JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS – SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

PO-ETHICS SECRETARIAT Logo
Viongozi wa Umma watakiwa kutenda haki wanapotekeleza majukumu yao
12 Feb, 2026
Viongozi wa Umma watakiwa kutenda haki wanapotekeleza majukumu yao

Wito umetolewa kwa Viongozi wa Umma kuongozwa na dhamira ya kutenda haki bila woga wanapotekeleza majukumu yao.

Wito huo umetolewa na Katibu Idara ya Ukuzaji wa Maadili kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw. Waziri Kipacha wakati akitoa mafunzo kuhusu Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa Waheshimiwa Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria.

Mafunzo hayo yametolewa  katika kikao kati ya Kamati hiyo na Taasisi zilizopo chini ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilichofanyika katika ofisi za Bunge jijini Dodoma tarehe 11 na  12 Februari, 2026.

Bw. Kipacha amesema kuwa, “Viongozi wa Umma wanapotekeleza majukumu yao wanapaswa kuongozwa na dhamira ya kutekeleza majukumu kwa uadilifu, uaminifu, haki, bila woga au upendeleo ili kuongeza imani ya wananchi kwa Serikalii yao,” ameeleza.

Kwa mujibu wa Bw. Kipacha, msingi huu ukipuuzwa hupunguza imani ya wananchi kuhusu uadilifu wa Viongozi wa Umma na utaratibu mzima wa utoaji maamuzi katika Taasisi za Umma.

“Viongozi wa Umma wamepewa dhamana ya kufanya maamuzi kwa niaba ya wananchi hivyo, inawalazimu kuzingatia viwango vya juu vya maadili.”

Amezitaja baadhi ya faida za maadili kuwa ni kuelewa, kuchambua na kupambanua mambo mema na maovu, mazuri na mabaya, mambo yanayokubalika na yasiyokubalika, yanayositirika na yasiyositirika na kuamua kutenda jambo sahihi wakati wote, mahali popote hata kama hakuna mtu anayekuona.

Katika mafunzo hayo, Bw. Kipacha amewakumbusha Waheshimiwa wabunge kuwa, “iwapo Mhe. Mbunge atakiuka Ibara ya 67 (1)(d) na 71 (1)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, uchaguzi Mkuu wa mwaka 2030 utakuwa haumuhusu.”

Katika kikao hicho Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala ,Katiba na Sheria ilikua chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Dkt. Damas Daniel Ndumbaro (Mb), wakati Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora iliwakilishwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Regina Qwaray (Mb).

Online Help
Kuanzisha Enzi Mpya katika Udhibiti wa Sekta ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania
Ofisi ya maadili inafanya kazi na imewashughulikia viongozi wengi sana kupitia Baraza la Maadili ambalo pia liliendeshwa mwaka 2013 Novemba mkoani Tabora. Viongozi mbalimbali waliokuwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili waliitwa kwenye Baraza na kuhojiwa na Baraza linatoa mapendekezo na kuyawasilisha mapendekezo hayo kwa Rais kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu na kisheria kwa viongozi husika.

" >
Kifungu cha 11(1) cha Sheria ya Maadili kimeainisha wazi mali zinazotakiwa kutajwa kuwa ni fedha taslimu, fedha zilizopo katika taasisi za kifedha kama vile benki, hisa, nyumba, mashamba, magari, mitambo na mali nyinginezo. Kiongozi anatakiwa kutoa tamko la mali anazomiliki yeye mwenyewe, mke/mume na watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane. Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni zinatakiwa kujazwa kila mwaka na kiongozi hutumiwa fomu hizo na Ofisi ya Maadili na pia zinapatikana katika mtandao wa maadili yaani www.ethicssecretariat.go.tz. Sheria inamtaka kiongozi kutolea tamko madeni yake ili kuweza kujua kuwa kiongozi anamiliki mali zipi na pia kutambua kuwa amezipata vipi mali hizo ukilinganisha na kipato cha kiongozi husika. Kiongozi kuwa na mali nyingi si dhambi kwani hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetamka wazi kuwa kila raia ana haki ya kumiliki mali ila ofisi inataka kujiridhisha uhalali wa jinsi mali ilivyopatikana. Mapendekezo katika Katiba mpya yanasisitiza maadili kwa kutenganisha uongozi na biashara.

" >
Wananchi wengi wamejijengea dhana kuwa bila pesa huwezi kupata huduma ya kiserikali kitu ambacho si kweli kwani huduma nyingi za kiserikali zinatolewa bure kabisa ila cha msingi wananchi wanatakiwa kutoa taarifa katika vyombo husika pindi wanapotakiwa kulipia huduma ambazo zinatolewa bure. Jamii inatakiwa kubadilika na kuamini kuwa si lazima kutoa rushwa ndipo upate huduma. Wapo wananchi wengi ambao walileta malalamiko kama hayo na Ofisi ya Maadili iliyashughulikia, hivyo wananchi wasisite kutembelea Ofisi zetu kwa ajili ya kutoa taarifa kama hizo.

" >
Kutoa lugha chafu ni ukiukwaji wa maadili. Ndani ya Bunge kuna Kamati ya Maadili ambayo ipo kwa ajili ya kuwawajibisha wabunge wanaotoa lugha chafu. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa upande wake ilifanya semina kwa wabunge ili kuwakumbusha mipaka ya utendaji kazi na maadili kwa ujumla, na tangu wakati huo matumizi ya lugha chafu bungeni yamepungua kwa kiasi kikubwa.

" >