Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma kurekebishwa.

Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imeanza mchakato wa kufanya marekebisho ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Namba 13 ya mwaka 1995 kwa lengo la kuboresha kifungu cha 4 chenye orodha ya Viongozi wanaowajibika na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa umma.
Akifungua kikao kazi cha kujadili mchakato wa kurekebisha sheria hiyo kwa niaba ya Kamishna wa Maadili Katibu Msaidizi Idara ya Ukuzaji Maadili Sekretarieti ya Maadili Bw. Fabian Pokela alisema kuwa kikao kazi hicho kina jukumu kubwa la kufanya marekebisho ya Sheria hiyo hususan kifungu cha 4 ambacho kina orodha ya Viongozi wanaohusika na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Bw. Pokela aliongeza kuwa dhumuni kubwa la kubadili sheria hiyo hususan kifungu cha 4 chenye orodha ya Viongozi wanaohusika na sheria ya Maadili ni baada ya kubaini kuwa wapo watumishi kutoka Taasisi mbalimbali za Umma na binafsi ambao ni Viongozi lakini hawajatajwa na Sheria hiyo jambo linalowafanya kutohusika kabisa na sheria hiyo
Aidha Bw, Pokela aliendelea kusema kuwa zipo pia nafasi ama nyadhifa mbalimbali ambazo zinaonekana wazi kuwa hatarishi kwa kukiuka maadili hivyo imeonekana kuwa watatakiwa kumulikwa vizurizaidi na Sheria ya Maadili ili waweze kusimamiwa katika utendaji kazi wao .
“Ni lazima nafasi hizi ziangaliwe kwa makini kwanizipo nyadhifa ambazo inaonekana wazi kabisa kwamba kiongozi husika katika utendaji wake wa kazi kwa namna moja ama nyingine anaweza kukiuka moja ya kanuni ama misingi ya Maadili ya Viongozi wa Umma hivyo ni lazima waongezwe kwenye Sheria ya Maadili ili waweze kumulikwa vizuri” alisema.
Bw. Pokela alieleza kuwamwenye mamlaka ya kubadili sheria yoyote ni Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania hivyo kikao kazi hicho ni cha muhimu kwani kinafanya kazi kwa niaba ya Rais hivyo ni lazima yapatikane mapendekezo yenye tija yatakayosaidia kupatikana kwa orodha kamili ya Viongozi watakaohusika na sheria hiyo ili kuboresha uwajibikaji wa Viongozi kwa pamoja.
Awali akimkaribisha Katibu, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria Bi. Emma Gelani alisema kuwa Lengo la kufanya maboresho ya Sheria ya Maadili ni kuongeza idadi ya viongozi wanaohusika na Sheria hiyo ili kuongeza wigo wa uwajibikaji wa viongozi katika sheria hiyo.
Aidha Bi. Emma alieleza kuwa washiriki wa kikao kazi hicho ni kutoka, Ofisi ya Rais Ikulu, Ofisi ya Rais Menejimenti yaUtumishi wa Umma na Utawala Bora, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Ofisi yaMsajili wa hazina.
Toka kuanzishwa kwa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma mnamo mwaka 1995, Sheria hiyo imepitia vipindi kadhaavya maboresho ambapo mwaka 2001 yalifanyika maboreshovivyo hivyo mwaka 2005 na maboresho ya mwishoyalifanyika mwaka 2013.
Kikao kazi hicho kilifanyika katika ukumbi wa Edema mkoani Morogoro kuanzia tarehe 31 Januari, 2023 hadi tarehe 03 Februari,2023.