JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS – SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

PO-ETHICS SECRETARIAT Logo
Vyombo vya habari ni daraja la kukuza Maadili ya Viongozi wa Umma.
10 Apr, 2026
Vyombo vya habari ni daraja la kukuza Maadili ya Viongozi wa Umma.

Vyombo vya habari nchini vimetajwa kuwa daraja kati ya wananchi na Viongozi wao  katika kukuza na kuimarisha maadili ya Viongozi wa Umma na serikali kwa ujumla.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Msaidizi Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Mashariki Bw. Hendry Sawe wakati akifungua kikao kazi na wadau wa habari wa mkoa wa Tanga . Wadau hao ni wamiliki, wahariri na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali mkoani Tanga.

Kikao kazi hicho kilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Bandari mkoani Tanga terehe 10 Aprili, 2026.

Katika hotuba yake kwa wadau hao Bw. Sawe alisema kuwa vyombo vya habari ni kiungo muhimu kati ya viongozi na wananchi pale vinapotekeleza wajibu wao kwa weledi na uadilifu wa hali ya juu vitachangia kwa kiasi kikubwa kujenga viongozi  waadilifu na jamii yenye misingi imara ya maadili.

Katika hatua nyingine Bw. Sawe alieleza kuwa vyombo vya habari vinaweza kusaidia kukuza maadili ya viongozi kwa kuandaa Makala ama vipindi vinavyoeleza kuhusu maadili ya viongozi, kuibua na kufichua vitendo visivyo vya kimaadili kama rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na mambo mengine kama hayo.

“Kumekua na changamoto ya Baadhi ya Vyombo vya habari kutoa habari za upotoshaji taarifa zisizo sahihi zinazosababisha kuporomoka kwa Imani ya wananchi dhidi ya Taasisi za Umma na Serikali kwa ujumla hivyo niwaombe mkatoe taarifa za ukweli na zenye takwimu sahihi zenye lengo la kuijenga nchi yetu” alisema.

Bw. Sawe alieleza kuwa  lengo la kikao kazi hicho ni kujenga ushirikiano endelevu kati ya Taasisi hiyo na vyombo vya habari nchini “Kama Taasisi tumeona ni vyema kufanya kikao kazi na nyinyi ili tuweze kujadiliana ni namna gani tunaweza kukuza maadili ya Viongozi wa Umma kupitia vyombo vya habari ambavyo ndio daraja kati ya wananchi na serikali ambayo inaongozwa na viongozi mbalimbali”alisema.

Naye  Bi. Evelyn Balozi  Meneja wa kituo cha redio cha Utume Fm kutoka wilayani Lushoto alisema kuwa kikao kazi hicho kimekua na manufaa makubwa kwa wanahabari hao kwani kimewapa fursa ya kuifahamu kwa kina  Sekretarieti ya Maadili ikiwa ni pamoja na majukumu yake na misingi ya Viongozi wanayopaswa kuifuata ’’Kupitia kikao kazi hiki tumejifunza pia  kuwa ni namna gani tunawajibika kuwa daraja kati ya Sekretarieti ya Maadili na jamii kwa kuibua matendo yasiyo ya kimaadili yanayofanywa na Viongozi pamoja  na kuelimisha jamii kuhusiana na masuala ya kimaadili’’ alisema.

Mada mbili ziliwasilishwa katika kikao kazi hicho ambazo ni pamoja na mada kuhusu Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma  sura 398 pamoja na mada Ushirikiano wa Sekretarieti ya Maadili na vyombo vya habari.

 

 

Online Help
Kuanzisha Enzi Mpya katika Udhibiti wa Sekta ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania
Ofisi ya maadili inafanya kazi na imewashughulikia viongozi wengi sana kupitia Baraza la Maadili ambalo pia liliendeshwa mwaka 2013 Novemba mkoani Tabora. Viongozi mbalimbali waliokuwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili waliitwa kwenye Baraza na kuhojiwa na Baraza linatoa mapendekezo na kuyawasilisha mapendekezo hayo kwa Rais kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu na kisheria kwa viongozi husika.

" >
Kifungu cha 11(1) cha Sheria ya Maadili kimeainisha wazi mali zinazotakiwa kutajwa kuwa ni fedha taslimu, fedha zilizopo katika taasisi za kifedha kama vile benki, hisa, nyumba, mashamba, magari, mitambo na mali nyinginezo. Kiongozi anatakiwa kutoa tamko la mali anazomiliki yeye mwenyewe, mke/mume na watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane. Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni zinatakiwa kujazwa kila mwaka na kiongozi hutumiwa fomu hizo na Ofisi ya Maadili na pia zinapatikana katika mtandao wa maadili yaani www.ethicssecretariat.go.tz. Sheria inamtaka kiongozi kutolea tamko madeni yake ili kuweza kujua kuwa kiongozi anamiliki mali zipi na pia kutambua kuwa amezipata vipi mali hizo ukilinganisha na kipato cha kiongozi husika. Kiongozi kuwa na mali nyingi si dhambi kwani hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetamka wazi kuwa kila raia ana haki ya kumiliki mali ila ofisi inataka kujiridhisha uhalali wa jinsi mali ilivyopatikana. Mapendekezo katika Katiba mpya yanasisitiza maadili kwa kutenganisha uongozi na biashara.

" >
Wananchi wengi wamejijengea dhana kuwa bila pesa huwezi kupata huduma ya kiserikali kitu ambacho si kweli kwani huduma nyingi za kiserikali zinatolewa bure kabisa ila cha msingi wananchi wanatakiwa kutoa taarifa katika vyombo husika pindi wanapotakiwa kulipia huduma ambazo zinatolewa bure. Jamii inatakiwa kubadilika na kuamini kuwa si lazima kutoa rushwa ndipo upate huduma. Wapo wananchi wengi ambao walileta malalamiko kama hayo na Ofisi ya Maadili iliyashughulikia, hivyo wananchi wasisite kutembelea Ofisi zetu kwa ajili ya kutoa taarifa kama hizo.

" >
Kutoa lugha chafu ni ukiukwaji wa maadili. Ndani ya Bunge kuna Kamati ya Maadili ambayo ipo kwa ajili ya kuwawajibisha wabunge wanaotoa lugha chafu. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa upande wake ilifanya semina kwa wabunge ili kuwakumbusha mipaka ya utendaji kazi na maadili kwa ujumla, na tangu wakati huo matumizi ya lugha chafu bungeni yamepungua kwa kiasi kikubwa.

" >