MKUU WA MKOA WA MARA AMEWATAKA VIONGOZI WA UMMA KUTOA MATAMKO YAO YA RASLIMALI NA MADENI KWA WAKATI.i

Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi ametoa wito kwa Viongozi wa Umma mkoani humo n kutoa matamko yao ya Raslimali na Madeni kwa wakati hasa katika kipindi hiki tunapokaribia mwisho wa mwaka kwa lengo la kuweka uwazi na kudhibiti matumizi mabaya ya madaraka.
Kanali Mtambi ametoa wito huo alipokuwa akifungua mafunzo kuhusu Maadili ya Viongozi wa Umma yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa mkoani Mara tarehe 17 Desemba 2024.
“Tuko mwishoni mwa mwaka ambapo viongozi wote wa Umma wanapaswa kutoa kutoa matamko yao kwa mwaka 2024 ili kukidhi matakwa ya kisheria.”amesema.
Aidha Kanali Mtambi katika hotuba yake alifafanua kuwa mafunzo haya yataongeza nidhamu na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu serikalini pia ni kielelezo cha dhamira ya Serikali ya awamu ya sita ya kuhakikisha kuwa suala la Maadili, Uadilifu na Uwajibikaji unaeleweka kwa wadau wote wa sekta ya Umma pamoja na sekta binafsi.
Ameongeza kuwa Maadili yana umuhimu mkubwa katika kujenga Imani ya Wananchi kwa viongozi wa Serikali kuhakikisha kuwa usimamizi wa Raslimali za Umma, kudhibiti mianya ya Rushwa, kuimarisha usimamizi wa sharia, kanuni na taratibu za utumishi wa umma na kudumisha Amani na utulivu na umoja wa kitaifa.
Kanali Mtambi alibainisha kuwa wapo viongozi wa Umma wasio waadilifu wamekuwa wakijihusisha na vitendo vinavyopelekea uwepo wa mgongano wa Maslahi kati ya na Taasisi wanazozisimamia nna kwamba suala hili linapunguza kasi ya ukuaji wa uchumi na kurudisha nyuma juhudi za Serikali za utoaji huduma kwa jamii.
Mafunzo hayo yaliwashirikisha Viongozi wa Umma wa Mkoa wa Mara wakiwemo wakuu wa Idara na Vitengo, Waheshimiwa Madiwani ambapo mada mbili zilijadiliwa ambazo ni Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma pamoja Ujazaji wa Matamko ya Raslimali na Madeni kwa njia ya Mtandao. (Online Decralation System-ODS).