JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS – SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

PO-ETHICS SECRETARIAT Logo
Viongozi Chemba wakumbushwa uwajibikaji wa pamoja katika kutekeleza majukumu yao
14 Feb, 2026
Viongozi Chemba wakumbushwa uwajibikaji wa pamoja katika kutekeleza majukumu yao

Viongozi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chemba iliyopo mkoani Dodoma wamekumbushwa kufanya kazi kwa pamoja huku wakisisitizwa kuzingatia viwango vya  juu vya uadilifu na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

Kauli hiyo imesemwa tarehe 14 Februari, 2026 na Katibu Msaidizi, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kati-Dodoma Bi. Jasmin Awadhi wakati akitoa mafunzo kuhusu Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa Viongozi wa Halmashauri hiyo.

“Kufanya kazi kwa mazoea kumechangia Taasisi nyingi kutofikia malengo yao, na hii ni kutokana na watu wachache kushikilia majukumu mengi kwa wakati mmoja na kuwanyima fursa wengine kuonyesha uwezo wao,’’ alisema Bi. Jasmin.

Aidha Bi. Jasmin ametumia mafunzo hayo kuwakumbusha Viongozi hao kufanya kazi kwa huruma, maelewano na kutumia njia sahihi za mawasiliano ili kuondoa sintofahamu katika utendaji wao na hatimaye kuleta maendeleo katika maeneo yao na Taifa kwa ujumla.

“Mawasiliano ni nyenzo muhimu katika utekelezaji wa majukumu yetu ya kila siku, hivyo kama njia hii haitatumika vyema hatuwezi kupiga hatua katika kutatua changamoto za wananchi maana kila mmoja atakua anafanya lake, hivyo msingi mzuri wa mawasiliano ni tija katika uwajibikaji hasa kwa kufata chaneli nzuri katika kuwasiliana huko.’’ Alisema.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Ovada ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw. Raphael Lebba amesema kuwa wao kama Viongozi wamepokea kwa mikono miwili mafunzo hayo maana miongoni mwao kuna Madiwani wengi wapya ambao walikua na upungufu katika kufahamu dhana nzima ya maadili.

 “Mimi hii ni awamu ya pili kupata mafunzo haya, lakini Madiwani wengine ni wapya hivyo kwangu ni fursa kujikumbusha tena maana Kiongozi lazima uwe na maadili ili kuwatendea haki watu unaowaongoza,’’ alisema Mhe. Lebba.

Katika mafunzo mada mbali mbali ziliwasilishwa na wawezeshaji kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambapo Madiwani, Wakuu wa Vitengo na Idara wa Halmashauri hiyo walipata nafasi ya kushiriki katika mafunzo hayo.

 

Online Help
Kuanzisha Enzi Mpya katika Udhibiti wa Sekta ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania
Ofisi ya maadili inafanya kazi na imewashughulikia viongozi wengi sana kupitia Baraza la Maadili ambalo pia liliendeshwa mwaka 2013 Novemba mkoani Tabora. Viongozi mbalimbali waliokuwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili waliitwa kwenye Baraza na kuhojiwa na Baraza linatoa mapendekezo na kuyawasilisha mapendekezo hayo kwa Rais kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu na kisheria kwa viongozi husika.

" >
Kifungu cha 11(1) cha Sheria ya Maadili kimeainisha wazi mali zinazotakiwa kutajwa kuwa ni fedha taslimu, fedha zilizopo katika taasisi za kifedha kama vile benki, hisa, nyumba, mashamba, magari, mitambo na mali nyinginezo. Kiongozi anatakiwa kutoa tamko la mali anazomiliki yeye mwenyewe, mke/mume na watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane. Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni zinatakiwa kujazwa kila mwaka na kiongozi hutumiwa fomu hizo na Ofisi ya Maadili na pia zinapatikana katika mtandao wa maadili yaani www.ethicssecretariat.go.tz. Sheria inamtaka kiongozi kutolea tamko madeni yake ili kuweza kujua kuwa kiongozi anamiliki mali zipi na pia kutambua kuwa amezipata vipi mali hizo ukilinganisha na kipato cha kiongozi husika. Kiongozi kuwa na mali nyingi si dhambi kwani hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetamka wazi kuwa kila raia ana haki ya kumiliki mali ila ofisi inataka kujiridhisha uhalali wa jinsi mali ilivyopatikana. Mapendekezo katika Katiba mpya yanasisitiza maadili kwa kutenganisha uongozi na biashara.

" >
Wananchi wengi wamejijengea dhana kuwa bila pesa huwezi kupata huduma ya kiserikali kitu ambacho si kweli kwani huduma nyingi za kiserikali zinatolewa bure kabisa ila cha msingi wananchi wanatakiwa kutoa taarifa katika vyombo husika pindi wanapotakiwa kulipia huduma ambazo zinatolewa bure. Jamii inatakiwa kubadilika na kuamini kuwa si lazima kutoa rushwa ndipo upate huduma. Wapo wananchi wengi ambao walileta malalamiko kama hayo na Ofisi ya Maadili iliyashughulikia, hivyo wananchi wasisite kutembelea Ofisi zetu kwa ajili ya kutoa taarifa kama hizo.

" >
Kutoa lugha chafu ni ukiukwaji wa maadili. Ndani ya Bunge kuna Kamati ya Maadili ambayo ipo kwa ajili ya kuwawajibisha wabunge wanaotoa lugha chafu. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa upande wake ilifanya semina kwa wabunge ili kuwakumbusha mipaka ya utendaji kazi na maadili kwa ujumla, na tangu wakati huo matumizi ya lugha chafu bungeni yamepungua kwa kiasi kikubwa.

" >