Sekretarieti ya Maadili yajipanga kutekeleza Ilani ya CCM katika eneo la Maadili.

Sekretarieti ya Maadili yajipanga kutekeleza Ilani ya CCM katika eneo la Maadili.
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imejipanga kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi katika eneo la Maadili ya Viongozi wa Umma baada yakushinda uchaguzi wa 2020 nakuunda Serikali.
Hayo yalisemwa na Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Sivangilwa Mwangesi alipokuwa akifungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Sekretarieti ya Maadili lililofanyika 2 Machi, 2021Mjini Morogoro.
Mhe. Jaji Mwangesi alisema kuwa Katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 katika aya ya 112 ya Ilani ya Uchaguzi chama kiliahidi kuendelea kuhakikisha suala la Maadili yaViongozi wa Umma linatiliwa mkazo na kuimarishwa zaidi ili wananchi waendelee kunufaika na huduma kulingana namatarajio yao.
Kwa mujibu wa Mhe. Jaji Mwangesi ili kufikia malengo hayo Chama kiliahidi kuielekeza Serikali (Sekretarieti ya Maadili) kutekeleza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na:Kusimamia nidhamu ,uadilifu, uwazi,uzalendo wa kitaifa,moyo wa kujitolea na uwajibikaji miongoni mwa Viongozi na Watumishi wa Umma;
Mhe Jaji Mwangesi aliendelea kuyataja mambo mengine yaliyoahidiwa na Ilani nikuongeza watumishi wenye sifa stahiki kwenye utoaji huduma nakuhimiza watumishiwa umma kufanyakazi kwa juhudi, maarifa, ubunifu naweledi katika kujenga Taifa letu; Kudhibiti Migongano wa Maslahi katika shughuli za umma kwakusimamia mifumo iliyopo na Kujenga jamiii nayoheshimu na kuthamini utu, haki, maadili na nidhamu.
Kuhusu uelekeo wa taasisi katika kutekeleza majukumu yake Mhe. Jaji Mwangesi alisema kuwa Taasisi yoyote ile ni Lazima iwe na mwelekeo au malengo ya muda mrefu na mfupi katika kufikia malengo yake.
Hivyo basi Mhe. Jaji Mwangesi aliwaeleza Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Sekretarieti ya Maadili kuwa kwakuzingatia majukumu yake ya kikatiba na kisheria itaendelea kujikita katika Dira yake ya kuwa Taasisi yenye ufanisi na kuaminika katika kukuza na kusimamia Misingi ya Maadili ya Viongozi wa Umma nchini.
Wakati huo huo Mhe.Jaji Mwangesi alitumia fursa hiyo kuwaasa Watumishi wa Sekretarieti ya Maadili kuwa na Ushirikiano ili kuwa na Utendaji wenye tija katika Taasisi
“Kila mmoja ni lazima aione Idara/Kitengo au Ofisi ya Kanda ina umuhimu sawa na nyingine; Mguu unapochafuka mkono usisite kuusafisha sote tunajenga nyumba moja hakuna haja ya kugombea fito” alisisitiza Mhe.JajiMwangesi.
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma iliunda Baraza la Wafanyakazi tarehe 14 Januari, 2005 ikiwa ni utekelezaji wa Waraka wa Rais Namba moja wa mwaka 1970,Waraka ambao Baba wa Taifa Hayati Mwl.Julius Nyerere aliagiza kilaTaasisi ya Umma iwena Baraza la Wafanyakazi mahali pa kazi ili kuimarisha zaidi matumizi ya Dhana ya Utatu baina ya Serikali, Mwajiri na Wafanyakazi.