JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS – SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

Viongozi wa mkoa wa Dodoma wapigwa msasa kuhusu Sheria ya maadili ya Viongozi wa Umma.
27 Oct, 2023
Viongozi wa mkoa wa Dodoma wapigwa msasa kuhusu Sheria ya maadili ya Viongozi wa Umma.

Viongozi wa mkoa wa Dodoma wapigwa msasa kuhusu Sheria ya maadili ya Viongozi wa Umma.

Mhe. Rosemary Senyemule, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amesema kuwa kiongozi wa umma haonekani kuwa muadilifu endapo watumishi wengine anao wasimamia wanakiuka misingi ya maadili.

Mhe. Senyemule ameeleza hayo katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma Februari 8, 2023 wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa viongozi wa umma wapya wa mkoa huo.

“Haitoshi kiongozi wa umma pekee kuonekana katika jamii kuwa ni mwadilifu wakati watumishi wengine anao wasimamia wanalalamikiwa kutozingatia maadili. Kazi ya kiongozi wa umma ni kuhakikisha watumishi walio chini yako ni waadilifu na rasilimali zote za umma zinatunzwa vizuri wakiwemo watumishi,” amesema

Amesema, “mafunzo haya yatatusaidia kuwa waadilifu na kuondoa dhana kuwa maadili ya viongozi wa umma sio kujaza fomu za tamko tu, bali yanahusisha misingi mingine ikiwemo uadilifu, kuheshimu sheria, kujali watu wengine, uwazi, kujizuia na tamaa na kuepuka mgongano wa maslahi.”

Elimu tutakayoipata ni dhamira ya dhati ya Serikali kuwasaidia watumishi wake kutekeleza vizuri majukumu yao, ndio maana tumekuja kukumbushana sheria, kanuni na taratibu za kuzingatia tunapotimiza wajibu wetu kama viongozi, tukitoka hapa tuwe mfano bora na tutoe huduma bora kwa Watanzania.

Mhe, Mkuu wa mkoa katika hotuba yake amesisitiza kuwa, maadili ni kichocheo kikubwa cha maendeleo ya taifa kwa sababu hujenga umoja, amani, upendo, uvumilivu, utii na mshikamano katika Taifa.

“Ukiukwaji wa maadili kwa viongozi wa umma usipothibitiwa, unaathirii ustawi wa nchi na maendeleo ya jamii, wananchi wanakosa imani kwa viongozi wao na serikali yao, “amesema.

Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa mkoa, maaadili ya kiongozi wa umma yanaanza na kiongozi mwenyewe, muonekano na vitendo vyake katika jamii vinatakiwa kuonyesha kuwa ni muadilifu.

“Kiongozi wa umma hutenganishwi na cheo chako, huwezi kuacha cheo chako mahali popote unapokuwa unatembea nacho. Watu wakiona mwenendo wako, matendo yako yaonyeshe kuwa wewe ni nani na utambuliwe kwa vitendo vyako,” amesema na kuongeza kuwa tunapopata mafunzo hapa, kila mtu ajipe rejea katika utendaji wake wa kazi jamii inamuonaje?

Aiidha, Mkuu huyo wa Mkoa katika hotuba yake amefafanua kuwa, baada ya mafunzo hayo, mkoa wake utakuwa mfano na utatoa huduma bora kwa wananchi na hakutakuwepo tena malalamiko ya mara kwa mara kuhusu utoaji mbaya wa huduma.

Ameongeza kuwa maneno yaliyoko katika Ahadi ya Uadilifu yanayotamkwa pindi viongozi wa Umma wanapoteuliwa ni matamu sana kuyatamka na kila kiongozi alioko hapa ameyatamka, lakini tunayazingatia kiasi gani? Aliuliza.

Awali Bw. Waziri Kipacha, Katibu Idara ya Ukuzaji Maadili, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozii wa Umma alieleza kuwa jumla ya mada tano zitatolewa katika mafunzo hayo.

Amezitaja mada hizo kuwa ni; Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na 13 ya mwaka 1995, Kanuni za Mgongano wa Maslahi, Uwajibikaji wa pamoja, Kanuni za Ahadi ya Uadilifu na Tamkoo la Maslahi, rasilimali na madeni.

Mafunzo hayo yenye lengo la kuwajengea uwezo Viongozi wa Umma kuhusu Maadili ya Viongozi wa Umma yameandaliwa na Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Online Help
Kuanzisha Enzi Mpya katika Udhibiti wa Sekta ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania
Ofisi ya maadili inafanya kazi na imewashughulikia viongozi wengi sana kupitia Baraza la Maadili ambalo pia liliendeshwa mwaka 2013 Novemba mkoani Tabora. Viongozi mbalimbali waliokuwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili waliitwa kwenye Baraza na kuhojiwa na Baraza linatoa mapendekezo na kuyawasilisha mapendekezo hayo kwa Rais kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu na kisheria kwa viongozi husika.

" >
Kifungu cha 11(1) cha Sheria ya Maadili kimeainisha wazi mali zinazotakiwa kutajwa kuwa ni fedha taslimu, fedha zilizopo katika taasisi za kifedha kama vile benki, hisa, nyumba, mashamba, magari, mitambo na mali nyinginezo. Kiongozi anatakiwa kutoa tamko la mali anazomiliki yeye mwenyewe, mke/mume na watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane. Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni zinatakiwa kujazwa kila mwaka na kiongozi hutumiwa fomu hizo na Ofisi ya Maadili na pia zinapatikana katika mtandao wa maadili yaani www.ethicssecretariat.go.tz. Sheria inamtaka kiongozi kutolea tamko madeni yake ili kuweza kujua kuwa kiongozi anamiliki mali zipi na pia kutambua kuwa amezipata vipi mali hizo ukilinganisha na kipato cha kiongozi husika. Kiongozi kuwa na mali nyingi si dhambi kwani hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetamka wazi kuwa kila raia ana haki ya kumiliki mali ila ofisi inataka kujiridhisha uhalali wa jinsi mali ilivyopatikana. Mapendekezo katika Katiba mpya yanasisitiza maadili kwa kutenganisha uongozi na biashara.

" >
Wananchi wengi wamejijengea dhana kuwa bila pesa huwezi kupata huduma ya kiserikali kitu ambacho si kweli kwani huduma nyingi za kiserikali zinatolewa bure kabisa ila cha msingi wananchi wanatakiwa kutoa taarifa katika vyombo husika pindi wanapotakiwa kulipia huduma ambazo zinatolewa bure. Jamii inatakiwa kubadilika na kuamini kuwa si lazima kutoa rushwa ndipo upate huduma. Wapo wananchi wengi ambao walileta malalamiko kama hayo na Ofisi ya Maadili iliyashughulikia, hivyo wananchi wasisite kutembelea Ofisi zetu kwa ajili ya kutoa taarifa kama hizo.

" >
Kutoa lugha chafu ni ukiukwaji wa maadili. Ndani ya Bunge kuna Kamati ya Maadili ambayo ipo kwa ajili ya kuwawajibisha wabunge wanaotoa lugha chafu. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa upande wake ilifanya semina kwa wabunge ili kuwakumbusha mipaka ya utendaji kazi na maadili kwa ujumla, na tangu wakati huo matumizi ya lugha chafu bungeni yamepungua kwa kiasi kikubwa.

" >