JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS – SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS. MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA ATEMBELEA OFISI YA RAIS, SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA.
23 Aug, 2024
NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS. MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA ATEMBELEA OFISI YA RAIS, SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Clement Sangu amesema suala la maadili ndiyo  silaha na kila kitu katika jamii na kwamba maadili ni suala mtambuka ambalo linatakiwa kuanzia ngazi ya familia mpaka kwenye utumishi wa umma.

Mhe. Waziri amesema hayo alipotembelea ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma makao makuu jijini Dodoma  tarehe 23 Agosti, 2024 ikiwa ni mara yake ya kwanza kutembelea ofisi hizo tangu ateuliwe kushika wadhifa wa Naibu Waziri.

“Maadili ni tuzo kubwa katika Taifa letu, ndio maana kila mahali unapopita, maadili yanapewa kipaumbele kwasababu ni jambo mtambuka,” alisema.

Mhe. Sangu katika hotuba yake ameipongeza Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kufanya kazi kwa weledi na kufanya kazi kwa kuzingatia misingi ya maadili.

Ameitaja misingi hiyo kuwa ni kuzingatia utaalam, kuwa mwadilifu na kutimiza wajibu.

“Misingi hii isipozingatiwa usababisha uvunjifu wa sheria, mienendo isiyofaa na utovu wa nidhamuazi,” amesema.

Aidha, Mhe. Sangu ametoa rai kwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kutumia mbinu za kisasa katika utendaji wake wa kazi hasa zoezi ila uhakiki wa mali na madeni ya viongozi.

“Tumieni mbinu za kisasa za kiuchunguzi mnapo hakiki mali za viongozi  katika kufuatilia vitendo vya ukiukwaji wa Maadili kwa viongozi wa umma. Hili zoezi linaweza kufanyika vizuri kwa kutumia TEHAMA.”

Katika hatua nyingine, Mhe. Sangu amesema, kuanzishwa kwa mfumo mpya wa ujazaji wa matamko kwa njia ya mtandao (On line Decrelation Systerm) kutasaidia kupata ukweli na uhalisia wa matamko ya viongozi wa umma kwa urahisi na usahihi na kuondokana na mzigo uliokuwepo wa mlundikano  wa makaratasi kama ilivyokuwa hapo awali na kwamba suala hili liwe endelevu na lipewe kipaumbele kwa uzito wake.

“Pamoja na mfumo huu, fanyani utafiti kuhusu hali ya maadili nchini na kuwachukulia hatua viongozi wote wanaokiuka maadili ikiwemo wanaotoa matamko ya uongo. Hawa wapelekeni kwenye Baraza la Maadili,” alisema.

Awali akimkaribisha Mgeni rasmi Katibu Idara ya Ukuzaji Maadili Bw. Waziri Kipacha aliyataja majukumu ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuwa ni pamoja na  Kupokea matamko ya raslimali na madeni, Kupokea malalamiko kuhusu ukiukwaji wa maadili kutoka kwa wananchi, Kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma au malalamiko dhidi ya kiongozi, Kufanya uhakiki wa raslimali na madeni ya viongozi wa Umma, Kutoa elimu ya maadili kwa viongozi wa umma, Kufanya utafiti kuhusu hali ya maadili nchini na Kubuni mikakati ya  kukuza uadilifu nchini.

Kikao hicho kilichojumuisha watumishi wote wa Sekretarieti ya Maadili Makao Makuu na ofisi ya Kanda ya Kati, kilifanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma jijini Dodoma.

 

Online Help
Kuanzisha Enzi Mpya katika Udhibiti wa Sekta ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania
Ofisi ya maadili inafanya kazi na imewashughulikia viongozi wengi sana kupitia Baraza la Maadili ambalo pia liliendeshwa mwaka 2013 Novemba mkoani Tabora. Viongozi mbalimbali waliokuwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili waliitwa kwenye Baraza na kuhojiwa na Baraza linatoa mapendekezo na kuyawasilisha mapendekezo hayo kwa Rais kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu na kisheria kwa viongozi husika.

" >
Kifungu cha 11(1) cha Sheria ya Maadili kimeainisha wazi mali zinazotakiwa kutajwa kuwa ni fedha taslimu, fedha zilizopo katika taasisi za kifedha kama vile benki, hisa, nyumba, mashamba, magari, mitambo na mali nyinginezo. Kiongozi anatakiwa kutoa tamko la mali anazomiliki yeye mwenyewe, mke/mume na watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane. Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni zinatakiwa kujazwa kila mwaka na kiongozi hutumiwa fomu hizo na Ofisi ya Maadili na pia zinapatikana katika mtandao wa maadili yaani www.ethicssecretariat.go.tz. Sheria inamtaka kiongozi kutolea tamko madeni yake ili kuweza kujua kuwa kiongozi anamiliki mali zipi na pia kutambua kuwa amezipata vipi mali hizo ukilinganisha na kipato cha kiongozi husika. Kiongozi kuwa na mali nyingi si dhambi kwani hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetamka wazi kuwa kila raia ana haki ya kumiliki mali ila ofisi inataka kujiridhisha uhalali wa jinsi mali ilivyopatikana. Mapendekezo katika Katiba mpya yanasisitiza maadili kwa kutenganisha uongozi na biashara.

" >
Wananchi wengi wamejijengea dhana kuwa bila pesa huwezi kupata huduma ya kiserikali kitu ambacho si kweli kwani huduma nyingi za kiserikali zinatolewa bure kabisa ila cha msingi wananchi wanatakiwa kutoa taarifa katika vyombo husika pindi wanapotakiwa kulipia huduma ambazo zinatolewa bure. Jamii inatakiwa kubadilika na kuamini kuwa si lazima kutoa rushwa ndipo upate huduma. Wapo wananchi wengi ambao walileta malalamiko kama hayo na Ofisi ya Maadili iliyashughulikia, hivyo wananchi wasisite kutembelea Ofisi zetu kwa ajili ya kutoa taarifa kama hizo.

" >
Kutoa lugha chafu ni ukiukwaji wa maadili. Ndani ya Bunge kuna Kamati ya Maadili ambayo ipo kwa ajili ya kuwawajibisha wabunge wanaotoa lugha chafu. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa upande wake ilifanya semina kwa wabunge ili kuwakumbusha mipaka ya utendaji kazi na maadili kwa ujumla, na tangu wakati huo matumizi ya lugha chafu bungeni yamepungua kwa kiasi kikubwa.

" >