JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS – SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

MKURUGENZI PSSF AFIKISHWA MBELE YA BARAZA LA MAADILI
27 Oct, 2023
MKURUGENZI PSSF AFIKISHWA MBELE YA BARAZA LA MAADILI

Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Bw. Ernest Khisombi Septemba 12, 2022amefikishwa mbele ya Baraza la Maadili kwa tuhuma za kujipatia mkopo wa gari binafsi wenye thamani ya Shilingi 196,570,931.00 kinyume na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya mwaka 1995.

Akisoma mashtaka mbele ya Baraza la Maadili, Wakili wa Serikali Bw. Hassan Mayunga ameliambia Baraza kuwa, mtuhumiwa anashtakiwa kwa makosa mawili ambayo ni kukopa fedha za mfuko kiasi cha shilingi 117,808,470.00 bila kufuata utaratibu.

Katika lalamiko hilo Na. 5 la mwaka 2022, kosa la pili ni kulipiwa kodi kiasi cha shilingi 78,762,461.00 bila kufuata utaratibu wa Sera ya Mikopo ya PSSSF.

Kwa mujibu wa Bw. Mayunga, kitendo hicho kinamfanya Bw. Khisombi ambaye ni Kiongozi wa Umma kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma kushidwa kutimiza matakwa ya kifungu cha 6(1)(a) na (b) na hivyo kukiuka maadili ya viongozi wa umma kwa mujibu wa kifungu cha 6(2) cha Sharia ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Hata hivyo, Bw. Khisombi amezikana tuhuma hizo na kulieleza Baraza la Maadili kuwa, “fedha hizi ni ihaki yangu kama Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi kwa mujibu wa Sera ya Mikopo ya Mfuko.”

Shahidi wa mlalamikaji Bw. Gideon Mafwiri ameliambia Baraza kuwa kiongozi huyo alijipatia mkopo kinyume na utaratibu uliowekwa na mfuko wa mikopo wa PSSF.

Mfuko wa mikopo umeweka utaratibu wa ni viongozi wapi wanastahili kulipiwa kodi na mfuko nan i gali la namna gani litalipiwa kodi na mfuko kwa mujibu wa taratibu,” alisema.

Kwa mujibu wa maelezo ya shahidi, utaratibu wa Mfuko ni kuwa maombi ya mkopo yaidhinishwe na Kamati ya Mkopo ya Mfuko, mkopaji kulipia asilimia 5 ya mkopo kabla hajapatiwa mkopo pamoja na kulipiwa kodi gari jipya la kiongozi kwa asilimia 100.

“Sera ya mikopo ukurasa wa 10 inasema mkopo huo outalipiwa asilimia 5 kabla mkopaji hajapatiwa. Utaratibu huu haukufuatwa,” amesema.

Bw. Mafwiri ameeleza kuwa wakati mfuko unalipia kodi ya gari la Bw. Khisombi, gari hilo halikuwa jipya kama Sera ya Mfuko huo inavyoelekeza. Ushahidi wa shauri hilo Na. 5 la mwaka 2022 umekamilika na kufungwa kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Baraza hilo.

Baraza la Maadili lililoanza vikao vyake vya uchunguzi Septemba 6, 2022, limekwisha sikiliza malalamiko mengine kuhusu ukiukwaji wa Sheria ya Maadili ya Viongizi wa Umma dhidi ya Bw. Godfrey Chibulunje aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu katika Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Bw. Hoseah Kashimba, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSF) na Bi. Beatrice Lupi, Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSF).

Baraza hili linaloongozwa na jaji (Msf) Ibrahimu Mipawa na wajumbe Bw. Peter Ilomo na Bi Suzan Mlawi linafanya uchunguzi wa wazi kwa mujibu wa Kifungu cha 25 (5) na 29 (6) cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma (Sura 398).

Online Help
Kuanzisha Enzi Mpya katika Udhibiti wa Sekta ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania
Ofisi ya maadili inafanya kazi na imewashughulikia viongozi wengi sana kupitia Baraza la Maadili ambalo pia liliendeshwa mwaka 2013 Novemba mkoani Tabora. Viongozi mbalimbali waliokuwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili waliitwa kwenye Baraza na kuhojiwa na Baraza linatoa mapendekezo na kuyawasilisha mapendekezo hayo kwa Rais kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu na kisheria kwa viongozi husika.

" >
Kifungu cha 11(1) cha Sheria ya Maadili kimeainisha wazi mali zinazotakiwa kutajwa kuwa ni fedha taslimu, fedha zilizopo katika taasisi za kifedha kama vile benki, hisa, nyumba, mashamba, magari, mitambo na mali nyinginezo. Kiongozi anatakiwa kutoa tamko la mali anazomiliki yeye mwenyewe, mke/mume na watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane. Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni zinatakiwa kujazwa kila mwaka na kiongozi hutumiwa fomu hizo na Ofisi ya Maadili na pia zinapatikana katika mtandao wa maadili yaani www.ethicssecretariat.go.tz. Sheria inamtaka kiongozi kutolea tamko madeni yake ili kuweza kujua kuwa kiongozi anamiliki mali zipi na pia kutambua kuwa amezipata vipi mali hizo ukilinganisha na kipato cha kiongozi husika. Kiongozi kuwa na mali nyingi si dhambi kwani hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetamka wazi kuwa kila raia ana haki ya kumiliki mali ila ofisi inataka kujiridhisha uhalali wa jinsi mali ilivyopatikana. Mapendekezo katika Katiba mpya yanasisitiza maadili kwa kutenganisha uongozi na biashara.

" >
Wananchi wengi wamejijengea dhana kuwa bila pesa huwezi kupata huduma ya kiserikali kitu ambacho si kweli kwani huduma nyingi za kiserikali zinatolewa bure kabisa ila cha msingi wananchi wanatakiwa kutoa taarifa katika vyombo husika pindi wanapotakiwa kulipia huduma ambazo zinatolewa bure. Jamii inatakiwa kubadilika na kuamini kuwa si lazima kutoa rushwa ndipo upate huduma. Wapo wananchi wengi ambao walileta malalamiko kama hayo na Ofisi ya Maadili iliyashughulikia, hivyo wananchi wasisite kutembelea Ofisi zetu kwa ajili ya kutoa taarifa kama hizo.

" >
Kutoa lugha chafu ni ukiukwaji wa maadili. Ndani ya Bunge kuna Kamati ya Maadili ambayo ipo kwa ajili ya kuwawajibisha wabunge wanaotoa lugha chafu. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa upande wake ilifanya semina kwa wabunge ili kuwakumbusha mipaka ya utendaji kazi na maadili kwa ujumla, na tangu wakati huo matumizi ya lugha chafu bungeni yamepungua kwa kiasi kikubwa.

" >