JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS – SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

PO-ETHICS SECRETARIAT Logo
Waandishi wa vyombo vya habari waaswa kutumia kalam zao vyema.
08 Apr, 2026
Waandishi wa vyombo vya habari waaswa kutumia kalam zao vyema.

Wahariri na waandishi wa vyombo vya habari wameaswa kutumia kalamu zao vyema wakati wa kuandaa na  kuripoti baadhi ya matukio mbalimbali  ili kukuza uadilifu nchini na kuleta Imani ya wananchi kwa viongozi wao na serikali kwa ujumla.

Hayo yalisemwa na Katibu Msaidizi Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kanda ya Mashariki - Morogoro Bw, Hendry Sawe alipokua akifungua mafunzo ya maadili kwa wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari kutoka mkoani Morogoro.Mafunzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa Hazina Ndogo mkoani Morogoro tarehe 08 Aprili,2026

Bw. Sawe alisema kuwa  ni vyema waandishi wa habari wakaandika habari ambazo zina tija kwa wananchi  kwani kile wananchi wanacholishwa  kuhusu viongozi wao ndicho wanachokiamini  “Niwaombe mkatumie kalamu zenu vyema katika kuhabarisha umma na kufichua matendo yasiyo ya kimaadili kwa Viongozi wa Umma”alisema.

Bw, Hendry Sawe alisema kuwa Taasisi imeona vyema kutoa mafunzo ya maadili kwa wanahabari hao ikiwa na lengo la kuimarisha mashirikiano kati ya Taasisi  kama msimamizi wa maadili na vyombo vya habari kama mdau muhimu wa ukuzaji wa maadili.

“Tumeandaa mafunzo haya mahsusi kwa wahariri na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari kwa sababu tunajua vyombo hivi ni wadau wakubwa wa ukuzaji wa maadili hivyo tumekuja kujadiliana namna gani tunaweza kukuza hali ya maadili ya Viongozi wa Umma nchini”alisema.

Naye Msimamizi wa ITV media mkoa wa Morogoro Bi. Idda Mushi alisema kuwa mafunzo hayo yatakua manufaa makubwa kwa waandishi wa habari katika kuandaa na kuandika habari mbalimbali “Sote ni mashahidi hatujatoka patupu tumeelimishwa kuhusu mambo mbalimbali ya kimaadili ambayo mengi tulikua hatuyafahamu kwa hiyo niwasihi wenzangu tukitoka hapa tukaandae Makala, habari mbalimbali za kimaadili zenye faida kwa jamii kwa ujumla” alisema.

Bi. Idda alisisitiza suala zima la waandishi kuwa wazalendo katika utekelezaji wa majukumu yao ya uandishi kwani kukosa uzalendo kwa mwandishi kunaweza kuiathiri nchi .“Ndugu zangu niwakumbushe kuwa Tanzania  ni moja na ni yetu sote hakuna mtu  atakayetoka  nje na kuja kuijenga kwa hiyo kila tunachokifanya tuwe wazalendo na nchi yetu tukitumia vibaya kalamu zetu tunaweza kuharibu badala ya kuijenga nchi yetu kama ambayo tumekusudia” alisema.

Mada mbili ziliwasilishwa katika mafunzo hayo ambayo ni mada kuhusu Sheria ya Maadili pamoja na mada kuhusu majukumu ya Sekretarieti ya Maadili.

 

Online Help
Kuanzisha Enzi Mpya katika Udhibiti wa Sekta ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania
Ofisi ya maadili inafanya kazi na imewashughulikia viongozi wengi sana kupitia Baraza la Maadili ambalo pia liliendeshwa mwaka 2013 Novemba mkoani Tabora. Viongozi mbalimbali waliokuwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili waliitwa kwenye Baraza na kuhojiwa na Baraza linatoa mapendekezo na kuyawasilisha mapendekezo hayo kwa Rais kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu na kisheria kwa viongozi husika.

" >
Kifungu cha 11(1) cha Sheria ya Maadili kimeainisha wazi mali zinazotakiwa kutajwa kuwa ni fedha taslimu, fedha zilizopo katika taasisi za kifedha kama vile benki, hisa, nyumba, mashamba, magari, mitambo na mali nyinginezo. Kiongozi anatakiwa kutoa tamko la mali anazomiliki yeye mwenyewe, mke/mume na watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane. Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni zinatakiwa kujazwa kila mwaka na kiongozi hutumiwa fomu hizo na Ofisi ya Maadili na pia zinapatikana katika mtandao wa maadili yaani www.ethicssecretariat.go.tz. Sheria inamtaka kiongozi kutolea tamko madeni yake ili kuweza kujua kuwa kiongozi anamiliki mali zipi na pia kutambua kuwa amezipata vipi mali hizo ukilinganisha na kipato cha kiongozi husika. Kiongozi kuwa na mali nyingi si dhambi kwani hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetamka wazi kuwa kila raia ana haki ya kumiliki mali ila ofisi inataka kujiridhisha uhalali wa jinsi mali ilivyopatikana. Mapendekezo katika Katiba mpya yanasisitiza maadili kwa kutenganisha uongozi na biashara.

" >
Wananchi wengi wamejijengea dhana kuwa bila pesa huwezi kupata huduma ya kiserikali kitu ambacho si kweli kwani huduma nyingi za kiserikali zinatolewa bure kabisa ila cha msingi wananchi wanatakiwa kutoa taarifa katika vyombo husika pindi wanapotakiwa kulipia huduma ambazo zinatolewa bure. Jamii inatakiwa kubadilika na kuamini kuwa si lazima kutoa rushwa ndipo upate huduma. Wapo wananchi wengi ambao walileta malalamiko kama hayo na Ofisi ya Maadili iliyashughulikia, hivyo wananchi wasisite kutembelea Ofisi zetu kwa ajili ya kutoa taarifa kama hizo.

" >
Kutoa lugha chafu ni ukiukwaji wa maadili. Ndani ya Bunge kuna Kamati ya Maadili ambayo ipo kwa ajili ya kuwawajibisha wabunge wanaotoa lugha chafu. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa upande wake ilifanya semina kwa wabunge ili kuwakumbusha mipaka ya utendaji kazi na maadili kwa ujumla, na tangu wakati huo matumizi ya lugha chafu bungeni yamepungua kwa kiasi kikubwa.

" >