JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS – SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

Viongozi wa Halmashauri ya Chemba wajengewa uwezo kuhusu uwajibikaji wa pamoja.
27 Oct, 2023
Viongozi wa Halmashauri ya Chemba wajengewa uwezo kuhusu uwajibikaji wa pamoja.

Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imewapatia mafunzo ya kuwajengea uwezo kuhusu uwajibikaji wa pamojaviongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma. Mafunzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba tarehe 16 Februari, 2023.

Akifungua mafunzo hayo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Bw. Sambala Said alisema kuwamafunzo hayo ni muhimu sana kwa viongozi kwani yatasaidia kuwatengenezea ramani na kuwapa uelekeo ni namna gani wanapaswa kutekeleza majukumu yao.

Bw. Sambala alisema kuwa, “ni vizuri viongozi kupatiwa mafunzo kama haya ili kuleta uwajibikaji wa pamoja katika utekelezaji wa majukumu yetu,jambo litakalosaidia kutengeneza timu moja itakayoleta matokeo chanya ambayo ndiyo lengo hasa la serikali yetu” alisema.

Kwa mujibu wa Bw. Sambala kiongozi yeyote anapaswa kuwa mstari wa mbele kufuata taratibu na miongozo mbalimbali iliyowekwa na Serikali kwasababu kiongozi ni kioo cha jamii inayomzunguka.

“Ni wajibu wa kiongozi kuishi maisha ya kuigwa katika jamii husika, jambo hili litasababisha wananchi kuwa na imani na viongozi wao,” alisema.

Aidha, Bw. Sambala alitumia fursa hiyo kuwaasa Viongozi wa Umma kutotumia nafasi walizo nazo kukiuka misingi yamaadili kama vile kupokea ama kutoa rushwa, kujiingiza katika mgongano wa Maslah, kufanya kazi kwa ukweli na uwazi pamoja na misingi mingine ambayo ikikiukwa inaitia dosari serikali na kuleta sintofahamu kwa wananchi.

Kwa upande wake Katibu Msaidizi Kanda ya Kati, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bi. Jasmin Awadhi alisema kuwa Serikali kupitia Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambacho ndicho chombo kilichopewa mamlaka ya kusimamia maadili ya Viongozi wa Umma ina jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa Viongozi katika ngazi zote wanafanya kazi kwa umoja na kwa kushirikiana ili kuweza kufikia malengo yaliyowekwa na serikali ikiwa ni pamoja na kuwapatia wananchi maendeleo.

Bi. Jasmin alieleza kuwa lengo la mafunzo hayo ni kujenga umoja kwa viongozi na hii ni baada ya kuonekana mvutano katika Halmashauri mbalimbali nchini baina ya madiwani na wataalamu kutoelewana katika utendaji kazi wao na kuleta migogoro jambo linalosababisha kucheleweshwa kwa shughuli mbalimbali za serikali katika Halmashauri hizo.

Aidha Bi. Jasmin alisema kuwa, “mafunzo hayo pia yanalenga kuwakumbusha viongozi wajibu wao katika utendaji kazi, misingi ya maadili, wito wa viongozi hao katika kazi jambo litakalosaidia viongozi kuwajibika kwa pamoja na kuleta maendeleo katika jamii kama vile ujenzi wa shule, hospitali, barabara na nyingine nyingi.”

Akiwasilisha mada kuhusu Mgongano wa Maslahi Bi. Modester Mtui, Afisa kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma alisema kuwa suala la mgongano wa maslahi kwa sasa limekua ni tatizo kubwa katika jamii kwani Viongozi wengi wamejikuta wakijiingiza katika mgongano wa maslahi ama kwa kujua au bila kujua.

“Kumekuwa na tabia ya Viongozi ama watumishi wa Umma kufanya kazi zao binafsi ama za nje wakati wa muda wa kazi, kupokea zawadi kinyume na sheria, kupendelea na nyingine nyingi ambazo kwa kujua ama kutokujua anakua amejiingiza katika mgongano wa maslah ” alisema

Mada mbalimbali ziliwasilishwa katika mafunzo hayo ikiwa ni pamoja na Mgongano wa Maslah, Uwajibikaji wa pamoja pamoja na Tamko la Rasilimali na Madeni.

Online Help
Kuanzisha Enzi Mpya katika Udhibiti wa Sekta ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania
Ofisi ya maadili inafanya kazi na imewashughulikia viongozi wengi sana kupitia Baraza la Maadili ambalo pia liliendeshwa mwaka 2013 Novemba mkoani Tabora. Viongozi mbalimbali waliokuwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili waliitwa kwenye Baraza na kuhojiwa na Baraza linatoa mapendekezo na kuyawasilisha mapendekezo hayo kwa Rais kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu na kisheria kwa viongozi husika.

" >
Kifungu cha 11(1) cha Sheria ya Maadili kimeainisha wazi mali zinazotakiwa kutajwa kuwa ni fedha taslimu, fedha zilizopo katika taasisi za kifedha kama vile benki, hisa, nyumba, mashamba, magari, mitambo na mali nyinginezo. Kiongozi anatakiwa kutoa tamko la mali anazomiliki yeye mwenyewe, mke/mume na watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane. Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni zinatakiwa kujazwa kila mwaka na kiongozi hutumiwa fomu hizo na Ofisi ya Maadili na pia zinapatikana katika mtandao wa maadili yaani www.ethicssecretariat.go.tz. Sheria inamtaka kiongozi kutolea tamko madeni yake ili kuweza kujua kuwa kiongozi anamiliki mali zipi na pia kutambua kuwa amezipata vipi mali hizo ukilinganisha na kipato cha kiongozi husika. Kiongozi kuwa na mali nyingi si dhambi kwani hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetamka wazi kuwa kila raia ana haki ya kumiliki mali ila ofisi inataka kujiridhisha uhalali wa jinsi mali ilivyopatikana. Mapendekezo katika Katiba mpya yanasisitiza maadili kwa kutenganisha uongozi na biashara.

" >
Wananchi wengi wamejijengea dhana kuwa bila pesa huwezi kupata huduma ya kiserikali kitu ambacho si kweli kwani huduma nyingi za kiserikali zinatolewa bure kabisa ila cha msingi wananchi wanatakiwa kutoa taarifa katika vyombo husika pindi wanapotakiwa kulipia huduma ambazo zinatolewa bure. Jamii inatakiwa kubadilika na kuamini kuwa si lazima kutoa rushwa ndipo upate huduma. Wapo wananchi wengi ambao walileta malalamiko kama hayo na Ofisi ya Maadili iliyashughulikia, hivyo wananchi wasisite kutembelea Ofisi zetu kwa ajili ya kutoa taarifa kama hizo.

" >
Kutoa lugha chafu ni ukiukwaji wa maadili. Ndani ya Bunge kuna Kamati ya Maadili ambayo ipo kwa ajili ya kuwawajibisha wabunge wanaotoa lugha chafu. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa upande wake ilifanya semina kwa wabunge ili kuwakumbusha mipaka ya utendaji kazi na maadili kwa ujumla, na tangu wakati huo matumizi ya lugha chafu bungeni yamepungua kwa kiasi kikubwa.

" >