya kiserikali kitu ambacho si kweli kwani huduma nyingi za kiserikali zinatolewa bure kabisa ila cha msingi wananchi wanatakiwa kutoa taarifa katika vyombo husika pindi wanapotakiwa kulipia huduma ambazo zinatolewa bure. Jamii inatakiwa kubadilika na kuamini kuwa si lazima kutoa rushwa ndipo upate huduma. Wapo wananchi wengi ambao walileta malalamiko kama hayo na Ofisi ya Maadili iliyashughulikia, hivyo wananchi wasisite kutembelea Ofisi zetu kwa ajili ya kutoa taarifa kama hizo.

" >
Kutoa lugha chafu ni ukiukwaji wa maadili. Ndani ya Bunge kuna Kamati ya Maadili ambayo ipo kwa ajili ya kuwawajibisha wabunge wanaotoa lugha chafu. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa upande wake ilifanya semina kwa wabunge ili kuwakumbusha mipaka ya utendaji kazi na maadili kwa ujumla, na tangu wakati huo matumizi ya lugha chafu bungeni yamepungua kwa kiasi kikubwa.

" >