JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS – SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

Viongozi wa Halmashauri ya Mpwawa waaswa kufanya kazi kwa kushirikiana
05 Sep, 2024
Viongozi wa Halmashauri ya Mpwawa waaswa kufanya kazi kwa  kushirikiana

Viongozi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ambao ni madiwani pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wameaswa kuzingatia dhana nzima ya uwajibikaji wa pamoja wakati wanatekeleza majukumu yao ya kila siku ili kuweza kuwaletea wananchi maendeleo kuipatia serikali mafanikio.

Wito huo umetolewa na Katibu Msaidizi Sekretarieti ya Maadili Kanda ya Kati – Dodoma Bi. Jasmin Awadh wakati akitoa mafunzo hayo kwa viongozi hao yaliyofanyika katika Halmashauri hiyo tarehe 05 Septemba, 2024

Aidha Bi. Jasmin alieleza kuwa suala la uwajibikaji wa pamoja kwa Viongozi lisipozingatiwa litasababisha ucheleweshwaji wa huduma za kijamii kwa wananchi kama vile hospitali, shule,  barabara n.k na wananchi watapoteza imani yao kwa serikali.

”Kunapokua na mkinzano baina ya viongozi juu ya namna ya utekelezaji wa huduma mbalimbali  za kijamii huyu anasema tufanye vile yule anasema tufanye  vile lazima huduma hizo zikwame ama kutokufanyika kabisa”

Bi.Jasmin aliwahimiza viongozi hao kushirikiana katika kupanga vipaumbele vya Taasisi ili kuhakikisha kwamba malengo yaliyopangwa na halmashauri yanatekelezwa ipasavyo ikiwemo kuwafikishia wananchi huduma wanazohitaji.

“Nyinyi kama Viongozi mnapaswa kuwashirikisha watumishi walio chini yenu juu ya mikakati mliyonayo ili muweze kushirikiana kuitekeleza mnapaswa nyote muwe na uelekeo mmoja kila mtumishi aelewe jukumu lake katika kufanikisha malengo ya Taasisi”

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa Mhe. George Rume alisema kuwa mafunzo hayo kwa viongozi hao ni muhimu sana kwani yatawasaidia kuleta mabadiliko katika halmashauri yao kwani suala la maadili ni la muhimu sana hasa ushirikiano na uwajibikaji katika kutekeleza majukumu yetu.

Kwa mujibu wa Mhe Rume alieleza kuwa kiongozi yeyote ni lazima ajue dira ya Taasisi yake kwamba nini anatakiwa kufanya  ili aweze kuwaongoza walio chini yake kuitekeleza na kuleta maendeleo kwa wananchi na serikali kwa ujumla.

”Tukianza kukinzana viongozi kwa viongozi hatufiki popote na tutazorotesha juhudi za serikali za kuwaletea wananchi maendeleo’’ alisema.

Mafunzo hayo ni mkakati na kipaumbele cha Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuhakikisha kwamba Viongozi wote wanashirikiana katika Taasisi zao wanafanya kazi kwa pamoja kwa kuzingatia viwango vya juu vya maadili na kuleta matunda kwa wananchi

 

Online Help
Kuanzisha Enzi Mpya katika Udhibiti wa Sekta ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania
Ofisi ya maadili inafanya kazi na imewashughulikia viongozi wengi sana kupitia Baraza la Maadili ambalo pia liliendeshwa mwaka 2013 Novemba mkoani Tabora. Viongozi mbalimbali waliokuwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili waliitwa kwenye Baraza na kuhojiwa na Baraza linatoa mapendekezo na kuyawasilisha mapendekezo hayo kwa Rais kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu na kisheria kwa viongozi husika.

" >
Kifungu cha 11(1) cha Sheria ya Maadili kimeainisha wazi mali zinazotakiwa kutajwa kuwa ni fedha taslimu, fedha zilizopo katika taasisi za kifedha kama vile benki, hisa, nyumba, mashamba, magari, mitambo na mali nyinginezo. Kiongozi anatakiwa kutoa tamko la mali anazomiliki yeye mwenyewe, mke/mume na watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane. Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni zinatakiwa kujazwa kila mwaka na kiongozi hutumiwa fomu hizo na Ofisi ya Maadili na pia zinapatikana katika mtandao wa maadili yaani www.ethicssecretariat.go.tz. Sheria inamtaka kiongozi kutolea tamko madeni yake ili kuweza kujua kuwa kiongozi anamiliki mali zipi na pia kutambua kuwa amezipata vipi mali hizo ukilinganisha na kipato cha kiongozi husika. Kiongozi kuwa na mali nyingi si dhambi kwani hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetamka wazi kuwa kila raia ana haki ya kumiliki mali ila ofisi inataka kujiridhisha uhalali wa jinsi mali ilivyopatikana. Mapendekezo katika Katiba mpya yanasisitiza maadili kwa kutenganisha uongozi na biashara.

" >
Wananchi wengi wamejijengea dhana kuwa bila pesa huwezi kupata huduma ya kiserikali kitu ambacho si kweli kwani huduma nyingi za kiserikali zinatolewa bure kabisa ila cha msingi wananchi wanatakiwa kutoa taarifa katika vyombo husika pindi wanapotakiwa kulipia huduma ambazo zinatolewa bure. Jamii inatakiwa kubadilika na kuamini kuwa si lazima kutoa rushwa ndipo upate huduma. Wapo wananchi wengi ambao walileta malalamiko kama hayo na Ofisi ya Maadili iliyashughulikia, hivyo wananchi wasisite kutembelea Ofisi zetu kwa ajili ya kutoa taarifa kama hizo.

" >
Kutoa lugha chafu ni ukiukwaji wa maadili. Ndani ya Bunge kuna Kamati ya Maadili ambayo ipo kwa ajili ya kuwawajibisha wabunge wanaotoa lugha chafu. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa upande wake ilifanya semina kwa wabunge ili kuwakumbusha mipaka ya utendaji kazi na maadili kwa ujumla, na tangu wakati huo matumizi ya lugha chafu bungeni yamepungua kwa kiasi kikubwa.

" >