MKURUGENZI TACAIDS AFIKISHWA MBELE YA BARAZA LA MAADILI KWA TUHUMA ZA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA

Mkurugenzi Tathimini na Ufuatiliaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI nchini (TACAIDS) amefikishwa mbele ya Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma jijini Dodoma kwa makosa mawili likiwemo la matumizi mabaya ya matumizi ya madaraka na rasilimali za umma.
Dkt. Jerome Philip Kamwela anadaiwa kutenda kosa hilo tarehe 5/6/2019 majira ya saa 8 usiku maeneo ya Mbezi Beach katika halmashauri ya wilaya Kinondoni, Dar es Salaam.
Hata hivyo, taarifa za ajali hiyo zilitolewa na mlalamikiwa tarehe 23/9/2019 baada ya mwajili kupata malalamiko kutoka jeshi la polisi wilaya ya Kinondoni.
Wakili wa Serikali Fikiri Ngakonda alidai kuwa, “mnamo tarehe 5/6/2019 majira ya saa 8 usiku katika eneo la Mbezi Beach, Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam mtuhumiwa alitumia gari ya ofisi yenye namba za usajili DFPA 2055 Toyota Land Cruser Prado kinyume na taratibu na kusababisha ajali kwa kugonga mnazi uliopo katika uzio wa nyumba ya Bi. Josephine Kombo na kuleta uharibifu wa gari na ukuta wa nyumba.”
Wakili Ngakonda ametaja kosa la pili kuwa ni kushindwa kutoa taarifa mahali popote kuhusu tukio hilo kinyume na taratibu za matumizi ya magari ya umma.
“Dkt. Kamwela baada ya kusababisha ajali bila sababu ya msingi hakutoa taarifa ya tukio hilo katika kituo chake cha kazi wala polisi kinyume na kifungu cha 6(1)(a) cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma,” amesema.
Wakili Ngakonda alidai mbele ya Baraza kuwa kitendo hicho ni kinyume na matakwa ya vifungu vya 12(1)(d) na 6(1)(a) vya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya mwaka 1995, na hivyo kukiuka maadili ya viongozi wa umma kwa mujibu wa kifungu cha 6(2).
Imedaiwa mbele ya Baraza kuwa kibali cha gari hilo kinamtaka mtumiaji kutumia gari kwa matumizi ya umma ikiwemo kutoka nyumbani hadi kazini ama akitekeleza matujukumu ya umma wakati wa kazi ndani ya Dar es Salaam.
Hata hivyo, pamoja na mtuhumiwa kukana kosa, alikili kuwa alipata ajali kama Baraza lilivyoelezwa.
Dkt. Kamwela amelieleza Baraza kuwa, “Ni kweli nilipata ajali siku tajwa na nililifanyia gari matengenezo kama jambo la dhalula kwasababu yalikuwa madogo.”
Aliongeza kuwa, “dereva yeyote anaweza kupata ajali. Sikupata ajali kwasababu ya ukiukwaji wa maadili wala sikuwa na nia ovu.”
Alipoulizwa na Wakili wa Serikali kwanini hakutoa taarifa za tukio hilo kwa mwajili wake na katika jeshi la polisi kama taratibu zinavyoelekeza, Dkt. Kamwela alisema, “sikutoa taarifa mahali popote kwasababu madhara yalikuwa madogo.