Rais Samia aliagiza Baraza la Maadili kuanza kazi kwa kuangalia kesi za maadili katika utumishi wa umma.

Rais Samia aliagiza Baraza la Maadili kuanza kazi kwa kuangalia kesi za maadili katika utumishi wa umma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka wajumbe wa Baraza la Maadili kuanza kazi mara moja kwa kuangalia kesi za maadili zilizoko katika utumishi wa umma zitakazo wasilishwa katika Baraza hilo.
Amesema hayo baada ya kuwaapisha wajumbe wa Baraza la Maadili Aprili2, 2022 katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.
Wajumbe wa wa baraza hilo walioapishwa ni Mwenyekiti wa Baraza Jaji (Mst) Mhe. Ibrahimu Mipawa, Bw. Peter Ilomo na Bi Suzan Mlawi. Hafla hiyo iliudhuriwa pia na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
Kwamujibu wa Mhe. Rais, “mambo mengi yanatokea serikalini kwasababu hakuna Baraza la Maadili, hivyo nimeona muape na muanze kazi.”
Alieleza kuwa kesi nyingi za watumishi wa umma zinapelekwa katika taasisi nyingine za umma badala yakusikilizwa na Baraza kutokana na Baraza kutokuwepo.
“Sijawahi kupokea taarifa ya Baraza. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma inafanyaje kazi kamaBaraza lililoteuliwa mwaka 2019 halijaapa? Nimeona muape na kuanza kazi.”