JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS – SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

PO-ETHICS SECRETARIAT Logo
Vyombo vya habari vyatajwa nguzo muhimu katika kukuza na kuimarisha maadili nchini
09 Apr, 2026
Vyombo vya habari vyatajwa nguzo muhimu katika kukuza na kuimarisha maadili nchini

Vyombo vya habari nchini vimetajwa kuwa nguzo muhimu katika kukuza na kuimarisha maadili kwa Viongozi wa Umma na Taifa kwa ujumla.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Msaidizi Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda Maalum Bi. Elizabeth Komba wakati akifungua kikao kazi na wadau wa habari wa Kanda hiyo ambao ni wamiliki, wahariri na waandishi wa habari kwa lengo la kujenga ushirikiano endelevu kati ya Taasisi hiyo na vyombo vya habari nchini.

Kikao kazi hicho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Shule ya Uongozi Mwalimu Nyerere mjini Kibaha mkoani Pwani tarehe 9 Aprili, 2026.

Katika hotuba yake kwa wadau hao Bi. Elizabeth alisema kuwa vyombo vya habari sio kioo tu cha jamii bali ni chombo cha kuunda na kukuza maadili nchini.

“Tunaamini kuwa vyombo vya habari vina nafasi ya kipekee katika kukuza maadili, uwajibikaji na uwazi katika jamii, kwa maneno mengine nyinyi ni nguzo muhimu katika kujenga au kubomoa maadili katika jamii, hivyo tutumie tasnia hii kujenga jamii yenye uadilifu,” alisema Bi. Elizabeth.

Aidha Bi. Elizabeth ameongeza kuwa vyombo vya habari vina nafasi kubwa katika kukuza uwajibikaji kwa kufichua vitendo vya rushwa, ubadhilifu au matumizi mabaya ya madaraka kwani vinaweka wazi ukweli ambao ni rahisi kwa muhusika kuwajibika.

“Kama tukitumia vyombo vya habari kwa njia sahihi tunaweza kujenga jamii yenye uadilifu uwazi na haki na tukivitumia vibaya tunaweza kuharibu maadili na kuleta migawanyiko miongoni mwetu na hatimaye kujenga jamii isiyokua na uzalendo,” alisisitiza.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw. Omary Juma amesema kuwa ushirikiano huo utakua endelevu na mara kwa mara watakua wanakutana kwa lengo la kufanya majadiliano kwa ajili ya kupata namna bora ya  kukuza na kuimarisha maadili nchini.

Online Help
Kuanzisha Enzi Mpya katika Udhibiti wa Sekta ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania
Ofisi ya maadili inafanya kazi na imewashughulikia viongozi wengi sana kupitia Baraza la Maadili ambalo pia liliendeshwa mwaka 2013 Novemba mkoani Tabora. Viongozi mbalimbali waliokuwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili waliitwa kwenye Baraza na kuhojiwa na Baraza linatoa mapendekezo na kuyawasilisha mapendekezo hayo kwa Rais kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu na kisheria kwa viongozi husika.

" >
Kifungu cha 11(1) cha Sheria ya Maadili kimeainisha wazi mali zinazotakiwa kutajwa kuwa ni fedha taslimu, fedha zilizopo katika taasisi za kifedha kama vile benki, hisa, nyumba, mashamba, magari, mitambo na mali nyinginezo. Kiongozi anatakiwa kutoa tamko la mali anazomiliki yeye mwenyewe, mke/mume na watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane. Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni zinatakiwa kujazwa kila mwaka na kiongozi hutumiwa fomu hizo na Ofisi ya Maadili na pia zinapatikana katika mtandao wa maadili yaani www.ethicssecretariat.go.tz. Sheria inamtaka kiongozi kutolea tamko madeni yake ili kuweza kujua kuwa kiongozi anamiliki mali zipi na pia kutambua kuwa amezipata vipi mali hizo ukilinganisha na kipato cha kiongozi husika. Kiongozi kuwa na mali nyingi si dhambi kwani hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetamka wazi kuwa kila raia ana haki ya kumiliki mali ila ofisi inataka kujiridhisha uhalali wa jinsi mali ilivyopatikana. Mapendekezo katika Katiba mpya yanasisitiza maadili kwa kutenganisha uongozi na biashara.

" >
Wananchi wengi wamejijengea dhana kuwa bila pesa huwezi kupata huduma ya kiserikali kitu ambacho si kweli kwani huduma nyingi za kiserikali zinatolewa bure kabisa ila cha msingi wananchi wanatakiwa kutoa taarifa katika vyombo husika pindi wanapotakiwa kulipia huduma ambazo zinatolewa bure. Jamii inatakiwa kubadilika na kuamini kuwa si lazima kutoa rushwa ndipo upate huduma. Wapo wananchi wengi ambao walileta malalamiko kama hayo na Ofisi ya Maadili iliyashughulikia, hivyo wananchi wasisite kutembelea Ofisi zetu kwa ajili ya kutoa taarifa kama hizo.

" >
Kutoa lugha chafu ni ukiukwaji wa maadili. Ndani ya Bunge kuna Kamati ya Maadili ambayo ipo kwa ajili ya kuwawajibisha wabunge wanaotoa lugha chafu. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa upande wake ilifanya semina kwa wabunge ili kuwakumbusha mipaka ya utendaji kazi na maadili kwa ujumla, na tangu wakati huo matumizi ya lugha chafu bungeni yamepungua kwa kiasi kikubwa.

" >