Viongozi watakiwa kuepuka vitendo visivyo vya Maadili:

Viongozi wa Umma wametakiwa kuepuka vitendo visivyo na maadili katika utekelezaji wa majukumu yao katika kuwatumikia wananchi.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu tawala wa mkoa wa Tabora Bw Daniel Barago alipokuwa akifungua mafunzo kuhusu sheria ya maadili ya viongozi wa umma kwa Viongozi wa mkoa huo yaliyofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tabora tarehe 14 Februari 2023.
Bwana Barago katika hotuba yake amevitaja vitendo hivyo visivyo na maadili ambavyo ni utoajin wa huduma usioridhisha kwa wananchi, kujihusisha na mgongano wa maslahi, matumizi mabaya ya madaraka, wizi na ubadhirifu wa mali za umma, rushwa, unyanyasaji wa kijinsia, matumizi ya lugha chafu, na kwamba vitendo hivyo vinaashiria ukosefu wa maadili.
Aidha Bwana Barago alifafanua kuwa, ni muhimu kwa viongozi kutenda kazi kwa kuzingatia Maadili, kwani matumaini ya wananchi kwa serikali yao ni kuapatia huduma bora kwa wakati na bila upendeleo.
“Tanzania inahitaji kuwa na viongozi ambao ni mfano mzuri wa uzingatiaji wa maadili, unaozingatia Sheria, Kanuni na Taratibu katika utendaji wao wa kazi alisisitiza”
Katibu Tawala huyo katika hotuba yake alisisitiza kuwa kiongozi anatakiwa kutotumia vibaya raslimali za umma, kujizuia na mgongano wa maslahi, kutojilimbikizia mali na kutotumia madaraka yake vibaya na kwamba maadili hayo yamelenga katika kuhakikisha kuwa viongozi wa Umma wamatekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu, uwazi, haki, kutopendelea na uwajibikaji ili kujenga, kudumisha na kulinda imani ya wananchi kwa viongozi na Serikali yao.
Bwana Barago aliongeza kuwa, Tanzania inahitaji kuwa na viongozi ambao ni mfano mzuri wa uzingatiaji wa maadili, wanaozingatia Sheria, Kanuni na Taratibu katika utendaji wao wa kazi na kwamba wana dhima ya kuhakikisha kuwa wanazingatia viwango vya juu vya maadili na kujiepusha na mgongano wa maslahi ili kuimarisha imani ya wananchi kuhusu uadilifu wao na katika utaratibu wa kufanya maamuzi ya Serikali.
Aliongeza kuwa, Kiongozi wa siasa au mtumishi yoyote wa umma anatakiwa atumie wadhifa wake kwa maslahi ya umma na wananchi kwa ujumla na sio kwa manufaa yake binafsi.
Mafunzo hayo kuhusu Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma yamewashirikisha