JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS – SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

PO-ETHICS SECRETARIAT Logo
Viongozi wapigwa msasa kuhusu Ujazaji wa Tamko la Rasilimali na Madeni kwa njia ya mtandao.
03 Mar, 2026
Viongozi wapigwa msasa kuhusu Ujazaji wa Tamko la Rasilimali na Madeni kwa njia ya mtandao.

Viongozi na Maafisa TEHAMA kutoka mkoa wa Morogoro wamepatiwa mafunzo juu ya namna ya ujazaji wa Tamko la Rasilimali na Madeni kwa njia ya Mtandao (ODS). Mafunzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro tarehe 03 Machi,2026

Akifungua mafunzo hayo Katibu Msaidizi Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Mashariki – Morogoro Bw. Hendry Sawe alisema kuwa pamoja na majukumu mengine yanayotekelezwa na Sekretarieti ya Maadili Taasisi hii pia ina jukumu la kupokea matamko yanayotolewa na Viongozi wa Umma.

“Ifahamike kuwa Utoaji wa Tamko hili ni takwa la kisheria, Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma kifungu cha 9 kifungu kidogo cha 1 kinawataka Viongozi wa Umma kutoa matamko yao pindi wanapoingia katika nafasi zao za uongozi ndani ya siku 30 na pia kila ifikapo 31 Desemba ya kila mwaka   na hata wanapoondoka katika nafasi zao za uongozi” alisema.

Bw. Sawe alieleza kuwa tangu kuanzishwa kwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma mwaka 1995 na utekelezaji wa sheria 1996 Viongozi wa Umma walikua wakitoa matamko yao kwa njia ya nakala ngumu jambo ambalo lilikuwa lianachelewesha zoezi hilo na kulifanya kuwa gumu

“Kutokana na mabadiliko ya Sayansi na teknolojia yameisukuma Serikali kuja na mkakati wa Tehama lakini pia sera ya TEHAMA 2022/27 unaohamasisha matumizi ya TEHAMA sera ya TEHAMA 2025 inaeleza umuhimu wa Taasisi za Umma kutumia teknolojia” alisema.

Bw. Sawe aliendelea kusema kuwa kutokana na mabadiliko hayo mwaka 2025 Sekretarieti ya Maadili ilianzisha mfumo wa ujazaji wa Tamko la Rasilimali na Madeni kwa njia ya mtandao lengo likiwa ni kurahisiha zoezi hilo linalowasaidia Viongozi kujaza fomu hii mahali popote alipo na bila changamoto yoyote.

“Sisi kama Sekretarieti tunatamani kuona Viongozi wanaweza kutekeleza takwa hili la kisheria bia changamoto yoyote.

Katika hatua nyingine Bw. Sawe alitoa rai kwa Viongozi hao kuhakikisha kuwa wanatimiza takwa hilo la kisheria ili kukuza uadilifu nchini.

“Ikumbukwe kwamba ni kinyume na sheria kwa Viongozi wa Umma kushindwa kutoa ama kuchelewa kutoa tamko la rasilimali na madeni” alisema.

Naye mshiriki wa mafunzo hayo ambae ni Mkuu wa Hazina ndogo mkoani Morogoro Bw, Abubakar Nacharo ameishukuru Sekretarieti ya Maadili kwa kuanzisha mfumo huu wa ujazaji wa tamko kwa njia ya mtandao kwani unawasaidia Viongozi kujaza kwa h

“Niishukuru Sekretarieti ya Maadili kwa kuamua kuja kutukumbusha wajibu wa kuzingatia na namna ya ujazaji wa fomu hizi kwa njia ya mtandao, hapo awali tulikua tunajaza kwenye karatasi mara nyingine tunakosea na pia inachukua muda mwingi lakini sasa mfumo huu utatuwezesha kujaza kwa uharaka, usahihi na kwa uadilifu wa hali ya juu” alisema.

Mada mbili ziliwasilishwa katika mafunzo hayo ambazo ni pamoja na mada kuhusu Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma pamoja na mada kuhusu Ujazaji wa Tamko la Rasilimali na Madeni kwa njia ya mtandao.

 

Online Help
Kuanzisha Enzi Mpya katika Udhibiti wa Sekta ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania
Ofisi ya maadili inafanya kazi na imewashughulikia viongozi wengi sana kupitia Baraza la Maadili ambalo pia liliendeshwa mwaka 2013 Novemba mkoani Tabora. Viongozi mbalimbali waliokuwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili waliitwa kwenye Baraza na kuhojiwa na Baraza linatoa mapendekezo na kuyawasilisha mapendekezo hayo kwa Rais kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu na kisheria kwa viongozi husika.

" >
Kifungu cha 11(1) cha Sheria ya Maadili kimeainisha wazi mali zinazotakiwa kutajwa kuwa ni fedha taslimu, fedha zilizopo katika taasisi za kifedha kama vile benki, hisa, nyumba, mashamba, magari, mitambo na mali nyinginezo. Kiongozi anatakiwa kutoa tamko la mali anazomiliki yeye mwenyewe, mke/mume na watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane. Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni zinatakiwa kujazwa kila mwaka na kiongozi hutumiwa fomu hizo na Ofisi ya Maadili na pia zinapatikana katika mtandao wa maadili yaani www.ethicssecretariat.go.tz. Sheria inamtaka kiongozi kutolea tamko madeni yake ili kuweza kujua kuwa kiongozi anamiliki mali zipi na pia kutambua kuwa amezipata vipi mali hizo ukilinganisha na kipato cha kiongozi husika. Kiongozi kuwa na mali nyingi si dhambi kwani hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetamka wazi kuwa kila raia ana haki ya kumiliki mali ila ofisi inataka kujiridhisha uhalali wa jinsi mali ilivyopatikana. Mapendekezo katika Katiba mpya yanasisitiza maadili kwa kutenganisha uongozi na biashara.

" >
Wananchi wengi wamejijengea dhana kuwa bila pesa huwezi kupata huduma ya kiserikali kitu ambacho si kweli kwani huduma nyingi za kiserikali zinatolewa bure kabisa ila cha msingi wananchi wanatakiwa kutoa taarifa katika vyombo husika pindi wanapotakiwa kulipia huduma ambazo zinatolewa bure. Jamii inatakiwa kubadilika na kuamini kuwa si lazima kutoa rushwa ndipo upate huduma. Wapo wananchi wengi ambao walileta malalamiko kama hayo na Ofisi ya Maadili iliyashughulikia, hivyo wananchi wasisite kutembelea Ofisi zetu kwa ajili ya kutoa taarifa kama hizo.

" >
Kutoa lugha chafu ni ukiukwaji wa maadili. Ndani ya Bunge kuna Kamati ya Maadili ambayo ipo kwa ajili ya kuwawajibisha wabunge wanaotoa lugha chafu. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa upande wake ilifanya semina kwa wabunge ili kuwakumbusha mipaka ya utendaji kazi na maadili kwa ujumla, na tangu wakati huo matumizi ya lugha chafu bungeni yamepungua kwa kiasi kikubwa.

" >