JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS – SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

VIONGOZI WA UMMA WAASWA KUWA MSTARI WA MBELE KWA KUFANYA KAZI KWA UADILIFU.
27 Oct, 2023
VIONGOZI WA UMMA WAASWA KUWA MSTARI WA MBELE KWA KUFANYA KAZI KWA UADILIFU.

Viongozi wa Umma wanategemewa kuwa mstari wa mbele katika kuzingatia na kutekeleza majukumu ya umma kwa uadilifu ikiwa ni pamoja na kusimamia na kuhakikisha kuwa rasilimali za nchi zinatumika kwa maslahi mapana ya nchi yetu.

Hayo yalisemwa na Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Sivangilwa Mwangesi wakati akifungua mafunzokuhusu ya Maadili yaliyotolewa kwa Viongozi mbalimbali wa Umma. Mafunzo hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Ofisi ndogo ya Bunge Jijini Dar es Salaam.

Akifungua mafunzo hayo Mhe. Mwangesi alisema kuwa jitihada za Serikali kupitia Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kutoa mafunzo hayo kwa Viongozi ni kielelezo dhahiri kuwa Serikali ya awamu ya Sita imedhamiria kuhakikisha kuwa suala la maadili ya uongozi linaeleweka kwa wadau wote wa sekta ya Umma na sekta binafsi.

Mhe. Mwangesi alisema kuwa Tanzania inahitaji Viongozi ambao ni mfano mzuri wa uzingatiajiwa maadili, Viongozi wanaozingatia Sheria, Kanuni na taratibu katika utendaji wao wa kazi, Viongozi wanaotumia nafasi zao za uongozi kwa kuwaletea wananchi maendeleo na si kwa maslahi yao binafsi jambo ambalo litawafanya wananchi kuwa na imani kwa viongozi wanaowaongoza na Serikali yao kwa ujumla. “Uongozi ni dhamanahivyo kiongozi yeyote anatakiwa atumie wadhifa wake kwa manufaa ya wananchi na si kwa manufaa yake binafsi’’alisema.

Aidha, Mhe. Mwangesi alieleza kuwa ukuzaji wa maadili kwa viongozi wa umma nchini ni moja ya jitihada za kuhakikisha kuwa malengo ya Dira ya Taifa yanafikiwa kama yalivyopangwa “kwa mujibu wa Dira ya Maendeleo ya Taifa katika kipengele cha Utawala Bora inatarajiwa kwamba ifikapo mwaka 2025 uadilifu unapaswa kuwa sehemu ya utamaduni wa jamii ya Tanzania na hilo linawezekana ikiwa kila mmoja atatimiza wajibu wake’’alisema.

Mhe.Mwangesi aliendelea kusema kuwa katika kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo, Serikaliimedhamiria kujenga utumishi wa umma ulio imara ambao utakuwa muhimili mkuu wa kujenga uchumi bora na kuondoa umaskini miongoni mwa wananchi “Nitoe rai kwenu Viongozi kuwa mafunzo haya yawe chachu ya kuongeza kasi ya kujenga na kukuza maadili kati yetu ili tuweze kutoa huduma bora kwa wananchi’’ alisema.

Pamoja na hayo Mhe. Mwangesi aliwakumbusha Viongozi wa Umma kuhusu misingi ya maadili ambayo ni pamoja na Kiongozi wa Umma kutoa matamko mbalimbali ikiwemo Tamko la Rasilimali, Maslah na Madeni, kutotumia vibaya rasilimali za umma, kutekeleza majukumu yao kwa uaminifu, uaminifu, uwazi, haki na kutopendelea pamoja na misingi minginemingi kama ilivyoainishwa kwenye Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma. “Kama kila kiongozi ataamua kufuata misingi hii basi rasilimali za nchi yetu zitakua salama na wanannchi watakua na imani kubwa kwa Serikali yao” alisema.

Mhe. Mwangesi alimaliza kwa kusema kuwa pamoja na jitihada zinazofanywa na Serikali ya kukuza maadili nchini ni muhimu jamii ikatambua kuwa vita dhidi ya ukiukwaji wa maadili siyo la Serikali pekee bali ni jukumu la jamii nzima, kuanzia mtu mmoja mmoja, katika ngazi ya familia, taasisi mbalimbali za kidini, sekta binafsi, asasi zisizo za kiraia pamoja na taasisi nyingine nyingi.

Katika mafunzo hayo ya siku moja mada mbalimbali zitawasilishwa ikiwa ni pamoja na mada kuhusu Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, mada kuhusu uwajibikaji wa pamoja, Kanuni za Mgongano wa Maslah, Kanuni za Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma na mada kuhusu Tamko la Rasilimali na Madeni. Mada hizozitawajengea Viongozi uwezo wa kuifahamu zaidi Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma na kanuni zake jambo litakalowasaidia kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwa uadilifu mkubwa.

Online Help
Kuanzisha Enzi Mpya katika Udhibiti wa Sekta ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania
Ofisi ya maadili inafanya kazi na imewashughulikia viongozi wengi sana kupitia Baraza la Maadili ambalo pia liliendeshwa mwaka 2013 Novemba mkoani Tabora. Viongozi mbalimbali waliokuwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili waliitwa kwenye Baraza na kuhojiwa na Baraza linatoa mapendekezo na kuyawasilisha mapendekezo hayo kwa Rais kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu na kisheria kwa viongozi husika.

" >
Kifungu cha 11(1) cha Sheria ya Maadili kimeainisha wazi mali zinazotakiwa kutajwa kuwa ni fedha taslimu, fedha zilizopo katika taasisi za kifedha kama vile benki, hisa, nyumba, mashamba, magari, mitambo na mali nyinginezo. Kiongozi anatakiwa kutoa tamko la mali anazomiliki yeye mwenyewe, mke/mume na watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane. Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni zinatakiwa kujazwa kila mwaka na kiongozi hutumiwa fomu hizo na Ofisi ya Maadili na pia zinapatikana katika mtandao wa maadili yaani www.ethicssecretariat.go.tz. Sheria inamtaka kiongozi kutolea tamko madeni yake ili kuweza kujua kuwa kiongozi anamiliki mali zipi na pia kutambua kuwa amezipata vipi mali hizo ukilinganisha na kipato cha kiongozi husika. Kiongozi kuwa na mali nyingi si dhambi kwani hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetamka wazi kuwa kila raia ana haki ya kumiliki mali ila ofisi inataka kujiridhisha uhalali wa jinsi mali ilivyopatikana. Mapendekezo katika Katiba mpya yanasisitiza maadili kwa kutenganisha uongozi na biashara.

" >
Wananchi wengi wamejijengea dhana kuwa bila pesa huwezi kupata huduma ya kiserikali kitu ambacho si kweli kwani huduma nyingi za kiserikali zinatolewa bure kabisa ila cha msingi wananchi wanatakiwa kutoa taarifa katika vyombo husika pindi wanapotakiwa kulipia huduma ambazo zinatolewa bure. Jamii inatakiwa kubadilika na kuamini kuwa si lazima kutoa rushwa ndipo upate huduma. Wapo wananchi wengi ambao walileta malalamiko kama hayo na Ofisi ya Maadili iliyashughulikia, hivyo wananchi wasisite kutembelea Ofisi zetu kwa ajili ya kutoa taarifa kama hizo.

" >
Kutoa lugha chafu ni ukiukwaji wa maadili. Ndani ya Bunge kuna Kamati ya Maadili ambayo ipo kwa ajili ya kuwawajibisha wabunge wanaotoa lugha chafu. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa upande wake ilifanya semina kwa wabunge ili kuwakumbusha mipaka ya utendaji kazi na maadili kwa ujumla, na tangu wakati huo matumizi ya lugha chafu bungeni yamepungua kwa kiasi kikubwa.

" >