JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS – SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

Viongozi wa Umma waaswa kuwa na Maadili
27 Oct, 2023
Viongozi wa Umma waaswa kuwa na Maadili

Viongozi wa Umma waaswa kuwa na maadili mema katika utendaji kazi wao wa kila siku. Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. Rebecca Sanga alipokua akifungua mafunzo ya Maadili kwa Viongozi wa Umma kutoka Taasisi, Idara na Mashirika ya Umma Mkoani Morogoro. Mafunzo hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Hazina ndogo mkoani Morogoro tarehe 07 Februari, 2023.

Akifungua mafunzo hayo Mhe.Sanga alisema kuwa maadili nyenzo muhimu sana kwa kila kiongozi kuwa nayo, maadili ni dhana pana inayojumuisha ; mwenendo mwema, mambo ya haki, usawa na mafundisho mema na ndio kiini cha kufanikiwa kwa maendeleo ya sekta mbalimbali za kijamii kama elimu , maji, umeme na nyingine nyingi.

Mhe. Sanga alieleza kuwa kila kiongozi yeyote wa Umma anapaswa kufanya kazi kwa kuzingatiamaadili kwani kiongozi ni kioo cha jamii yoyote ile hivyo kiongozi anapokua na maadili hawez kufanya mambo ambayo ni kinyume na taratibu, sheria na miongozo mbalimbali iliyowekwa nchini kama vile kutokutoa ama kupokea rushwa, ukiukwaji wa haki za binadamu, kujiingiza katika mgongano wa maslahi, pamoja na taratibu nyingine jambo ambalo litawafanya wananchi kuwa na imani na serikali yao “Maadili ni kinga dhidi ya maovu yote”alisema.

Mhe. Sanga alisema kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inasisitiza Viongozi kuwa na maadili mema , viongozi kuwa na tabia na mienendo isiyotia shaka, viongozi kutokua na dosari za kimaadili “Niwaase viongozi wenzangu kuwa wakati wote uadilifu uwe kipaumbele katika maisha ya kila siku tukiwa kazini ama nje ya mahala pa kazi” alisema.

Aidha Mhe. Sanga alitumia fursa hiyo kuwakumbusha Viongozi maelekezo mbalimbali ya serikali yanayohusu maadili ikiwa ni pamoja na: Kiongozi kutanguliza maslah ya umma mbele badala ya maslah binafsi, Kiongozikutanguliza uzalendo na maslah ya Umma mbele kwa ajili ya maendeleo ya Taifakatika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo, Kiongozi kuzingatia maadili,nidhamu katika kazi, kuwa mstari wa mbele katika vita dhidi ya rushwa , kuzingatiahaki za binadamu, kuwa na uwazi katika utendaji kazi na mengine mengi.

Pamoja na hayo Mhe. Sanga alieleza kuwa mafunzo hayo kwa viongozi wa umma yatasaidia kuwajenga kimaadili na kuwakumbusha umuhimu wa kuzingatia misingi ya maadili wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku na ni sehemu ya mikakati ya kuwajengea uwezo wadau mbalimbali ambao ni pamoja na Viongozi wa Umma ambao kimsingi ndio wanaohusika na utekelezaji wa shughuli za serikali lakini pia ni wasimamizi wa rasilimali za umma.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi Katibu Msaidizi Kanda ya Mashariki Bw. Henry Sawe alisema kuwa mafunzo hayo kwa viongozi wa umma ni hatua muhimu katika jitihada za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma katika kusimamia na kukuza maadili nchini.

Bw. Sawe alieleza kuwa jitihada hizozinakwenda sambamba na dhamira ya Serikali ya kuhakikisha kuwa tunakua na Taifa lililojengwa juu ya misingi na mifumo ya maadili. “sote tunafahamu kwamba Serikali yetu imekua wakati wote ikiweka uzito unaostahili katika suala la kusimamia na kukuza uadilifu nchini.

Katika mafunzo hayo ya siku moja mada mbalimbali ziliwasilishwa ikiwa ni pamoja na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya mwaka 1995 pamoja na kanuni zake, Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi na Watumishi wa Umma, Tamko la Rasilimali na Madeni, Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi na Watumishi wa Umma, pamoja na uwajibikaji katika utumishi wa Umma.

Online Help
Kuanzisha Enzi Mpya katika Udhibiti wa Sekta ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania
Ofisi ya maadili inafanya kazi na imewashughulikia viongozi wengi sana kupitia Baraza la Maadili ambalo pia liliendeshwa mwaka 2013 Novemba mkoani Tabora. Viongozi mbalimbali waliokuwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili waliitwa kwenye Baraza na kuhojiwa na Baraza linatoa mapendekezo na kuyawasilisha mapendekezo hayo kwa Rais kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu na kisheria kwa viongozi husika.

" >
Kifungu cha 11(1) cha Sheria ya Maadili kimeainisha wazi mali zinazotakiwa kutajwa kuwa ni fedha taslimu, fedha zilizopo katika taasisi za kifedha kama vile benki, hisa, nyumba, mashamba, magari, mitambo na mali nyinginezo. Kiongozi anatakiwa kutoa tamko la mali anazomiliki yeye mwenyewe, mke/mume na watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane. Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni zinatakiwa kujazwa kila mwaka na kiongozi hutumiwa fomu hizo na Ofisi ya Maadili na pia zinapatikana katika mtandao wa maadili yaani www.ethicssecretariat.go.tz. Sheria inamtaka kiongozi kutolea tamko madeni yake ili kuweza kujua kuwa kiongozi anamiliki mali zipi na pia kutambua kuwa amezipata vipi mali hizo ukilinganisha na kipato cha kiongozi husika. Kiongozi kuwa na mali nyingi si dhambi kwani hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetamka wazi kuwa kila raia ana haki ya kumiliki mali ila ofisi inataka kujiridhisha uhalali wa jinsi mali ilivyopatikana. Mapendekezo katika Katiba mpya yanasisitiza maadili kwa kutenganisha uongozi na biashara.

" >
Wananchi wengi wamejijengea dhana kuwa bila pesa huwezi kupata huduma ya kiserikali kitu ambacho si kweli kwani huduma nyingi za kiserikali zinatolewa bure kabisa ila cha msingi wananchi wanatakiwa kutoa taarifa katika vyombo husika pindi wanapotakiwa kulipia huduma ambazo zinatolewa bure. Jamii inatakiwa kubadilika na kuamini kuwa si lazima kutoa rushwa ndipo upate huduma. Wapo wananchi wengi ambao walileta malalamiko kama hayo na Ofisi ya Maadili iliyashughulikia, hivyo wananchi wasisite kutembelea Ofisi zetu kwa ajili ya kutoa taarifa kama hizo.

" >
Kutoa lugha chafu ni ukiukwaji wa maadili. Ndani ya Bunge kuna Kamati ya Maadili ambayo ipo kwa ajili ya kuwawajibisha wabunge wanaotoa lugha chafu. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa upande wake ilifanya semina kwa wabunge ili kuwakumbusha mipaka ya utendaji kazi na maadili kwa ujumla, na tangu wakati huo matumizi ya lugha chafu bungeni yamepungua kwa kiasi kikubwa.

" >