SHILINGI MILIONI 335 ZAMFIKISHA MKURUGENZI MKUU WA PSSSF MBELE YA BARAZA LA MAADILI

SHILINGI MILIONI 335 ZAMFIKISHA MKURUGENZI MKUU WA PSSSF MBELE YA BARAZA LA MAADILI
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Bwana Hoseah Kashimba, amefikishwa kwenye Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma hivikaribunikwa tuhuma za ukiukwaji wa Sheria ya Maadili ikiwemo matumizi mabaya ya shilingi 335,314,803.84 fedha za mfuko.
Wakili wa Serikali Bwana Hassan Mayunga aliliambia Baraza la maadili ya Viongozi wa Ummakuwa Bwana Kashimba alitenda kosa hilo wakati akitekeleza majukumu yake ya Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF kati ya mwaka 2020 na 2021.
Alisema, “Bila kufuata taratibu mlalamikiwa alitumia fedha za Mfuko wa Hifadhi ya jamii kwa Watumishi wa Umma kiasi cha shilingi 211,671,962.00 kwa kuzikopa na kununua gari binafsi akijua kuwa fedha hizo hazikutengwa katika bajeti ya mwaka 2020/2021.”
Katika shtaka la pili, Bwana Kashimba anatuhumiwa kutumia fedha za umma katika mfuko wa PSSSF kiasi cha shilingi 123,642,841.84 kwa ajili ya kulipia kodi kama sehemu ya fedha zake za malipo ya ununuzi wa gari binafsi, kinyume na kifungu cha 6(1)(a),(b)(i) na (f) cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya mwaka 1995.
Aidha Bwana Kashimba anatuhumiwa kupokea moja kwa moja fedha kutok a PSSSF kiasi cha shilingi 123,642,841.84 kwa ajili ya kulipia kodi ya ununuzi wa gari badala kodi hiyokulipwa moja kwa mojaMamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Baraza lilielezwa kuwa kitendo hicho ni kinyume na Kifungu cha 6(1)(a), (b)(i) cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma kikisomwa pamoja na Kanuni ya 3(2)(a)ya Kanuni za Udhibiti wa Mgongano wa Maslahi na kanuni ya 7(d) na (e) ya Kanuni za Ahadi ya Uadilifu.
“Mlalamikiwa alipokea kiasi cha shilingi 45,000,000.00 kutoka kwenye mfuko wa PSSSF ikiwa ni malipo ya samani bila kuilipia kodikinyume na kifungu cha 6(1)(a) na (c) cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma,” alisema.
Mlalamikiwa alikana mashtaka yote matatu.
Katikautetezi wake Bw. Kashimba alilieleza baraza kuwafedha zote alizokopa kwa ajili ya ununuzi wa gari binafsi pamoja na kodi ni stahili yakekama Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF na hakuna taratibu au kanuni yoyote iliyokiukwa.
Vikao vya Baraza la maadili ya viongozi wa Umma ni utekelezaji wa matakwa ya Ibara ya 132 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kuhusu kusimamia tabia na mwenendo wa viongozi wa umma waliotajwa katika Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.