JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS – SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

PO-ETHICS SECRETARIAT Logo
Sekretarieti ya Maaadili wapigwa msasa namna ya kukuza Maadili kwa njia ya vyombo vya Habari
05 May, 2026
Sekretarieti ya Maaadili wapigwa msasa namna ya kukuza Maadili kwa njia ya vyombo vya Habari

Viongozi na Maafisa Maadili kutoka Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma wamepatiwa mafunzo ya namna ya kutumia vyombo vya habari katika kukuza maadili kwa Viongozi wa Umma na wananchi kwa ujumla.

Mafunzo hayo maalamu yenye lengo la kuwajengea uwezo maafisa hao katika kuandaa na kuwasilisha mada kwa hadhira kwa kutumia njia za kisasa yanafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Flomi mjini Morogoro kuanzia tarehe 4 hadi 8 Mei, 2026.

Akifungua mafunzo hayo, Kamishna wa Maadili nchini, Jaji (Stahiki) Sivangilwa Mwangesi amewataka wakufunzi wa mafunzo hayo kuwapitisha washiriki katika mada ambazo zitawasaidia katika kutoa elimu ya maadili kwa umma.

"Mafunzo haya yanakwenda moja kwa moja kwenye kiini cha jukumu letu kuhakikisha ujumbe wa maadili unawafikia walengwa kwa lugha inayofaa kwa hoja zinazojengwa kwa kupitia Sheria, taratibu na kanuni na pia kwa kutumia mbinu zinazoendana na mazingira ya sasa ya mawasiliano" alisema Mhe. Mwangesi.

Jaji Mwangesi ameeleza kuwa baada ya washiriki kupata mafunzo hayo ni matumaini yake kuwa yatawasaidia katika kuboresha maeneo muhimu kama vile kujenga uwezo wa kutambua hadhira, kuandaa maudhui ya maadili yenye mifano halisi, kushiriki kwa kujiamni kwenye vipindi mbalimbali kupitia vyombo vya habari kama, redio, televisheni pamoja na hadhara mbalimbali.

Aidha, Jaji Mwangesi amesisitiza kuwa mafunzo hayo yanatasaidia kuwasiliana kwa ustaha na weledi pamoja na kutumia vizuri mitandao ya kijamii kwa munufaa ya Taasisi katika kutoa elimu, kwani elimu ya maadili sio kusoma vifungu vya sheria tu bali ni uwezo wa kutafsiri Sheria na Sera katika ujumbe unaoeleweka katika mazingira halisi.

Wabobezi wa Tasnia ya habari ambao ni Dkt. Dotto Bulendu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustne(SAUT)-Mwanza na Dkt. Egbert Mkoko kutoka Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam (UDSM) idara ya Uandishi wa habari na Utangazaji (SJMC).

Baadhi ya mada zinazowasilishwa katika mafunzo hayo ni njia bora ya uwasilishaji wa mada mbalimbali kupitia hadhira tofauti, namna ya kutoa elimu kwa umma na jinsi ya kufanya hamasa pamoja na jinsi ya kujiandaa pindi muhusika anapotaka kwenda kutoa elimu ya maadili kupitia Redio, Televisheni na mitandao ya kijamii.

 

 

Online Help
Kuanzisha Enzi Mpya katika Udhibiti wa Sekta ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania
Ofisi ya maadili inafanya kazi na imewashughulikia viongozi wengi sana kupitia Baraza la Maadili ambalo pia liliendeshwa mwaka 2013 Novemba mkoani Tabora. Viongozi mbalimbali waliokuwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili waliitwa kwenye Baraza na kuhojiwa na Baraza linatoa mapendekezo na kuyawasilisha mapendekezo hayo kwa Rais kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu na kisheria kwa viongozi husika.

" >
Kifungu cha 11(1) cha Sheria ya Maadili kimeainisha wazi mali zinazotakiwa kutajwa kuwa ni fedha taslimu, fedha zilizopo katika taasisi za kifedha kama vile benki, hisa, nyumba, mashamba, magari, mitambo na mali nyinginezo. Kiongozi anatakiwa kutoa tamko la mali anazomiliki yeye mwenyewe, mke/mume na watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane. Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni zinatakiwa kujazwa kila mwaka na kiongozi hutumiwa fomu hizo na Ofisi ya Maadili na pia zinapatikana katika mtandao wa maadili yaani www.ethicssecretariat.go.tz. Sheria inamtaka kiongozi kutolea tamko madeni yake ili kuweza kujua kuwa kiongozi anamiliki mali zipi na pia kutambua kuwa amezipata vipi mali hizo ukilinganisha na kipato cha kiongozi husika. Kiongozi kuwa na mali nyingi si dhambi kwani hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetamka wazi kuwa kila raia ana haki ya kumiliki mali ila ofisi inataka kujiridhisha uhalali wa jinsi mali ilivyopatikana. Mapendekezo katika Katiba mpya yanasisitiza maadili kwa kutenganisha uongozi na biashara.

" >
Wananchi wengi wamejijengea dhana kuwa bila pesa huwezi kupata huduma ya kiserikali kitu ambacho si kweli kwani huduma nyingi za kiserikali zinatolewa bure kabisa ila cha msingi wananchi wanatakiwa kutoa taarifa katika vyombo husika pindi wanapotakiwa kulipia huduma ambazo zinatolewa bure. Jamii inatakiwa kubadilika na kuamini kuwa si lazima kutoa rushwa ndipo upate huduma. Wapo wananchi wengi ambao walileta malalamiko kama hayo na Ofisi ya Maadili iliyashughulikia, hivyo wananchi wasisite kutembelea Ofisi zetu kwa ajili ya kutoa taarifa kama hizo.

" >
Kutoa lugha chafu ni ukiukwaji wa maadili. Ndani ya Bunge kuna Kamati ya Maadili ambayo ipo kwa ajili ya kuwawajibisha wabunge wanaotoa lugha chafu. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa upande wake ilifanya semina kwa wabunge ili kuwakumbusha mipaka ya utendaji kazi na maadili kwa ujumla, na tangu wakati huo matumizi ya lugha chafu bungeni yamepungua kwa kiasi kikubwa.

" >