JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS – SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

Viongozi wa Umma wasisitizwa kufanya kazi kwa kushirikiana
29 Aug, 2023
Viongozi wa Umma wasisitizwa kufanya kazi kwa kushirikiana

Viongozi wa Umma wameaswa kuwa na uwajibikaji wa pamoja katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku. Hayo yalisema na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini Mhe. Benno Malisawakati akifungua mafunzo kwa Viongozi wa Umma wa Halmashauri mbili za Mkoa wa Mbeya ambazo ni halmashauri ya Jiji la Mbeyana halmashauri ya Mbeya DC Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Sekretariti ya Maadili ya Viongozi wa Umma yalifanyika katika Ukumbi wa Jengo la NHIF Jijini Mbeya tarehe 05 Mei,2023.

Akifungua mafunzo hayo Mhe. Malisa alieleza kuwa ni dhahiri kuwa Viongozi wote katika Halmashauri hizo wanapaswa kufanya kazi kwa kushirikiana kwa pamoja , kuwa na mawazo na uelekeo mmoja ili kurahisisha utekelezaji wa shughuli zote za serikali na kuweza kuleta matokeo chanya kwa wananchi na serikali kwa ujumla.

Mhe. Malisa alifafanua kuwa serikali inapeleka fedhanyingisana katika halmashauri mbalimbalinchini kwa sababu ndipo kunakotekelezwa miradi mingi inayowagusa wananchi moja kwa moja kama vile maji, elimu , afya na nyingine nyingi “Ndugu zangufursa hii tukaitumie vizuri ili matokeo ya fedha hizi yakaonekane wazi huu sio muda wa kulumbana, sio muda wa kususiana majukumu,sio muda wa kunyoosheana vidole bali ni muda wa kuunda timu moja, ni muda wa kila mmoja kuwajibika ipasavyo katika nafasi aliyo nayo nakufanya kazi kwa bidii ili tukaaminike kwa viongozi wetu wa juu” alisema.

Aidha Mhe. Malisa aliendelea kusema kuwaViongozi wanapowajibika kwa pamoja itarahisha utendaji kazi wao wa kila siku wa kuhakikisha kuwa wananchi wanatekelezewa miradi yote kama ilivyopangwa jambo linakalowafanya wananchikuwa na Imani na viongozi wao na kuiamini serikali kwa ujumla wake “Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu” alisema.

Pamoja na hayo Mhe. Malisa alizungumzia suala la mgongano wa maslahi kuwa limekua ni tatizo kubwa sana katika Halmashauri nyingi nchini. Suala hili limekua na changamoto nyingi katika kutekeleza miradi mbalimbali, Kiongozi anapokua na maslah binafsi katika mradi fulani husababisha kucheleweshwa kwa miradi hiyo ama kutekelezwa kwa kiwango kisichoridhisha ama kutokutekeleza kabisa kutokana na mvutano unaokuepobaina ya watekelezaji kwa sababu ya maslah binafsi.” Viongozi wenzangu hatukuteuliwa tukafanye kazi kwa kuangalia maslah yetu binafsi, tumeteuliwa tukawatumikie wananchi bila kutanguliza maslah yetu mbele tukatangulize maslah ya wananchi na Taifa kwa ujumla: alisema.

Awali akielezea dhumuni kubwa la mafunzo hayo Katibu Msaidizi Kanda yaNyanda za Juu kusini -Mbeya Bw, Pauline Kanoni alisema kuwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ina jukumu kubwa la kutoa elimu ya maadili kwa Viongozi wa Umma nchini ili kuwa na Viongozi waadilifu na wenye kuaminika kwa wanachi wao.

Pamoja na hayo Bw. Kanoni alisema kuwa mafunzo hayo yana lengo la kuwakumbusha Viongozi kuhusu Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Namba13ya mwaka 1995. Katika kuzingatia sheria hii yapo mambo ambayo viongozi wanapaswa kuzingatia wanapotekeleza majukumu yaokwa kuzingatia kanuni za Maadili pamoja na misingi ambayo imewekwa kulingana na sheria na katiba , kuwa wawazi kwenye shughuli wanazofanya na kutumia rasilimali za Umma vizuri.” Niwaase Viongozi kuwa na uwajibikaji wa pamoja katika kutekeleza majukumu yenu kwani haiwezekani Kiongozi anakwenda kinyume na maelekezo ya serikali , unakuta kingozi huyu anasema hivi mwingine anasema hivi hayo sio maadili viongozi wote wanapaswa kuwa na kauli moja“ alisema.

“Tunajua viongozi wetu sio kwamba hamna Maadili tunajua kuwa ni waadilifu wa kutosha lakini tumekuja kukumbushana tuu kwa sababu tunajua binadamu tunasahau hivyo tunakumbushana nini tunapaswa kufanya nini hatupaswi kufanya wakati wa utekelezaji wa majukumu yetu kwani kiongozi akikiuka maadili anaitia doa serikali yetu” alisema

Naye mshiriki wa mafunzo hayo Afisa Kilimo katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya Bi. Amina Nalicho alisema kuwa ili kuweza kupata matokeo chanya kwaserikali na wanachini dhahiri kuwa Viongozi wanapaswa kufanya kazi kwa pamoja“ kuna msemo usemao kidole kimoja hakivunji chawa” alisema.

Katika mafunzo hayo ya siku moja yalitolewakwa viongozi wapya ambao ni wakuu wa idara na vitengo kutoka Halmashauri yaMbeya Jiji pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya . Mada mbalimbali ziliwasilishwa ikiwa ni pamoja na Mada ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Tamko la Rasilimali na madeni, mada ya Ahadi ya Uadilifu,Mada ya Mgongano wa maslah Pamoja na mada ya uwajibikaji wa Pamoja.

Online Help
Kuanzisha Enzi Mpya katika Udhibiti wa Sekta ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania
Ofisi ya maadili inafanya kazi na imewashughulikia viongozi wengi sana kupitia Baraza la Maadili ambalo pia liliendeshwa mwaka 2013 Novemba mkoani Tabora. Viongozi mbalimbali waliokuwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili waliitwa kwenye Baraza na kuhojiwa na Baraza linatoa mapendekezo na kuyawasilisha mapendekezo hayo kwa Rais kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu na kisheria kwa viongozi husika.

" >
Kifungu cha 11(1) cha Sheria ya Maadili kimeainisha wazi mali zinazotakiwa kutajwa kuwa ni fedha taslimu, fedha zilizopo katika taasisi za kifedha kama vile benki, hisa, nyumba, mashamba, magari, mitambo na mali nyinginezo. Kiongozi anatakiwa kutoa tamko la mali anazomiliki yeye mwenyewe, mke/mume na watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane. Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni zinatakiwa kujazwa kila mwaka na kiongozi hutumiwa fomu hizo na Ofisi ya Maadili na pia zinapatikana katika mtandao wa maadili yaani www.ethicssecretariat.go.tz. Sheria inamtaka kiongozi kutolea tamko madeni yake ili kuweza kujua kuwa kiongozi anamiliki mali zipi na pia kutambua kuwa amezipata vipi mali hizo ukilinganisha na kipato cha kiongozi husika. Kiongozi kuwa na mali nyingi si dhambi kwani hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetamka wazi kuwa kila raia ana haki ya kumiliki mali ila ofisi inataka kujiridhisha uhalali wa jinsi mali ilivyopatikana. Mapendekezo katika Katiba mpya yanasisitiza maadili kwa kutenganisha uongozi na biashara.

" >
Wananchi wengi wamejijengea dhana kuwa bila pesa huwezi kupata huduma ya kiserikali kitu ambacho si kweli kwani huduma nyingi za kiserikali zinatolewa bure kabisa ila cha msingi wananchi wanatakiwa kutoa taarifa katika vyombo husika pindi wanapotakiwa kulipia huduma ambazo zinatolewa bure. Jamii inatakiwa kubadilika na kuamini kuwa si lazima kutoa rushwa ndipo upate huduma. Wapo wananchi wengi ambao walileta malalamiko kama hayo na Ofisi ya Maadili iliyashughulikia, hivyo wananchi wasisite kutembelea Ofisi zetu kwa ajili ya kutoa taarifa kama hizo.

" >
Kutoa lugha chafu ni ukiukwaji wa maadili. Ndani ya Bunge kuna Kamati ya Maadili ambayo ipo kwa ajili ya kuwawajibisha wabunge wanaotoa lugha chafu. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa upande wake ilifanya semina kwa wabunge ili kuwakumbusha mipaka ya utendaji kazi na maadili kwa ujumla, na tangu wakati huo matumizi ya lugha chafu bungeni yamepungua kwa kiasi kikubwa.

" >