JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS – SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

Mhe. SIMBACHAWENE: SEKRETARIETI YA MAADILI NENDENI MKASIKILIZE MALALAMIKO YA WANANCHI.
18 Mar, 2024
Mhe. SIMBACHAWENE: SEKRETARIETI YA MAADILI NENDENI MKASIKILIZE MALALAMIKO YA WANANCHI.

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (Mb) ametoa wito kwa watumishi wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kutoka ofisini kwenda kwa wananchi kusikiliza malalamiko yao na kuyatafutia ufumbuzi badala ya kukaa ofisini kusubiri wananchi wachache wanaolalamikia viongozi.

“Sekretarieti ya Maadili nendeni mkawasilikize wananchi, yapo mambo wanayapigia kelele sana kuhusu tabia na mwenendo wa viongozi wao. Kelele zao zinaposikika tokeni mkawasikilize, hii itasaidia kutatua kero zao  kwa wakati na mtawasaidia pia viongozi kujirudi na kufuata misingi ya maadii,” alisema.

Mhe. Simbachawene alisema hayo jijini Arusha tarehe 18 Machi, 2024 wakati akifungua kikao kazi cha Wachunguzi wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadii ya Viongozi wa Umma.

Kwa mujibu wa Mhe. Waziri, lazima watumishi wa Sekretarieti ya Maadili watoe elimu  kwa umma kuhusu misingi ya maadli ambayo ni pamoja na kufanya kazi kwa kuzingatia sheria kanuni na taratibu za Nchi, kutokutumia mali za umma kwa manufaa binafsi, kuepuka tabia na mienendo isiyofaa nk.

“Misingi hii lazima tuilinde na hili ndilo jukumu letu. Misingi hii isipozingatiwa, wananchi wanakosa huduma na malengo ya nchi hayatafikiwa,” alisema.

Katika hatua nyingine Mhe. Simbachawene alisema jukumu la kusimamia maadili linahitaji mtumishi anayetumia mbinu, busara na weledi wa hali ya juu kutokana na kuwahusu viongozi wakubwa na ni la kikatiba.

“Maadili ni zaidi ya sheria, lazima msimamie maadili ya viongozi wote kuanzia ngazi ya chini. Twende mbali tuanzie ngazi ya chini huko serikali za mitaa kusimamia maadili. Tusihangaike na viongozi wanaojaza fomu za Tamko tu kwasababu lazima kiongozi yeyote lazima awe mwadilifu,” alisema na kuongeza kuwa, “maadili katika jamii zetu ni jambo la msingi na lilikuwepo hata wakati wa ujima.”

Awali akimkaribisha Mhe. Waziri, Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji (Mst.) Sivangilwa Mwangesi alieleza kuwa Taasisi imeona umuhimu wa wachunguzi wote kuwa na kikao cha pamoja kujadili mustakabali wa majukumu yao.

“Hii ni mara yetu ya kwanza tangu Taasisi ilipoanzishwa mwaka 1996 kuwa na kikao kama hiki kwa lengo la kuwakutanisha wachunguzi wote ndani ya Taasisi kujadili kwa kina mambo mbalimbali yanayohusu utendaji wa kazi na mafanikio kwa mujibu wa matakwa ya Ibara ya 132 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977,” alisema.

Kwa mujibu wa kifungu cha 19(2) cha Sheria ya Maadili ya Viongizo wa Umma Na. 13 ya 1995, majukumu ya Sekretarieti ya Maadili ni kupokea malalamiko ya ukiukwaji wa maadili, kufanya uchunguzi, kupokea matamko, kufanya uhakiki na kutoa elimu ya maadili.

Majukumu mengine ni kufanya utafiti wa hali ya uadilifu nchini, kutoa ushauri katika mambo ya uadilifu na kubuni mikakti ya ukuzaji maadili.

Mhe. Sivangilwa alizitaja mada zitakazo wasilishwa kuwa ni; Utendaji katika Ofisi za Kanda, Viambata vya Makosa ya Maadili, Utaratibu wa zoezi la Uhakiki, Mikakati ya utendaji kazi pamoja na Changamoto na utatuzi wake katika kushughulikia malalamiko na uchunguzi.

 

 

 

Online Help
Kuanzisha Enzi Mpya katika Udhibiti wa Sekta ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania
Ofisi ya maadili inafanya kazi na imewashughulikia viongozi wengi sana kupitia Baraza la Maadili ambalo pia liliendeshwa mwaka 2013 Novemba mkoani Tabora. Viongozi mbalimbali waliokuwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili waliitwa kwenye Baraza na kuhojiwa na Baraza linatoa mapendekezo na kuyawasilisha mapendekezo hayo kwa Rais kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu na kisheria kwa viongozi husika.

" >
Kifungu cha 11(1) cha Sheria ya Maadili kimeainisha wazi mali zinazotakiwa kutajwa kuwa ni fedha taslimu, fedha zilizopo katika taasisi za kifedha kama vile benki, hisa, nyumba, mashamba, magari, mitambo na mali nyinginezo. Kiongozi anatakiwa kutoa tamko la mali anazomiliki yeye mwenyewe, mke/mume na watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane. Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni zinatakiwa kujazwa kila mwaka na kiongozi hutumiwa fomu hizo na Ofisi ya Maadili na pia zinapatikana katika mtandao wa maadili yaani www.ethicssecretariat.go.tz. Sheria inamtaka kiongozi kutolea tamko madeni yake ili kuweza kujua kuwa kiongozi anamiliki mali zipi na pia kutambua kuwa amezipata vipi mali hizo ukilinganisha na kipato cha kiongozi husika. Kiongozi kuwa na mali nyingi si dhambi kwani hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetamka wazi kuwa kila raia ana haki ya kumiliki mali ila ofisi inataka kujiridhisha uhalali wa jinsi mali ilivyopatikana. Mapendekezo katika Katiba mpya yanasisitiza maadili kwa kutenganisha uongozi na biashara.

" >
Wananchi wengi wamejijengea dhana kuwa bila pesa huwezi kupata huduma ya kiserikali kitu ambacho si kweli kwani huduma nyingi za kiserikali zinatolewa bure kabisa ila cha msingi wananchi wanatakiwa kutoa taarifa katika vyombo husika pindi wanapotakiwa kulipia huduma ambazo zinatolewa bure. Jamii inatakiwa kubadilika na kuamini kuwa si lazima kutoa rushwa ndipo upate huduma. Wapo wananchi wengi ambao walileta malalamiko kama hayo na Ofisi ya Maadili iliyashughulikia, hivyo wananchi wasisite kutembelea Ofisi zetu kwa ajili ya kutoa taarifa kama hizo.

" >
Kutoa lugha chafu ni ukiukwaji wa maadili. Ndani ya Bunge kuna Kamati ya Maadili ambayo ipo kwa ajili ya kuwawajibisha wabunge wanaotoa lugha chafu. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa upande wake ilifanya semina kwa wabunge ili kuwakumbusha mipaka ya utendaji kazi na maadili kwa ujumla, na tangu wakati huo matumizi ya lugha chafu bungeni yamepungua kwa kiasi kikubwa.

" >