VIONGOZI WA MKOA WA MTWARA WAMETAKIWA KUJIEPUSHA NA MGONGANO WA MASLAHI:

Viongozi wa Umma, mkoani Mtwara wametakiwa kujiepusha na mgongano wa maslahi wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku ili kujenga imani kwa Serikali na wananchi wanaowaongoza.
Kauli hiyo imetolewa na Kamishna wa Maadili Mhe, Jaji Sivangilwa Mwangesi katika kikao chake na viongoizi mkoani humo kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma mkoan iMtwara rehe22 juni, 2023.
Mhe Mwangesi katika hotuba yake amefafanua kuwa, kiongozi wa Umma akifanya kazi kwa Uadilifu, atatoa huduma bora na taratibu, kanuni na sheria na kwamba mianya ya mgongano wa Maslahi utapungua.
Mhe Mwangesi amebainisha kuwa, kiongozi akiwa mwadilifu, atakuwa jasir ikatika kutoa maamuzi ya haki, uwazi,na usawa katika utekelezaji wa majukumu yake.
Aidha Mhe Mwangesi, ameongeza kuwa, kiongozi akiwa mwadilifu atafata taratibu na sheria pia atasimamia misingi ya maadili ya viongozi kwa uwazi bila upendeleo na wananchi watakuwa na imani na viongozi wanaowaongoza.
Kuhusu suala la Zawadi, Mhe Mwangesia mewakumbusha viongozi kuwa, sheria inamtaka kiongozi kupokea zawad iisiyozidi shilingi laki mbili, iwapo zawadi hiyo itazidi kiasi hicho anatakiwa kuipeleka kwa afisa masuhuli kwa ajili ya kuitolea maamuzi.
Ziara hiyo ya Kamishna wa Maadili katika kanda ya kusini Mtwara,imefanyika ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma kitaifa iliyoanza rasmi tarehe 16 Juni na kuhitimishwa tarehe 23 Juni,2023