JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS – SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

Rais Samia arejesha Tamko lake Sekretarieti ya Maadili.
27 Oct, 2023
Rais Samia arejesha Tamko lake Sekretarieti ya Maadili.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. SamiaSuluhu Hassanamerejesha Tamko lake la Raslimali na Madenikatika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma Makao Makuu JijiniDodoma mapema wiki hii.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili, Kamishna wa Maadili Jaji wa Rufani Mhe.Sivangilwa Mwangesi amempongeza Mhe Rais kwa kuonyesha anaongoza kwa vitendo na kwa mfano na pia kwa kulipa umuhimu wa pekee takwa hilo la kisheria.

“Tunajua Mhe. Rais ana majukumu mengi lakini ameweza kulitekeleza takwa hilo la kikatiba na kisheria kikamilifu”.

Aidha Mheshimiwa Mwangesi ametoa wito kwa Viongozi wote wa Umma wanaowajibika na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma kurejesha matamko yao kwawakati ambapo amesema kuwa Kiongozi anatakiwa kurejesha tamko lake kabla au ifikapo tar 31 Desemba.

“Kama Rais wa nchi ametekeleza takwa hilo la kikatiba na kisheria kwa wakati nawasihi viongozi wengine kufanya hivyo kwani umebaki mwezi mmoja tu mpaka kufikia tarehe ya mwishoya kutekeleza takwa hilo kwa mujibu wa sharia”.

Kwa mujibu wa Mhe. Mwangesi Kiongozi wa umma kutorejesha Tamko la Rasilimali na Madeni ni kosa kwa mujibu wa kifungu cha 15 cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 13 ya mwaka 1995.

Mhe. Mwangesi alizitaja hatua zinazoweza kuchukuliwa kwa kiongozi wa umma ambaye atashindwa kutekeleza takwa hilo la kisheria ni pamoja na kutakiwa kutoa sababu na inapobainika kuwa sababu alizozitoa sio za msingi basi Sekretarieti ya Maadili humfikisha kiongozi huyo mbele ya Baraza la Maadili.

Amefafanua kuwa hadi kufikia tarehe 30 mwezi Novemba jumla ya Viongozi 161kati ya Viongozi zaidi ya 15,000 wanaopaswa kutoa matamko walikuwa wamerejesha matamko yao na kwamba idadi hiyo ni ndogo ikilinganishwa na idadi ya viongozi wote wanaotakiwa kurejesha matamko yao.

Ni takwa la Kisheria kwa Kiongozi wa Umma kurejesha Tamko la Raslimali na Madeni yake kuanzia tarehe1 Octoba hadi tarehe 30 Desemba kila mwaka.

Mhe. Mwangesi alitumia fursa hiyo kuujulisha umma juu ya tukio la Maadhimisho ya Siku ya Maadili Duniani ambayo kitaifa yatafanyika Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Mnazi Mmoja tarehe 10 Desemba, 2021.

Online Help
Kuanzisha Enzi Mpya katika Udhibiti wa Sekta ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania
Ofisi ya maadili inafanya kazi na imewashughulikia viongozi wengi sana kupitia Baraza la Maadili ambalo pia liliendeshwa mwaka 2013 Novemba mkoani Tabora. Viongozi mbalimbali waliokuwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili waliitwa kwenye Baraza na kuhojiwa na Baraza linatoa mapendekezo na kuyawasilisha mapendekezo hayo kwa Rais kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu na kisheria kwa viongozi husika.

" >
Kifungu cha 11(1) cha Sheria ya Maadili kimeainisha wazi mali zinazotakiwa kutajwa kuwa ni fedha taslimu, fedha zilizopo katika taasisi za kifedha kama vile benki, hisa, nyumba, mashamba, magari, mitambo na mali nyinginezo. Kiongozi anatakiwa kutoa tamko la mali anazomiliki yeye mwenyewe, mke/mume na watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane. Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni zinatakiwa kujazwa kila mwaka na kiongozi hutumiwa fomu hizo na Ofisi ya Maadili na pia zinapatikana katika mtandao wa maadili yaani www.ethicssecretariat.go.tz. Sheria inamtaka kiongozi kutolea tamko madeni yake ili kuweza kujua kuwa kiongozi anamiliki mali zipi na pia kutambua kuwa amezipata vipi mali hizo ukilinganisha na kipato cha kiongozi husika. Kiongozi kuwa na mali nyingi si dhambi kwani hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetamka wazi kuwa kila raia ana haki ya kumiliki mali ila ofisi inataka kujiridhisha uhalali wa jinsi mali ilivyopatikana. Mapendekezo katika Katiba mpya yanasisitiza maadili kwa kutenganisha uongozi na biashara.

" >
Wananchi wengi wamejijengea dhana kuwa bila pesa huwezi kupata huduma ya kiserikali kitu ambacho si kweli kwani huduma nyingi za kiserikali zinatolewa bure kabisa ila cha msingi wananchi wanatakiwa kutoa taarifa katika vyombo husika pindi wanapotakiwa kulipia huduma ambazo zinatolewa bure. Jamii inatakiwa kubadilika na kuamini kuwa si lazima kutoa rushwa ndipo upate huduma. Wapo wananchi wengi ambao walileta malalamiko kama hayo na Ofisi ya Maadili iliyashughulikia, hivyo wananchi wasisite kutembelea Ofisi zetu kwa ajili ya kutoa taarifa kama hizo.

" >
Kutoa lugha chafu ni ukiukwaji wa maadili. Ndani ya Bunge kuna Kamati ya Maadili ambayo ipo kwa ajili ya kuwawajibisha wabunge wanaotoa lugha chafu. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa upande wake ilifanya semina kwa wabunge ili kuwakumbusha mipaka ya utendaji kazi na maadili kwa ujumla, na tangu wakati huo matumizi ya lugha chafu bungeni yamepungua kwa kiasi kikubwa.

" >