Mkuchika azindua Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu.

Mkuchika azindua Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki zaBinadamu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Mkuchika (Mb) amezindua maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu kitaifa Jijini Dodoma.
Katika Hotubayake Mhe. Waziri alisema kuwaSiku ya Maadili na Haki za Binadamu inayoadhimishwa hapa nchini kila mwakaimetokana na maadhimisho ya siku mbili tofauti ambazo huadhimishwa kitaifa ,yaani Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Rushwa na Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu.
Mhe.Waziri alieleza kuwa jukumu kubwa la Serikali ni kuwaletea wananchi maendeleo hivyo usimamizi wa maadili mema, haki za binadamu na mapambano dhidi ya rushwa linatakiwa kuwa suala endelevu kwa kuwa ndio msingi wa utoaji huduma inayokidhi matarajio ya Umma.
Mhe. Waziri aliendelea kusema kuwa ni dhahiri kwamba Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Dkt John Pombe Mgufuli imefanya kazi kubwa katika kusimamia misingi ya maadili na utawala bora.
Kwa mujibu wa Mhe. Mkuchika juhudi hizo zinatambulika ndani na nje ya nchina kwa miaka ya hivi karibuni nchi yetu imekuwa inatolewa mfano wa nchi zilizofanikiwa sana katika masuala ya uadilifu, mapambano dhidi ya rushwa na matumizi mazuri ya rasilimali za nchi.
“utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uchumi umekuwa ukidumazwa kwa kiasi kikubwa na vitendo vya rushwa na ukiukwaji wa haki za binadamu ambako kunachangiwa na ukosefu wa maadili kwa baadhi ya watendaji katika nyanja zote”.
“Hivyo basi kwa kutambua ukubwa wa changamoto hiyo Serikaliya Awamu ya Tano imekuwa na mikakati mbalimbali inayoainishwa majukumu ya kila sekta ikiwa ni pamoja na Mkakati wa Taifa Dhidi ya Rushwa na Mpango wa Utekelezaji Awamu ya tatu ( National Anti-Corruption Strategy and Action Plan-NACSAP111) uliozinduliwaDesemba 2016”.Alifafanua Mhe. Mkuchika.
Mhe. Mkuchika aliongeza kusema kuwa unapozungumzia haki za binadamu huwezi kuepuka kuzungumzia huduma mbalimbali ambazo mwanadamu huzihitaji katika maisha yake ya kila siku ikiwa ni pamoja na huduma za afya na elimu ambapo upatikanaji wa huduma hizo hapa nchini umeboreshwa na unaendelea kuboreshwa ili kukidhi mahitaji na viwango.
Aidha Mhe. Waziri alimaliza kwa kutoa rai kwa waandishi wa habari kutafsiri na kuonyesha matokeo ya juhudi za Serikali katika kuimarisha Maadili, mapambano dhidi ya rushwa na uzingatiaji wa haki za binadamu.
Kwa mujibu wa Mhe. Mkuchika jambo hili ni muhimu sana wananchi kufahamu na kuifanya jamii nzima kuwa na maadili mema, kuheshimu haki za binadamu na kuchukia na kupiga vita rushwa ili kuiunga mkono azma ya Serikali katika kuimarisha maadili nchini.
Maadhimisho ya mwaka huu yatafanyika kwa kongamano litakalohusisha taasisi zisizo za kiserikali pamoja na wabia wa maendeleo na kauli mbiu itakua “Uzingatiaji wa Ahadi ya Uadilifu kwaViongozi na Watumishi kwa Ustawi wa Utawala Bora na Haki za Binadamu nchini”